Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Tanzania azungumzia mvutano kati ya wenye maduka na wamachinga Kariakoo
Katika mahojiano maalumu na The Chanzo leo, Septemba 9, 2021, Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Tanzania Ludovick Kiondo amesema kwamba wamachinga wanatumika kama mtaji wa kura bila kujali mapato ya nchi.
Kiondo amesema hayo kufuatia tahuruki iliyojitokeza Kariakoo, Dar es Salaam, leo Alhamisi kati ya mwenye duka mmoja aliyetaka wamachinga kuondoka mbele ya duka lake na wamachinga kugoma kufanya hivyo.
Taharuki hiyo iliyodumu kwa dakika kadhaa imemfanya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla kumuagiza Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng’wilabuzu Ludigija kuandaa kikao kati ya Serikali, wenye maduka na wamachinga kutafuta namna za kuepusha taharuki kama hiyo kutokea tena.