Listen

Description

Leo kwa bahati nzuri tumepata fursa ya kuzungumza na Catherine Ruge, Katibu wa Baraza la Wanawake CHADEMA (BAWACHA), lakini pia mbunge mstaafu wa viti maalumu kupitia tiketi ya CHADEMA kwa Jimbo la Serengeti. Mnamo mwaka 2020, Ruge aligombea ubunge wa jimbo la Serengeti kupitia tiketi ya CHADEMA. Na leo, kwa bahati nzuri, tumebahatika kumualika kwenye Podcast yetu hii kuzungumzia, sana sana, harakati zake za kisiasa na mustakabali mzima wa BAWACHA na CHADEMA kwa ujumla na hali ya siasa zetu za nchi kwa sasa.