podcast
details
.com
Print
Share
Look for any podcast host, guest or anyone
Search
Showing episodes and shows of
Amedeus D. Raphael
Shows
Amedeus Live Podcast
UFUFUO NDIO UFUNGUO
Uzima wa milele, uzima wa aina ya Mungu ni matokeo ya kufufuka kwa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo. Jifunze zaidi kuhusu umuhimu wa ufufuo na matokeo yake katika maisha yetu. Hii rhapsodi ya Januari 4, 2024. Imeandikwa na Mchungaji Chris Oyakhilome na imesomwa na Amedeus Raphael.
2024-01-04
11 min
Amedeus Live Podcast
Maisha yako ya ustawi ndani ya Kristo
Haujaumbiwa shida, mateso, umaskini wala uhaba. Ulimwengu wote ni wako, wewe ni mrithi wa pamoja na Kristo. Sikiliza Kweli hii kutoka kwenye rhapsodi ya Uhakika, toleo la Januari 3, 2024. Hakika huu ni mwaka wako wa Ukombozi. Endelea kusikiliza podcast hii inayoitwa Amedeus Live kila siku ili uishi maisha ya ubora na ukuu ulioitwa kuyaishi.
2024-01-03
10 min
Amedeus Live Podcast
Maombi Maalumu Kwa Ajili Yako
Sikiliza Maombi haya Maalumu kwa Ajili Yako na fanya ukiri huu pamoja na mtumishi wa Bwana - Amedeus Deogratius, na utembee kwenye halisia za mbaraka wako ndani ya Kristo.
2023-12-30
03 min
Amedeus Live Podcast
Imani ya Aina ya Mungu
Sikiliza kongamano hili la imani ambalo lilifanyika mkoa wa Mbeya ambapo utajifunza namna ya kutenda kwa imani ya aina ya Mungu. Mtumishi Amedeus Deogratius alihudumu katika kongamano hili.
2023-12-29
08 min
Amedeus Live Podcast
Utukufu hadi Utukufu
Pro 4:18 Bali njia ya wenye haki ni kama nuru ing'aayo, Ikizidi kung'aa hata mchana mkamilifu. hii ndio inapaswa kuwa safari ya maisha yako kwenye kila nyanja ikiwemo na afya yako pia. Endelea kutumia kinywa chako kutunza afya yako.
2022-02-15
02 min
Amedeus Live Podcast
Maisha Marefu
Pro 3:1 Mwanangu, usiisahau sheria yangu, Bali moyo wako uzishike amri zangu. Pro 3:2 Maana zitakuongezea wingi wa siku. Na miaka ya uzima, na amani. Ni hamasa ya Mungu kwamba uwe afya njema siku zote na uishi maisha marefu yenye kumpa sifa na utukufu. Chagua kuishi sawasawa na neno lake kwa ajili yako. Tumia kinywa chako kurefusha maisha yako.
2022-02-15
02 min
Amedeus Live Podcast
Asili ya Kiungu
Wewe sio wa kawaida, umezaliwa kwa mbegu ya Mungu, wewe ni zaidi ya mwanadamu wa kawaida. Unao uzima wa aina ya Mungu.
2022-02-13
02 min
Amedeus Live Podcast
Maisha ya Utukufu
Safari ya Mtu mwenye haki ni kama siku ipambazukayo.... iking'aa na kung'aa mpaka mchana mkamilifu. #mchana #kung'aa #safari #haki
2022-02-12
02 min
Amedeus Live Podcast
Kutokuzeeka
Wewe umezaliwa na Neno la Mungu linalodumu na kuishi hata milele. Kataa afya yako isizeeke, kudhoofu au kuathiriwa na Magonjwa. #kutokuzeeka #umri #uzee #neno
2022-02-12
02 min
Amedeus Live Podcast
Nastawi Daima
Mimi ni kama mti uliopandwa kando kando ya vijito vya maji. Nazalisha matunda mwaka nzima. Maambukizi, viwavi na chochote kinachoharibu hakina nafasi ndani yangu. Maisha yangu ni kusonga mbele na kupanda juu tuu. Hallelujah.
2022-01-30
02 min
Amedeus Live Podcast
Maisha ya Utukufu
Tunaishi ndani yake, uzima wake ni uzima wetu! Tumeketishwa pamoja nae katika eneo la mamlaka na ukuu mbali sana na maradhi, magonjwa na mauti. Hallelujah!
2022-01-30
02 min
Amedeus Live Podcast
Ninaishi kwa Imani
Kwa maana pasipo imani huwezi kumpendeza Mungu..... Wenye haki wa Mungu wataishi kwa imani na sio kwa kuona, au kuhisi kwa milango ya fahamu ya mwili.
2022-01-27
02 min
Amedeus Live Podcast
Imani yangu ndio Ushindi
1Jn 5:4 Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu.
2022-01-27
02 min
Amedeus Live Podcast
Unabii wa Rhapsodi ya Uhakika mwaka 2022
Haya ni maneno ya unabii kwa ajili ya usambazaji wa Rhapsodi ya Uhakika (ya Mungu) Tanzania nzima. Bwana ametoa neno lake na jina la Bwana libarikiwe.
2022-01-26
40 min
Amedeus Live Podcast
Naleta Mabadiliko
Mimi sio mhanga wa maisha wala wa dunia. Mwili wangu ni Hekalu la Roho Mtakatifu. Ninaishi kwenye afya njema siku zote. Ninatawala na kumiliki katika maisha haya.
2022-01-23
02 min
Amedeus Live Podcast
Asili yangu ya Kiungu
Mimi ni wa juu na sio chini! Mimi ni raia wa Sayuni - mji Mtakatifu! Safari ya maisha ni kutoka utukufu hata utukufu.
2022-01-23
02 min
Amedeus Live Podcast
Sina mahusiano na Mauti
Mimi ni Roho Mmoja Pamoja na Bwana. Mwili wangu ni makao ya kudumu ya Roho wa Mungu. Mimi ni tawi na yeye ni Shina la Mzabibu.
2022-01-23
02 min
Amedeus Live Podcast
Uzima wa Mungu ndani Yako
Wewe una uzima wa aina ya Mungu. Uhai wako unabebwa na aina huu ya uzima. Wewe sio mwanadamu wa kawaida. Wewe ni mwana wa Mungu.
