Ebwana mambo vipi, jina lamgu ni Yesaya, ninakuletea mfululizo wa vipindi kwa njia ya sauti yaani Podcast. Dhumuni langu ni kukuelimisha, kukuhabarisha na kukuletea mijadala mbalimbali kuhusu Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na mimi nitajikita zaidi kwenye mifumo ya kompyuta.
Leo tutazungumza kuhusu viashiria vitakavyokusukuma kutumia ChatBot. Nimetoa mifano mbalimbali ya makampuni yanatumia ChatBot, kama CNN, Whole Food, Mwananchi Magazine, eShangazi, UBA Bank na KLM Royal Dutch Airlines. Ungana pamoja nami sasa unaweza pata tafsiri ya ChatBot kutoka katika mazungumzo haya.
Host: Yesaya R. Athuman