Walipoanza Men Men Men The Podcast mwishoni mwa mwaka 2019, Michael na Nadia walikuwa wawili tu – na maikrofoni. Hakukuwa na studio ya kitaalamu, wala mpango mkubwa. Kulikuwa tu na wazo moja: kuanzisha mazungumzo ya kweli kuhusu afya ya akili ya wanaume.
Hawakujua kama kuna mtu atawasikiliza. Hawakujua kama kuna yeyote atajali kuhusu maongezi haya. Lakini leo hii, baada ya miaka mitano na episodes 100, imekuwa wazi kuwa podcast hii imekuwa zaidi ya wao wawili. Imebeba sauti za uchungu, ushindi, maswali magumu, na ukweli ambao mara nyingi husalia kimya.
Katika episode hii ya kipekee, Michael na Nadia wanarudi walipoanzia – si kwa kurudia, bali kwa kutafakari. Wanazungumza kwa uhalisia kuhusu safari yao, changamoto walizokumbana nazo, na yale ambayo bado ni vita ambayo wanapigana nayo hadi leo.
Wanajiuliza: Je, bado wana kiu ya mabadiliko kama siku ya kwanza? Je, bado wanaamini kuwa mazungumzo haya ni muhimu katika jamii?
Jibu lao ni NDIO. Na kama wewe pia bado unaamini hivyo, basi episode hii ni kwa ajili yako pia.