2022-01-23
02 min
Amedeus Live Podcast
Ninao Uzima wa Mungu
Tendea kazi neno la Mungu kila Siku. Kataa kuathiriwa au kukwamishwa na Nguvu pinzani. Ukiri wako ni ufunguo wa afya yako.
2022-01-23
02 min
Amedeus Live Podcast
Twaa Ngao Yako
Fahamu silaha uliyopewa na Mungu kwa ajili ya kujikinga na mashubulizi ya adui. Usipojua namna ya kutumia silaha hii utakuwa mhanga katika maisha wakati sio kusudi la Mungu kwa ajili yako. Unaweza kupakua nakala ya rhapsodi hii kwa mwezi mzima kupitia link hii.
2022-01-14
05 min
Amedeus Live Podcast
Roho Moja Pamoja Naye
Mimi ni kiungo cha mwili Wake, cha nyama Yake, na cha mifupa Yake! Ninatembea katika ufahamu kwamba niko katika muunganiko na Yesu Kristo. Na kupitia roho, ninaufanya mwili wangu upate utukufu wa mwili Wake uliofufuka. Hakuna ugonjwa, maradhi au udhaifu unaoweza kusitawi katika mwili wangu, kwa sababu nimeunganishwa na Bwana na ni roho moja pamoja Naye. Uungu unafanya kazi ndani yangu. Utukufu kwa Mungu!
2022-01-10
10 min
Amedeus Live Podcast
USISHINDWE NA UOVU
Rhapsodi ya Uhakika, Dec 6, 2020. Mimi niko kwenye dunia, lakini mimi si wa dunia. Kwa hiyo, ninawaza, ninaongea, na kutenda tofauti na maisha ya dunia yalivyo. Nimetakaswa na Roho Mtakatifu, nikitengwa na Mungu kwa ajili ya kwa ajili ya matumizi matakatifu, yasiyo na mawaa. Ninatawala juu ya dhambi na kazi zake zotemagonjwa, udhaifu, umaskini, kifo nk. Amin.
2020-12-06
10 min
Amedeus Live Podcast
ATHIRI ULIMWENGU WAKO
Rhapsodi ya Uhakika, Dec 5, 2020 Mpendwa Baba, ahsante kwa kuniita katika maisha ya athari na kwa kunipa rasilimali kuu kuliko zote—ambayo ni Roho Mtakatifu—ili kunisaidia kutembea katika mapenzi Yako na makusudi Yako kwa ajili ya maisha yangu. Uliniumba katika Kristo Yesu kwa ajili ya kazi njema ambazo uliziandaa tangu kabla ya kuwekwa kwa misingi ya ulimwengu kwamba nienende katika hizo. Na sasa, kwa Roho Wako, maisha yangu yote yako katika kuliendea kusudi Lako na kutawazwa kwa Ufalme Wako katika mioyo ya wanadamu, katika Jina la Yesu. Amina.
2020-12-05
09 min
Amedeus Live Podcast
NI KUHUSIANA NA NENO KATIKA KINYWA CHAKO
RHAPSODI YA UHAKIKA, DEC 4, 2020. UKIRI Kupitia msaada wa Roho, na katika kulitafakari Neno la Mungu daima, ninazungumza kwa uangalifu maneno mazuri, ya kujenga, ya neema, yenye kuhuisha, yenye kuhamasisha, na yenye kutia moyo. Kwa maneno yangu, ninaumba mafanikio, ushindi, afya ya Kiungu na ustawi kutokea ndani, nikisimamisha haki ya Mungu katika ulimwengu wangu, katika Jina la Yesu. Amina.
2020-12-04
10 min
Amedeus Live Podcast
WEKA SHABAHA YAKO KWA BWANA NA KATIKA UFALME WAKE
Rhapsodi ya Uhakika: Dec 03, 2020. Ukiri. Nimehamishwa kutoka katika ulimwengu wa giza na kwenda katika “Ufalme wa Mwana wa pendo Lake.” Ijapokuwa ni ulimwenguni, nina fikra za ufahamu wa Ufalme wa Mbinguni. Hivyo, ninatenda kutoka katika uwanda wa ulimwengu wa roho, na hakuna kitu katika ulimwengu huu wa nyama kwamba ni cha thamani kwangu. Na hakika, kupitia kuenea kwa Injili kusikozuilika, Ufalme wetu unatawala juu ya mataifa. Amina!*
2020-12-03
10 min
Amedeus Live Podcast
ELEWA NA LITAMKE NENO
Rhapsodi ya Uhakika, Dec 02, 2020. Kuna Wakristo ambao uzoefu wao katika maisha ni kinyume cha imani yao na Neno la Mungu. Kwa mfano, wanaweza kuwa wanaamini kwamba kama Wakristo, hawapaswi kukandamizwa na Shetani, ila wanapitia uzoefu wa mkandamizo wa kishetani na hila. Wanaamini kuwa hawapaswi kuugua au kuwa na madhoofu katika miili yao, ili hali ni vigumu sana kwao kuwa na uzoefu wa afya njema. Kuna kitu hakipo sawa.
2020-12-02
10 min
Amedeus Live Podcast
Changia Kipindi cha Rhapsodi
Kuwa sehemu ya kupeleka injili katika ulimwengu nzima kwa kuchangia kipindi hichi cha rhapsodi ambacho pia kinaruka hewani kupitia radio za kawaida katika mikoa ya nyanda za juu kusini na katika visiwa vya zanzibar. Wasiliana na nasi katika namba zifuatazo: 0736000999.
2020-12-02
02 min
Amedeus Live Podcast
MBINGU MPYA NA NCHI MPYA
Rhapsodi ya Uhakika - Dec 1, 2020 Ukiri Mimi nimekufa kwa ulimwengu na ulimwengu umekufa kwangu. Hivyo, ninaweka umakini wangu katika Bwana na Ufalme Wake wa milele, nikimpenda Yeye kwa moyo wangu wote. Mambo ya Roho ni ya muhimu sana kwangu kuliko kitu chochote katika ulimwengu huu. Ninaishi kila siku ingali umakini wangu ukiwa katika Injili, kuihubiri na kuieneza kote ulimwenguni kwa uweza wa Roho Mtakatifu. Amina!*
2020-12-01
10 min
Amedeus Live Podcast
TWALITUKUZA JINA LAKE
Mungu amejitukuza Mwenyewe ndani yangu; sasa, ninaubeba utukufu huo kila mahali. Hakuna aibu maishani mwangu; ninatembea katika utukufu, na maisha yangu yamejawa utukufu—heshima, nakshi, ukuu, uzuri, upendeleo! Ninatembea kiuendelevu katika afya ya kiungu, ustawi, na kuiathiri dunia yangu kwa utukufu Wake. Asifiwe Mungu!
