Look, Princely anaendesha kampuni nzuri inayofanya vizuri kibiashara, kampuni yake ilishinda shindano na wakapata hela nzuri tu ya kumwezesha yeye kuendelea kutimiza ndoto zake. Anaishi kwenye eneo zuri, na ni mtu poa sana. Hawezi kuwa na tatizo, na afya yake ya akili haiwezi kuwa challenged, right? WRONGUkweli ni kwamba, si mara zote tuonekanavyo nje ndiyo tulivyo kwa ndani. Unaweza onekana kwamba una kila kitu nie, ila bado afya ya akili isiwe katika mahali sahihi. Inakuathiri vipi? Unatambuaje hilo? Unapambana halo kwa namna gani? Haya ni maongezi na Princely Glorious, mwanaume aliyeamua ku-share na sisi experience yake kwenye hili