Umeshawahi kutaka kufanya kitu ambacho wewe mwenyewe kwa dhati kabisa kutoka moyoni mwako unafahamu kwamba ni ndoto yako na unatamani sana kuitimiza ila watu wanaokuzunguka wasilione hilo wala kukubaliana nalo? Ulifanya nini? Uliweza kukomaa na kutimiza ndoto zako au uliamua kuua ndoto zako na kuishia kufanya kile ambacho kila mtu alikwambie ufanye?
Inahitaji ushujaa, uvumilivu na commitment ya hali ya juu ili kuweza kutimiza ndoto zako, na inakua ngumu zaidi pale ambapo jamii, familia na watu wake wa karibu wanaokuzunguka wanaposhindwa kuamini na kukusaidia kutimiza ndoto ulizonazo.
Phineas Steven kutoka “Unmatched Basketball” anajua vizuri sana kuhusu yote haya, Ila haikumzuia yeye kwenda mbele ili kuhakikisha ndoto yake inatimia. Karibu usikilize maongezi yake, karibu usikilize “unmatched mindset” yake ilivyomfikisha hapa alipo