2020-11-30
10 min
Amedeus Live Podcast
KUWA NA SHEREHE YA KUSIFU
Naye alipokwisha kufanya shauri na watu, akawaweka wale watakaomwimbia BWANA, na kumsifu katika uzuri wa utakatifu, wakitoka mbele ya jeshi, na kusema, Mshukuruni BWANA; kwa maana fadhili zake ni za milele (2 Mambo Ya Nyakati 20:21).
2020-11-29
09 min
Amedeus Live Podcast
UJAZO WAKE NDANI YAKO
Rhapsodi ya Uhakika - Nov 28, 2020. Mimi ni chombo kimbebacho Mungu; Kristo ndani yangu ni utukufu uliotambulika, ushindi uliohakikishwa, na usitawi uliothibitishwa. Hakuna hofu wala kuchanganyikiwa maishani mwangu. Bila kujali mitihani, majaribu ama changamoto zinazoweza kuja kinyume na mimi, mimi ni mshndi na kinara maishani. Haleluya!
2020-11-28
10 min
Amedeus Live Podcast
JIANDAE NA “NDEGE YA KWANZA”
Rhapsodi ya Uhakika - Nov 27, 2020. Mat 24:37 Kwa maana kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. Mat 24:38 Kwa kuwa kama vile siku zile zilizokuwa kabla ya Gharika watu walivyokuwa wakila, na kunywa, wakioa na kuolewa, hata siku ile aliyoingia Nuhu katika safina, Mat 24:39 wasitambue, hata Gharika ikaja, ikawachukua wote, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu
2020-11-27
10 min
Amedeus Live Podcast
MAARIFA YA WEWE NI NANI
Rhapsodi ya Uhakika, Nov 25. 2020 Unachohitaji ni maarifa sahihi na ya kutosha ya Neno la Mungu; hiki ndicho hukuweka juu maishani. Wengi hawana tatizo la imani, kwa maana kila mmoja wetu anayo imani (Warumi 12:3). Suala hapa ni ukosefu wao wa uelewa wa wao ni nani na nini ni milki yao katika Kristo.
2020-11-25
10 min
Amedeus Live Podcast
ZINGATIA RATIBA ZA WENGINE
Rhapsodi ya Uhakika, Nov 23, 2020. Jitahidi katika ubora wako usiiharibu siku ya wengine. Najua, kuna upande wa pili kwa jambo hili; unaweza kuwa ndiwe upaswaye kumuona mtu, lakini umeweka muda uo huo kuwaona watu wengine watano katika mji! Kwa hakika utakwenda angalau kumsubirisha mtu mmoja au zaidi kati yao, na hiyo si sawa. Hata ukiwa kama mkubwa (bosi) katika ofisi, kuwa makini na ratiba za walio chini yao. Watu waliofanikiwa wanajali [na kuzingatia] muda.
2020-11-23
09 min
Amedeus Live Podcast
UMO NDANI YA NURU
Rhapsodi ya Uhakika, Nov 22, 2020. Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu (1 Petro 2:9). SALA Ninakushukuru mpendwa Bwana kwa kunitoa gizani kuingia katika Ufalme wa Mwana wa pendo lako, ambamo ninatawala kwa neema kupitia haki, na kuufurahia uhuru tukufu wa wana wa Mungu. Wewe ni nuru ya maisha yangu, ambayo ninaitumia kujielekezea katika njia yangu kiubora katika ushindi, utawala, na mafanikio, katika Jina la Yesu. Amina.
2020-11-22
10 min
Amedeus Live Podcast
KILA KITU KIMETIISHWA CHINI YA KRISTO
Rhapsodi ya Uhakika- Npov 21, 2020. Alipokuwa katika kusema, tazama, wingu jeupe likawatia uvuli; na tazama, sauti ikatoka katika lile wingu, ikasema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye; msikieni yeye (Mathayo 17:5).
2020-11-21
10 min
Amedeus Live Podcast
MATUNDA YA UTII WAKE
Rhapsodi ya Uhakika, Nov 20, 2020 Basi tena, kama kwa kosa moja watu wote walihukumiwa adhabu, kadhalika kwa tendo moja la haki watu wote walihesabiwa haki yenye uzima (Warumi 5:18).
2020-11-20
09 min
Amedeus Live Podcast
JIKABIDHI KWAKE NA ULIFUATE NENO
Rhapsodi ya Uhakika- Nov 19, 2020 Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yoteatakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari. (Yohana 16:13).
2020-11-19
10 min
Amedeus Live Podcast
MWENDO WA IMANI
Rhapsodi ya Uhakika, Nov 18, 2020. Warumi 9:8 inasema, “Yaani, si watoto wa mwili walio watoto wa Mungu, bali watoto wa ile ahadi wanahesabiwa kuwa wazao.” Watoto wa mwili wanaongozwa na hisia zao. Badala ya kuenenda kwa imani, wanaendeshwa tu na kila ambacho wanaweza kuona kwa macho, kusikia, kugusa, kuonja, au kunusa kwa mwili. Lakini Ukristo ni mtembeo wa imani; ni maisha yapitayo hisia.
2020-11-17
11 min
Amedeus Live Podcast
Kuishi Katika Nuru yake ya Ajabu
Rhapsodi ya Uhakika, Nov 17, 2020. Ninaomba Mungu kwamba wototo wote wa Mungu wakaelewe andiko hilo hapa juu lina nguvu namna gani! Linasema tumekombolewa kutoka katika utawala wa giza na kuhamishiwa katika Ufalme wa Mwana wa pendo Lake. Hapo ndipo ulipo sasa! Lakini Mkristo asiyekuwa na uelewa huu atakuwa akiishi maisha ya giza, akifikiri mawazo ya giza, ambako tayari amekwisha ondolewa. Giza huwakilisha dhambi,
2020-11-17
10 min
Amedeus Live Podcast
KUISHI KATIKA RAHA YAKE
Rhapsodi ya Uhakika, Nov 16, 2020. Ahimidiwe Mungu! Amenipa maisha yapitayo kawaida ya haki, na ninatembea katika ushindi na utawala, kutokea mahali pa pumziko. Neema Yake yatosha kwangu, na katika mambo yote, ninatimiliza hatma yangu kitukufu na pasipo kusumbuka, katika Jina la Yesu. Amina.
