Listen

Description

Sheria Na. 12 ya mwaka 2003 iliyoianzisha TCRA inaipa Mamlaka wajibu katika majukumu mbalimbali ikiwemo; kukuza ushindani bora na uchumi wenye tija; kulinda maslahi ya watumiaji; kulinda mitaji ya Watoa Huduma wenye ufanisi; kukuza upatikanaji wa huduma zinazodhibitiwa kwa watumiaji wote wakiwamo wenye kipato kidogo, walioko vijijini na watumiaji walio na walioko katika mazingira magumu; pamoja na kuimarisha Elimu kwa Umma, uelewa na ufahamu  wa huduma zinazosimamiwa na TCRA.

Meneja wa TCRA, Ofisi ya Zanzibar anatueleza utekelezaji wa majukumu haya kwa kina katika ofisi za TCRA.

Kwa maoni na mapendekezo, tafadhali wasiliana nasi kupitia 0800008272 au tuandikie dawatilahuduma@tcra.go.tz

#NiRahisiSana!