Ukiachana na neno lake, zipo kanuni (siri) ambazo Mungu ameziweka kwa watu wake ili wamjue. Mithali 25:2 Anasema, '' Ni utukufu wa Mungu kuficha jambo;Bali ni utukufu wa mfalme kuchunguza jambo''. Andiko hili linatuthibitishia kwamba yako mambo ambayo ili umjue Mungu utatakiwa kuingia ndani ya kuchungza. Nina amini kupitia somo hili, neema ya Mungu itakupa kujua siri ambazo wengine wamezijua na wakatembea na Mungu kwa nguvu isiyo ya kawaida.