2020-11-16
10 min
Amedeus Live Podcast
JINA LAKO NI MUHIMU
Rhapsodi ya Uhakika. Nov 14, 2020. Mbarikiwa Baba, ninakushukuru kwa Neno Lako ambalo linafunua utambulisho wangu, urithi na uweza katika Kristo! Mapenzi Yako kwa ajili ya maisha yangu yamefunuliwa katika roho yangu na ninaishi kila siku kuyatimiza mapenzi na makusudi Yako kwa ajili ya maisha yangu, nikienenda katika njia Ulizoziandaa tayari kwa ajili yangu, katika Jina la Yesu. Amina.
2020-11-14
10 min
Amedeus Live Podcast
LINDA WOKOVU WAKO
Rhapsodi ya Uhakika, Nov 14, 2020. Sisi je! Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale waliosikia (Waebrania 2:3). Ninamtumikia Bwana katika roho na kweli. Pendo Lake daima na kwa uendelevu linaendelea kudhihirika kupitia mimi kuwamiminikia wengine. Hakuna nafasi kwa ajili ya chuki, uchungu, wivu, au majivuno ndani yangu, kwa maana pendo la Mungu limemiminwa kwa wingi katika moyo wangu na Roho Mtakatifu. Na pendo hilo lanibidisha kuihubiri Injili na kuwafikia waliopotea kwa upendo, kuwageuza kutoka gizani na kuwaleta kwa Kristo. Amina.
2020-11-14
10 min
Amedeus Live Podcast
Warithi wa Utajiri Usio na Mwisho
Rhapsodi ya Uhakika - Nov 13, 2020 “Kwangu mimi, ingawa mimi ndiye niliye mdogo kabisa kati ya watakatifu wote (watu wa Mungu waliowekwa wakfu), neema hii (kibali, upendeleo) niliopewa na kuaminiwa: kutangaza kwa Mataifa mali (isiyo na mipaka, usiyopimika, usiyo na hesabu, isiyohesabika, na isiyo na mwisho) ya utajiriwa Kristo usio na ukomo [utajiri ambao hakuna mwanadamu anaeweza kuuchunguza].”
2020-11-13
10 min
Amedeus Live Podcast
Uliyetukuzwa katika Kristo
Rhapsodi ya Uhakika - Nov 12, 2020. Mimi ni utukufu wa Mungu! Ninaonyesha na utukufu—Anaishi ndani yangu katika utimilifu Wake wote. Kupitia kujifunza na kulitafakari Neno, daima ninabadilishwa kutoka utukufu hata utukufu. Asifiwe utukufu—Anaishi ndani yangu katika utimilifu Wake wote. Kupitia kujifunza na kulitafakari Neno, daima ninabadilishwa kutoka utukufu hata utukufu. Asifiwe Mungu!
2020-11-12
10 min
Amedeus Live Podcast
Weka Umakini wako katika Lengo Kubwa Zaidi
Rhapsodi ya Uhakika - Nov 11, 2020. 2Co 5:18 Lakini vyote pia vyatokana na Mungu, aliyetupatanisha sisi na nafsi yake kwa Kristo, naye alitupa huduma ya upatanisho; 2Co 5:19 yaani, Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu neno la upatanisho. 2Co 5:20 Basi tu wajumbe kwa ajili ya Kristo, kana kwamba Mungu anasihi kwa vinywa vyetu; twawaomba ninyi kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na Mungu.
2020-11-11
18 min
Amedeus Live Podcast
Dhirisha Shukrani
Rhapsodi ya Uhakika, Nov 10, 2020. Nina shina na ninajengwa katika Bwana, nimeimarishwa katika imani na kufurika shukrani! Kila siku, ninachochewa kudhihirisha shukrani zangu kwa Mungu, na kwa wale ambao kupitia hao Ananibariki kila siku. Hivyo, ninaenenda katika upendeleo, furaha, na utoshelevu. Amina.
2020-11-10
10 min
Amedeus Live Podcast
Kiri Kweli yake Kwa Imani
Rhapsodi ya Uhakika - Nov 9, 2020. Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu (1 Yohana 5:4). Mimi ni shupavu katika imani na katika neema ambayo iko ndani ya Kristo Yesu. Ninatamka ushindi, mafanikio, afya, nguvu, na uhodari daima, kwa maana mkuu ni Yule aliye ndani yangu, kuliko yule aliye katika dunia. Neno la Mungu limeshika hatamu yote na linadhihirika ndani yangu, na kupitia roho yangu, nafsi, na mwili. Haleluya!
2020-11-09
10 min
Amedeus Live Podcast
Aliandaa Maisha Mazuri ya Ajabu kwa Ajili Yako
Rhapsodi ya Uhakika - Nov 8, 2020. Mimi ni kiumbe kipya, niliyeitwa kupokea baraka, niliyewezeshwa kufanikiwa katika kila jambo ninalolifanya! Hakuna ukame, kudumaa, ukosefu au kutokuwa na matunda katika maisha yangu, kwa maana nimechaguliwa na kuteuliwa kwa ajili ya maisha ya sifa, furaha, ubora, ushindi, na utukufu katika Kristo Yesu. Nimefanyika kuwa mchukuzi wa baraka za Mungu na mng’ao wa utukufu Wake. Haleluya!
2020-11-08
10 min
Amedeus Live Podcast
Mvumbue Yesu na Kutafuta kwako Kutakoma
Rhapsodi ya Uhakika - Nov 7, 2020. Col 1:15 naye ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote. Col 1:16 Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake. Col 1:17 Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye. Col 1:18 Naye ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha kanisa; naye ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu, ili kwamba awe mtangulizi katika yote. Col 1:19 Kwa kuwa katika yeye ilipendeza utimi...
2020-11-07
20 min
Amedeus Live Podcast
Ulikuja kwa Kusudi
Rhapsodi ya Uhakika - Nov 5, 2020. 1Jn 3:7 Watoto wadogo, mtu na asiwadanganye; atendaye haki yuna haki, kama yeye alivyo na haki; 1Jn 3:8 atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi.
2020-11-05
10 min
Amedeus Live Podcast
Hakuachi Kamwe
Rhapsodi ya Uhakika, Nov 4, 2020. Heb 13:5 Msiwe na tabia ya kupenda fedha; mwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa. Heb 13:6 Hata twathubutu kusema, Bwana ndiye anisaidiaye, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini?
