KLINIKI YA BABA MAMA NA MTOTO.
Karibu kliniki ya Baba, Mama na Mtoto
Kliniki hii imekusudia zaidi kuangazia namna Mahusiano ya wazazi kabla, wakati na baada ya mtoto kuzaliwa yanavyoweza kuathiri Afya ya Akili ya Mtoto kwa siku za Usoni. Kadhalika tutaangazia vihatarishi na kadhia nyinginezo mtambuka ambazo kwa namna moja au nyingine zinawaweka watoto wetu katika hatari ya kupata changamoto za Afya ya Akili.
Ni matumaini yetu kuwa utajifunza pamoja nasi na pia utachukuwa jukumu la kusambaza maarifa haya kwa kadiri utakavyoweza. Bilas haka wema wowote utakaoufanya utapata fungu lako. Inawezekana usiweze kumfikia kila mtoto ili umsaidia lakini kupitiwa maarifa haya unaweza kumgusa kila mtoto aliyezaliwa leo, jana na hata atakayezaliwa kesho.
MTA S02 - FATHER MOTHER AND CHILD CLINIC. (TRAILER)
Welcome to the Father, Mother and Child clinic
This clinic is more intended to highlight how the parents' relationships before, during and after the child is born can affect the mental health of the child in the future. Likewise, we will highlight risks and other cross-cutting issues that in one way or another put our children at risk of experiencing Mental Health challenges.
It is our hope that you will learn with us and will also take responsibility for spreading this knowledge as much as you can. Bilas haka whatever good you do you will get your share. You may not be able to reach every child in order to help them, but through this knowledge you can touch every child born today, yesterday and even those born tomorrow.