Listen

Description

Mambo vipi, kwenye toleo hili nimezungumza na Billy Patrick yeye amehudumu kama Google Developer Student Club Lead katika chuo cha Uhasibu Arusha (IAA). Nilipenda kufahamu mchakato mzima wa kuomba nafasi hiyo, ushirikiano aliopata kwa uongozi wa chuo na wanafunzi, na vipi kuhusu changamoto alizopitia.

Billy amenieleza Google Developer Student Club ni nini, namna inavyofanya kazi pia namna ya kufanya applicaion. Walengwa wa Google Developer Student Club ni kina nani.

Billy amenijulisha kwa mwaka 2019/2020 ni chuo cha Uhasibu Arusha pekee hapa Tanzania ndio kilikuwa na Google Developer Student Club. Hii inafanya Billy yeye kuwa Google Developer Student Club Lead wa kwanza kwa vyuo hapa Tanzania.

Billy ameniambia, kwa mwaka 2020/2021 kuna vyuo vitano, nadhani haya ni maendeleo makubwa katika kujenga developers wa kiwango hapa Tanzania.

Billy amenieleza alipata ushirikiano wakutosha kwenye chuo cha Uhasibu Arusha, big shout out kwa chuo cha Uhasibu Arusha kwa support kubwa hii maana waliweza toa hata Computer Lab kwa Google Developer Student Club.

Billy ameniambia mengi ikiwa ni pamoja na majukumu sasa ya Google Developer Student Club Lead na pia changamoto walizopitia. Pia amenipa faida alizopata katika kipindi chake alichohudumu kama Lead, na nini atafanya sasa baada ya kumaliza muda wake.

Ninahamasika vya kutoka na hamasa aliyotupa Billy, nimefurahishwa na namba ya vyuo vingine kuongezeka kujiunga na Google Developer Student Club. Vilevile hamasa ametoa kwa vyuo vingine kuweza support jitahada kama hizi kuweza andaa developers kwa kuweza jifunza Technolojia mbalimbali. 

Fuatilia sasa uweze kusikiliza haya na mengine mengi kutoka kwa Billy.

Host: Yesaya R. Athuman