2020-11-04
09 min
Amedeus Live Podcast
Usibabaike Kuhusu Mustakabali wa Siku Zijazo
Rhapsodi ya Uhakika - Nov 3, 2020. 2Co 4:16 Kwa hiyo hatulegei; bali ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku. 2Co 4:17 Maana dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda wa kitambo tu, yatufanyia utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana; 2Co 4:18 tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele.
2020-11-03
10 min
Amedeus Live Podcast
Enenda Katika Hekima
Rhapsodi ya Uhakika - Nov 2, 2020. Act 20:32 Basi, sasa nawaweka katika mikono ya Mungu, na kwa neno la neema yake, ambalo laweza kuwajenga na kuwapa urithi pamoja nao wote waliotakaswa.
2020-11-02
09 min
Amedeus Live Podcast
UHODARI [USHUJAA] KWA AJILI YA INJILI
Rhapsodi ya Uhakika, Nov 1, 2020. Watu walio na ujasiri hudumisha shabaha yao katika kile wanachoamini, na hakuna kilicho kikubwa sana kwao kukitoa au kukifanya katika kutimiza azma ya imani yao. Hivyo, weka ufahamu wako kwa Bwana na katika Neno Lake, na uwe tayari kila wakati kwa ajili ya kufanya jambo lo lote lile kwa ajili ya kuenea kwa Injili.
2020-11-01
10 min
Amedeus Live Podcast
Hekima Kwa Ajili Ya Maisha Ya Ukuu
Rhapsodi ya Uhakika - Oct 31, 2020 Pro 4:5 Jipatie hekima, jipatie ufahamu; usiusahau; Wala usiyakatae maneno ya kinywa changu. Pro 4:6 Usimwache, naye atakuhifadhi; Umpende, naye atakulinda. Pro 4:7 Bora hekima, basi jipatie hekima; Naam, kwa mapato yako yote jipatie ufahamu. Pro 4:8 Umtukuze, naye atakukuza; Atakupatia heshima, ukimkumbatia. Pro 4:9 Atakupa neema kuwa kilemba kichwani; Na kukukirimia taji ya uzuri.
2020-10-31
08 min
Amedeus Live Podcast
Washirika na Wasambazaji wa Uzima wa Kiungu
Rhapsodi ya Uhakika, Oct 30, 2020. Wewe ni mbebaji wa halisia za milele. Unapotokezea, uzima hudhihirika. Unapowagusa wagonjwa na walioonewa, uzima wa ndani yako unahamishiwa na kuingizwa ndani yao, ukiwaletea utimilifu na ukamilifu. Ndio maana Yesu akatuamuru katika Mathayo 10:8, ”Ponyeni wagonjwa, watakaseni wakoma, wainueni wafu, na mkawatimue pepo.”
2020-10-30
11 min
Amedeus Live Podcast
Zungumza Kwa Usahihi Na Uwe Na Maisha Makuu
Rhapsodi ya Uhakika - Oct 29, 2020. Mithali 18:21 inasema, “Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake.” Utavuna mavuno ya mambo mema kupitia maneno yako. Maneno ni vitu; maneno ni nguvu ya uumbaji. Maisha yako leo ni matokeo ya maneno yako. Mithali 15:4 inasema, “Ulimi safi ni mti wa uzima….” Kama maneno yako ni mazuri, maisha yako yatakuwa makamilifu, bora, na ya kuhamasisha.
2020-10-29
10 min
Amedeus Live Podcast
Kuishi katika Mamlaka Yake
Rhapsodi ya Uhakika, Oct 28, 2020. Waf 2:9 Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; Waf 2:10 ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; Waf 2:11 na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.
2020-10-28
10 min
Amedeus Live Podcast
Wenye Dhamana Ya Ujumbe Uzaao Matunda
Rhapsodi ya Uhakika, Oct 27, 2020. Kuishi bila Kristo ni kuishi pasipo Mungu; katika hukumu. Hii ndio maana unalazimika kuwa na bidii katika roho, ukiihubiri Injili (Warumi 12:11). Umetumwa kuipeleka nuru ya Injili kwa wale wenaoishi gizani (Matendo 13:7). Kwa hiyo, usiizuilie; usiwe mwenye kughairi. Kuwa na uthubutu na utambue kuwa wewe ni mwenye dhamana ya ujumbe wenye kuzaa matunda.
2020-10-27
10 min
Amedeus Live Podcast
Yeye Anamfadhili Mvuna Nafsi
Rhapsodi ya Uhakika - Oct 26, 2020 Baadhi ya watu wameutoa muda na mali zao katika kuhakikisha kuwa Injili inafika katika kila taifa la duniani. Wanafanya mambo makubwa katika kuiendeleza ajenda ya Mungu, wakiufidia upungufu na kutoweza kwa wengine. Wanatoa fedha nyingi sana katika kuisukuma Injili; na kadri watoavyo, ndivyo Bwana aelekezavyo zaidi rasilimali katika njia yao ili wakafanikishe mambo makubwa zaidi kwa ajili Yake. Atakusambazia yote utayoweza hitaji ili kulitimiliza kusudi Lake la kuvuna nafsi.
2020-10-26
10 min
Amedeus Live Podcast
Kudhihirisha Maisha Ya Kristo Ndani Yako
Rhapsodi ya Uhakika, Oct 24, 2020. Ukristo ni udhihirisho wa nje wa utendaji kazi wa Neno la Mungu ndani roho ya mwanadamu. Kama Mkristo, wewe ndiwe taswira ya Kristo, kila hatua unayoichukua inapaswa kuwa ni udhihirisho wa uzima wa Kiungu ndani yako. Hivyo ndivyo namna Yesu alivyoishi pale Alipokuwa akienenda katika dunia. Alikuwa ni udhihirisho wa Mungu; udhihirisho wa maisha ya Kiungu
2020-10-24
09 min
Amedeus Live Podcast
Fikiria Unyakuo Katika Mawazo Yako
Rhapsodi ya Uhakika Unyakuo wa Kanisa u karibu kuliko wakati wowote. Tu katika nyakati za hitimisho au mwishoni mwa “nyakati za ishara” kabla kutokea kwa Bwana. Ni muhimu kwamba ukawe tayari kwa ajili Yake. 1 Wathesalonike 4:16-17 inasema “wafu katika Kristo” watainuka kwanza, na wale walio hai na wamebaki watanyakuliwa pamoja nao ili kumlaki Bwana angani.
