Listen

Description

Dar es Salaam. Mnamo Disemba 9, 2021, Tanganyika inatimiza miaka 60 tangu ipate uhuru wake kutoka kwa Waingereza tarehe kama hiyo mwaka 1961. Tukiwa tunaelekea kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika, tunayofuraha ya kujumuika na Spika mstaafu na kada maarufu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mzee Pius Msekwa.

Pamoja na mambo mengine, Mzee Msekwa alikuwepo wakati Tanganyika inajipatia uhuru wake na hivyo kumuwezesha kushuhudia mabadiliko mengi ya kisiasa, kiuchumi na kijamii ambayo Tanganyika, na baada ya Muungano na Zanzibar mwaka 1964, Tanzania, imeyapitia katika kipindi hiki cha miaka 60.

Kitu cha kwanza ambacho The Chanzo ilitaka kufahamu kutoka kwa Mzee Msekwa ni tathimini yake ya safari hii ya miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika