Listen

Description

Kutana na Tito Magoti, mwanasheria kijana kutoka Tanzania. Mwaka 2019, alijikuta gerezani ambapo alikaa kwa zaidi ya mwaka mmoja. Sasa Tito ametoka, anaendelea na maisha yake.Unahitaji nini ili uweze ku “survive” maisha ya gerezani? Watu wako wanaokuzunguka inabidi wafanye nini ili waweze endelea kukutia moyo? Nini kilichompa Tito nguvu na moyo wa kuishi gerezani na kumfanya asikate tamaa ya maisha? Baada ya kutoka gerezani, jamii imempokeaje Tito? Yupo tayari kuishi maisha ya mtu anayeangaliwa sana na jamii kila anapokwenda? Gerezani kumembadilisha vipi Tito? Na zaidi ya yote, vipi kuhusu afya ya akili magerezani?Maswali ni mengi sana kutoka kwa Michael Baruti pamoja na Mwanasaikolojia Nadia Ahmed, karibu usikilize maongezi haya.