2020-10-24
10 min
Amedeus Live Podcast
Sababu Tatu Za Msingi Za Kwanini Uvune Nafsi
Rhapsodi ya Uhakika - Oct 23, 2020. Kuna sababu tatu za msingi za kwanini unalazimika kuihubiri Injili na kuvuna nafsi kama Mkristo. Kwanza ni imani yako katika Bwana Yesu na Injili Yake tukufu. Sababu ya pili ni upendo wako Kwake na tumaini la kurejea Kwake hivi punde. Sababu ya tatu ni maagizo Yake kwetu ya kuvuna nafsi. Sababu hizi tatu zikusukume kuvuna nafsi.
2020-10-23
10 min
Amedeus Live Podcast
Yesu Ndiye Mungu Mwenyewe
Rhapsodi ya Uhakika: Oct 22, 2020 Yesu ni Mungu katika mwili wa binadamu, lakini watu hawakujua. Yeye ni Adonai, Yaani Bwana, Mungu! Ndiye aliyemwambia Musa, “Baba zako, Ibrahimu, Isaka na Yakobo walinijua kama, Mungu Mwenyezi (mweza wa yote), lakini mimi ni Yehova” (Kutoka 6:3). Yehova ni Yahweh. Na kama haujawahi kuzaliwa mara ya pili, kama bado haujamfanya Yesu kuwa Bwana wa maisha yako, iseme sala hii na uimaanishe kwa moyo wako wote: “Ee Bwana Mungu, ninaamini kwa moyo wangu wote katika Yesu Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai. Ninaamini alikufa kwa ajili yangu na ya kuwa Mungu alimfufua kutoka...
2020-10-22
12 min
Amedeus Live Podcast
Mjue Kama Bwana
Rhapsodi ya Uhakika: Oct 21, 2020. Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba (Wafilipi 2:9-11).
2020-10-21
10 min
Amedeus Live Podcast
Yesu ni Udhihirisho wa Taswira ya Mungu
Rhapsodi ya Uhakika - Oct 20, 2020 Mpenzi Bwana Yesu, utukufu, heshima na ukuu wote ni Wako. Wewe ni Mfalme wa utukufu, furaha ya mbinguni, na nyota ing’aayo ya asubuhi! Wewe ni udhihirisho wa utukufu wa Mungu, uzuri wa Uungu, na taswira kamilifu ya Nafsi ya Baba. Ninakuabudu na kukuheshimu Mwokozi wa thamani, kwa maana hayupo wa kufanana na Wewe! Ufalme Wako na ukatawale nchini, na kusimama daima katika mioyo ya watu wote. Amina.
2020-10-20
12 min
Amedeus Live Podcast
JIgundue Ndani Yake
Rhapsodi ya Uhakika - Oct 19, 2020. Ukristo si kuhusiana na kukazana kuingia uweponi mwa Mungu; Ukristo ni kubeba uwepo wa Mungu. Wewe ni hema Yake ya ushuhuda iishiyo. Unapofika popote, uwepo wa Mungu hufika! Wewe ndiwe “uwepo.” Haleluya!
2020-10-19
09 min
Amedeus Live Podcast
Wewe Unaimiliki Dunia
Rhapsodi ya Uhakika - Oct 18, 2020. 1Co 3:21 Basi, mtu ye yote na asijisifie wanadamu. Kwa maana vyote ni vyenu; 1Co 3:22 kwamba ni Paulo, au Apolo, au Kefa; au dunia, au uzima, au mauti; au vile vilivyopo sasa, au vile vitakavyokuwapo; vyote ni vyenu; 1Co 3:23 nanyi ni wa Kristo, na Kristo ni wa Mungu.
2020-10-18
10 min
Amedeus Live Podcast
Lifuate Neno wala Sio Akili Zako
Rom 8:7 Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii. Rom 8:8 Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu. Rom 8:9 Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake.
2020-10-17
10 min
Amedeus Live Podcast
Jijue Wewe ni Nani na Ishi sawasawa na Asili yako
Rhapsodi ya Uhakika - Oct 16, 2020. Jas 1:22 Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu. Jas 1:23 Kwa sababu mtu akiwa ni msikiaji wa neno tu, wala si mtendaji, mtu huyo ni kama mtu anayejiangalia uso wake katika kioo. Jas 1:24 Maana hujiangalia, kisha huenda zake, mara akasahau jinsi alivyo. Jas 1:25 Lakini aliyeitazama sheria kamilifu iliyo ya uhuru, na kukaa humo, asiwe msikiaji msahaulifu, bali mtendaji wa kazi, huyo atakuwa heri katika kutenda kwake.
2020-10-16
08 min
Amedeus Live Podcast
Uzao wa Upendo
Upendo huvumila kwa kitambo kirefu na una subira pamoja na fadhili; upendo kamwe hauhusudu wala kutokota kwa wivu, haujivuni wala hautakabari, haujidhihirishi kwa majivuno (1 Wakorintho 13:4 toleo la “AMPC”).
2020-10-15
10 min
Amedeus Live Podcast
Jina lake lina Mamlaka Yote
Rhapsodi ya Uhakika - Oct 14, 2020. Matendo 3:16 Na kwa imani katika jina lake, jina lake limemtia nguvu mtu huyu mnayemwona na kumjua; na imani ile iliyo kwake yeye imempatia huyu uzima huu mkamilifu mbele yenu ninyi nyote. Kitabu cha kila siku, chenye neno la kila siku, kina andikwa na Mchungaji Chris Oyakhilome. Kinapatikana kwenye lugha zaidi ya 2200 duniani na kina sababisha shuhuda njema na bora kwa mia ya mamilioni ya watu ulimwenguni kote. Neno ni jipya kila siku na unaweza kubofya link hapo chini kupata nakala yako leo hii. pakua rhapsodi app leo kupitia lin...
2020-10-14
10 min
Amedeus Live Podcast
Yesu ni Neno Lililojivika Mwili
Rhapsodi ya Uhakika - Oct 13, 2020. Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika (Yohana 1:1-3). Kitabu cha kila siku, chenye neno la kila siku, kina andikwa na Mchungaji Chris Oyakhilome. Kinapatikana kwenye lugha zaidi ya 2200 duniani na kina sababisha shuhuda njema na bora kwa mia ya mamilioni ya watu ulimwenguni kote. Neno ni jipya kila siku na unaweza kubofya link hapo chini kupata nakala yako leo hii. pakua rhapsodi app leo kupitia li...
