Dini ina mchango mkubwa sana katika uendeshaji wa nchi. Mbali na kushuhudia shule, vituo vya afya na hospital na vyuo vikuu vinavyojengwa na kuendeshwa na taasisi mbali mbali za dini nchini Tanzania, tumekuwa tukishuhudia pia namna ambavyo viongozi wa dini wamekuwa wakipaza sauti zao kutoa muelekeo wa kisiasa, kiuchumi, na hata kidiplomasia ambao Tanzania inapaswa kuufuata.
Kuweza kujadili mambo haya kwa ujumla na nini mchango wa taasisi ya dini katika kujenga taifa la haki na kidemokrasia, tunayofuraha kubwa sana kuungana na Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Karagwe, Dk Benson Bagonza