Kanuni kubwa inayoendesha maisha ya watu kiujumla ni kanuni ya mahusiano. Kila kitu kwenye maisha kinategemea kanuni hii ya msingi. Namna mtu anavyohusiana na watu kwenye maisha yake inatengeneza mazingira ya mtu huyo kufanikiwa ama kufeliWakati wa chuo kadhalika tunapata fursa mbalimbali za kukutana na kuhusiana na watu wa aina mbalimbali. Kwa sehemu kubwa kufanikiwa au kufeli kwa mwanafunzi awapo chuoni kunategemeana na aina ya mahusiano na watu anaojihusisha nao