Listen

Description

Tatizo la nguvu za kiume ni tatizo gani? Linaathiri wanaume wangapi duniani? Chanzo cha hili tatizo ni nini? Matumizi ya dawa za asili kama “Vumbi la Congo” na “Al Kasusi” ni kweli yanasaidia kutatua tatizo hili? Ni tatizo linalotibika? Kuna madaktari wanaoweza kusaidia kwenye hili tatizo? Linahusiana vipi na afya ya akili? Mbona mara nyingine hili tatizo kama linapotea na mara nyingine kama linarudi? Kuna suluhisho la kudumu?

Haya ni baadhi ya maswali ambayo wanaume wengi sana hujiuliza kuhusiana na “Nguvu za Kiume”. Katika nia ya kujenga na kuboresha afya ya akili kwa wanaume, episode hii imeamua kuzungumzia hili tatizo kwa undani tukiwa na matumaini kwamba kwa yeyote atakayesikiliza basi ataweza kupata taarifa za kina na taarifa sahihi.

Michael pamoja na Nadia wamefanya mazungumzo ya kina na “Urologist” kutoka Tanzania, Dr Boio Nyamwihura ili kupata ukweli na taarifa zaidi kutusu mwanaume na “nguvu za kiume”