Linapokuja swala la ndoa na mafanikio ya ndoa watu wengi huwa na mitazamo tofauti. Wapo wanaosema ndoa ni ngumu na si rahisi kufanikiwa kwenye ndoa, na wapo wanaosema ndoa ni ngazi ya mafanikio pale wanandoa wanapokubaliana kwenye hilo.
Leo hii, sisi tunajiuliza, ni nini nafasi ya mwanaume kwenye kuifanya ndoa ifanikiwe? Ni kweli kwamba ndoa inapaswa kuwa ngumu? Kwa wanaume ambao wamefanikiwa kuishi kwenye ndoa vizuri na kwa muda mrefu, ipi imekuwa chachu ya mafanikio hayo?
Julius Mlacha ana umri wa miaka 50, na ndoa yake inakaribia miaka 25. Ameungana na Michael na Nadia kwenye maongezi haya akielezea kiundani siri ya mafanikio kwenye ndoa yake, na namna gani mwanaume ana nafasi na jukumu kubwa sana kwenye kuhakikisha ndoa yake inadumu na ina stawi katika namna bora. Huu ni ukweli kuhusu ndoa yake