Mahusiano huisha, na mara nyingine pia ndoa huvunjika. Si vitu ambavyo tunafurahia vikitokea ila uhalisia wa maisha ndivyo ulivyo. Swali ni pale tu, vipi ndoa ikivunjika wakati tayari kuna mtoto ambaye ni zao la ndoa hiyo ni nini kifanyike ili wazazi wote wawili waweza kuwa na haki sawa juu ya mtoto au watoto wao?
Michael na Nadia wameketi pamoja na J (si jina lake halisi) wakijadili namna mwisho wa mahusiano ya ndoa yake kulivyokua chanzo cha yeye kutopata nafasi ya kuwa baba kwa namna ambayo angependa kuwa baba kwa mtoto wake
J anawakilisha wanaume wengine kwenye mazungumzo haya, ambao kwa namna moja au nyingine wangependa kuhusika kwenye maisha ya watoto wao, ila kutokana na namna mahusiano yao na wenzi wao au namna yalivyo au yalivyoisha imekua ngumu kwao kupata nafasi hii. Swali ni, tufanye nini ili hata kama mahusiano yanaisha, bado mwanaume anapata nafasi ya kuwa baba na kuhusika kwenye maisha ya mtoto wake?
Karibu kusikiliza mazungumzo haya