2020-10-13
10 min
Amedeus Live Podcast
Chukua Nafasi yako kama Mfalme-Kuhani
Rhapsodi ya Uhakika - Oct 12, 2020 Ghasia hazitasikika tena katika nchi yako, wala ukiwa au uharibifu ndani ya mipaka yako, bali utaziita kuta zako Wokovu na malango yako Sifa (Isaya 60:18 tolea la “AMPC”). Kitabu cha kila siku, chenye neno la kila siku, kina andikwa na Mchungaji Chris Oyakhilome. Kinapatikana kwenye lugha zaidi ya 2200 duniani na kina sababisha shuhuda njema na bora kwa mia ya mamilioni ya watu ulimwenguni kote. Neno ni jipya kila siku na unaweza kubofya link hapo chini kupata nakala yako leo hii. pakua rhapsodi app leo kupitia link hii. https...
2020-10-12
11 min
Amedeus Live Podcast
Muunganiko wetu na Baba - ROR Oct 11, 2020
Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye (1 Wakorintho 6:17).
2020-10-11
10 min
Amedeus Live Podcast
Tamka Na Umba Kile Unachokitaka
Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hata vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri (Waebrania11:3).
2020-10-09
10 min
Amedeus Live Podcast
Ni Kuhusiana Na Asili Yako Ya Kiungu
Rhapsodi ya Uhakika - Oct 9. “…kwa maana nalitoka kwa Mungu, nami nimekuja; wala sikuja kwa nafsi yangu, bali yeye ndiye aliyenituma.” Kwa matokeo ya muunganiko huu, Alisema, “Na yote aliyo nayo Baba ni yangu…” (Yohana 16:15).
2020-10-09
09 min
Amedeus Live Podcast
Sisi tu watu wa Namna Yake - ROR Oct 8, 2020
2Co 6:16 Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. Kitabu cha kila siku, chenye neno la kila siku, kina andikwa na Mchungaji Chris Oyakhilome. Kinapatikana kwenye lugha zaidi ya 2200 duniani na kina sababisha shuhuda njema na bora kwa mia ya mamilioni ya watu ulimwenguni kote. Neno ni jipya kila siku na unaweza kubofya link hapo chini kupata nakala yako leo hii. pa...
2020-10-08
09 min
Amedeus Live Podcast
Dumisha Hamasa yako kwa ajili ya Injili - ROR Oct 7, 2020
Rom 12:11 kwa bidii, si walegevu; mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia Bwana; Kuwa mwenye bidii na hamasa katika kazi ya injili. Kitabu cha kila siku, chenye neno la kila siku, kina andikwa na Mchungaji Chris Oyakhilome. Kinapatikana kwenye lugha zaidi ya 2200 duniani na kina sababisha shuhuda njema na bora kwa mia ya mamilioni ya watu ulimwenguni kote. Neno ni jipya kila siku na unaweza kubofya link hapo chini kupata nakala yako leo hii. pakua rhapsodi app leo kupitia link hii. https://t.co/GFr1tICObJ Jiunge na mtandao wa w...
2020-10-08
09 min
Amedeus Live Podcast
Unakila kitu unachokihitaji
ROR Oct 6, 2020. Baada ya mambo hayo neno la Bwana likamjia Abramu katika njozi, likinena, Usiogope, Abramu, MIMI NI NGAO YAKO, NA THAWABU YAKO KUBWA SANA Mwanzo 15:1 > Mungu ni urithi wako, fungu lako, Ngao yako, tambua hili na tembea katika maarifa ya kweli hii. Kitabu cha kila siku, chenye neno la kila siku, kina andikwa na Mchungaji Chris Oyakhilome. Kinapatikana kwenye lugha zaidi ya 2200 duniani na kina sababisha shuhuda njema na bora kwa mia ya mamilioni ya watu ulimwenguni kote. Neno ni jipya kila siku na unaweza kubofya link hapo chini kupata nakala yako leo...
2020-10-06
11 min
Amedeus Live Podcast
Rhapdosi ya Uhakika - Oktoba 2020
Kitabu cha kila siku, chenye neno la kila siku, kina andikwa na Mchungaji Chris Oyakhilome. Kinapatikana kwenye lugha zaidi ya 2200 duniani na kina sababisha shuhuda njema na bora kwa mia ya mamilioni ya watu ulimwenguni kote. Neno ni jipya kila siku na unaweza kubofya link hapo chini kupata nakala yako leo hii. http://distribution.rhapsodyofrealities.org/dept/?team=center1 na bofya link hii kupakua app ya rhapsodi leo hii. https://t.co/GFr1tICObJ
2020-10-01
50 min
Amedeus Live Podcast
Rhapdosi ya Uhakika - September 2020
Kitabu cha kila siku, chenye neno la kila siku, kina andikwa na Mchungaji Chris Oyakhilome. Kinapatikana kwenye lugha zaidi ya 2000 dunia na kina sababisha shuhuda njema na bora kwa mia ya mamilioni ya watu ulimwenguni kote. Neno ni jipya kila siku na unaweza kubofya link hapo chini kupata nakala yako leo hii. http://distribution.rhapsodyofrealities.org/dept/?team=center1
2020-09-01
5h 10
Amedeus Live Podcast
Rhapdosi ya Uhakika - August 2020
Kitabu cha kila siku, chenye neno la kila siku, kina andikwa na Mchungaji Chris Oyakhilome. Kinapatikana kwenye lugha zaidi ya 2000 dunia na kina sababisha shuhuda njema na bora kwa mia ya mamilioni ya watu ulimwenguni kote. Neno ni jipya kila siku na unaweza kubofya link hapo chini kupata nakala yako leo hii. http://distribution.rhapsodyofrealities.org/dept/?team=center1
2020-08-01
7h 12
Amedeus Live Podcast
Rhapdosi ya Uhakika - Julai 2020
Kitabu cha kila siku, chenye neno la kila siku, kina andikwa na Mchungaji Chris Oyakhilome. Kinapatikana kwenye lugha zaidi ya 2000 dunia na kina sababisha shuhuda njema na bora kwa mia ya mamilioni ya watu ulimwenguni kote. Neno ni jipya kila siku na unaweza kubofya link hapo chini kupata nakala yako leo hii. http://distribution.rhapsodyofrealities.org/dept/?team=center1
2020-07-01
7h 06
Amedeus Live Podcast
Rhapsodi ya Uhakika - June 2020
Kitabu kinachotoka kila mwezi chenye neno la kila siku. Kitabu kimendikwa na Mchungaji Chris Oyahkilome na Kimesomwa na Ndg. Amedeus Deogratius. Utajifunza mengi yapasayo maisha ya ushindi, afya bora, ustawi, upendo, haki, imani na namna bora ya kumwabudu Mungu katika roho na kweli.
2020-06-01
6h 15
Amedeus Live Podcast
Unabii - Elewa Nguvu inayotawala Mustakhabali wa Maisha Yako
Kitabu kimeandikwa na Mch. Chris Oyakhilome na Kimefanyiwa mapitio kwa njia ya Sauti na Amedeus D.R. Kimegawanyika katika sura 8 na kinaanza na Utangulizi unaitwa watu wa Unabii. Utangulizi - Watu wa Unabiii Utabiri na Kutamka Kabla ya Jambo kutukia. Bonde la Mifupa Mikavu Nyinyi Ndinyi Miungu Wewe ni Nabii wa Maisha Yako Ongoza Mkondo wa Maisha yako kwa Kinywa Chako Nini unapaswa kufanya na Unabii? Maongezi yako ni Mustakhabali wako Chukua hatua
2020-05-20
11 min
Amedeus Live Podcast
Rhapsodi ya Uhakika - May 2020
Pata wasaa wa kusikiliza neno la Mungu kila siku kupitia kitabu cha Rhapsodi ya Uhakika, chenye neno la kila siku. Kitabu hiki kina andikwa na Mchungaji Chris Oyahkilome na kinasomwa kwenu na Mtumishi Amedeus Deogratius.
2020-05-01
6h 40
Amedeus Live Podcast
Rhapsodi ya Uhakika April ,2020 - "Mwezi wa Maombi"
Pata Nakala mbalimbali za mwezi wa nne kama: Kuomba kwa ajili ya Nafsi Zilizopotea - April 1
2020-04-01
5h 17
Amedeus Live Podcast
Rhapsodi ya Uhakika March 2020 "Mwezi wa Maarifa"
Sikiliza neno la Mungu lilojaa maarifa, hekima na ujuzi juu ya aina ya maisha ya kiungu ambayo Mungu amekukirimia. Zipo Episode 31 kwa ajili ya kuboresha maisha yako na kukuleta katika urithi wako ndani ya Kristo. Mungu akubariki Sana.
2020-03-03
5h 15
Amedeus Live Podcast
Rhapsodi ya Uhakika - Feb. 2020 "Mwezi wa Nyimbo"
Sikiliza nakala mbalimbali za rhapsodi ya Uhakika kwa lugha ya kiswahili, kitabu kinachotoka kila mwezi na chenye neno la kila siku. Mojawapo Yale utakayosikia mwezi huu ni pamoja na Yesu Ni Adonai, Pokea, simama wima na imara, waongoze wengine katika wokovu n.k. kitabu hiki kinaandikwa na mtumishi wa Mungu MCH. Chris Oyakhilome, PhD.
2020-02-28
2h 40
Amedeus Live Podcast
Tabia za Mkristo katika Maisha ya Kila Siku
Amri mpya ni Ipi? Maungamo yako ya Kila siku ni yapi? Namna ya kutatua mafarakano au ugomvi katika maisha. Jifunze namna ya kutakasa mawazo na fikra zako. Nyanja tano kuu katika maisha za kuishi na kudhihirisha Utawala uliopewa ndani ya Kristo. .
2019-09-22
40 min
Amedeus Live Podcast
Kanuni za Mafanikio
Je, mtazamo wa Mungu ni nini kuhusu Mafanikio? Fahamu kusudi la Mungu kuhusu Mafanikio. Kanuni za Mafanikio sawa sawa na Neno la Mungu. Fungi la Kumi, Limbuko la Kwanza, Matoleo ya Hiari, Matoleo ya Mbegu (Mbegu ya Imani). Biblia inasemaje kuhusu swala la Kufanya kazi na kutokuwa tegemezi.
2019-09-21
35 min
Amedeus Live Podcast
Tumia Kinywa Chako Vyema
Kinywa chako kinatoa dira ya maisha. Uzima na mauti vipo kwenye Nguvu ya Kinywa, kwa hiyo zungumza uzima, afya, ushindi, mafanikio na yote yanayofanana na haya na wala sio mengineyo.
2019-08-29
11 min
Amedeus Live Podcast
Fanya Nguvu Ipatikane
Unaweza kuathiri ulimwengu wako kwa namna kubwa sana kupitia maombi yako. Maombi ya mwenye haki yafaa sana akiomba kwa bidiii.
2019-08-28
09 min
Amedeus Live Podcast
Noeli (Krismasi) ni Kristo Ndani Yako.
Alikuja ili iwezekane kwetu sisi kupokea fursa kufanyika kuwa wana wa Mungu. Kristo ndani yangu ni Tumaini la Utukufu.
2019-08-27
11 min
Amedeus Live Podcast
Likubali Pendo Lake
Ni kuhusiana na Pendo lake na sababu ya Kristo Kuja kuzaliwa hapa duniani. Jifunze kuhusu Pendo la kimiminika la Kristo.
2019-08-27
10 min
Amedeus Live Podcast
Kristo Pasaka Wetu
Sikiliza somo hili na upate kujua maana halisi ya neno pasaka na umuhimu wake kwenye maisha yako ya kila siku. Biblia inasema utaijua kweli na kweli itakuweka huru. Sikiliza Kweli hii nayo itakuweka huru. #Mti wa Uzima
2019-08-22
07 min
Amedeus Live Podcast
Alituleta katika Ushirika
Dhumuni kubwa zaidi lilomfanya Yesu aje duniani ni ili kutuleta katika ushirika na Baba, katika umoja na Mungu. Alikuja ili atulete katika daraja moja na Mungu.
2019-08-22
08 min
Amedeus Live Podcast
Amedeus Live
Jukwaa sahihi kwa ajili yako wewe na familia yako, ndugu, jamaa na marafiki. Jumuika nasi kila siku kujifunza neno la Mungu, kupitia rhapsodi ya Uhakika matoleo ya rika zote, fanya ukiri wa Imani kila mara na shiriki katika ibada za maombi na maombezi kwa ajili ya familia, miji,na mataifa ya ulimwengu. Hii ni podcast Yako.
2019-08-21
01 min