podcast
details
.com
Print
Share
Look for any podcast host, guest or anyone
Search
Showing episodes and shows of
Innocent Ngaoh
Shows
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Zijue Aina 05 Za Nidhamu Zenye Kuleta Mafanikio Makubwa...!
Hivi unajua Kiwango Cha Mafanikio Yako inategemea sana na Kiwango Cha Nidhamu Yako. Kupitia episode hii utajua Aina Tano za Nidhamu Zenye Kuleta matokeo Makubwa kama utazingatia na kuziishi kwenye maisha Yako. Unahitaji sana kuwa na Kiwango kikubwa Cha Nidhamu. Sikiliza na uanze kufanikiwa Kwa kuwa utaanza kuishi Kwa Nidhamu kwe ye maisha Yako.
2024-04-02
10 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Jinsi Ya KUJITAMBULISHA DM Au Kwenye Text Kwa Mara Ya Kwanza Unapomtafuta Mtu Yoyote.
Kama wewe ni wale ambao unawatumia watu DM au text za kawaida Kwa Mara ya Kwanza kama vile "Niaje, Mambo, Vipi, Shwari Mkuu, Harakati Ni Vipi Kiongozi, Mrembo mambo n.k" Tambua unakosea sana Tena sana hiyo siyo Kujitambulisha badala ni salamu tu. Swali linakuja unajua jinsi ya Kujitambulisha mtu akiona DM au text Yako apate kuijibu bila kupuuzia. Unahitaji kuzingatia maeneo matano wakati unamuandika Mtu DM Yako; 1. Jina la mtu unayemtumia ujumbe wako. 2. Jina lako. 3. Shughuli Yako. 4. Hitaji au shida Yako. 5. Hitimisho. Ukizingatia mambo yote hayo DM zako zitajibiwa mpaka ushangae. Kwa mfano... "Habari kaka Amos Nyanda naitwa Innocent...
2024-03-14
08 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Jinsi Ya Kuamini UWEZO Wako Na Kuamini Katika Wewe...!
Umekosa sapoti au kushikwa mkono Katika kazi zako au mapambano Yako? Unapitia hali ya kukataliwa na kuona hakuna anayejua thamani Yako Wala Kuamini Katika Wewe? Unapitia hali ya kukata tamaa kwenye kitu unachofanya kwa kuwa matokeo yamechelewa. Unatamani kuwa Bora ila hujui ufanye Nini? Kuna watu wanakurudisha nyuma na kutoamini katika mapambano Yako ila unashindwa kuwaondoa kwa sababu yoyote Ile. Basi... Episode hii itakupa nguvu na maarifa sahihi ya kuonyesha Uwezo Wako na Kuamini Katika Wewe yaani "BELIEVE IN YOURSELF." Sikiliza na ujifunze
2024-03-05
10 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Jinsi Ya Kumla TEMBO Mzima Bila Kubakisha Hata Mfupa...!
Kama unataka Kutimiza Malengo yako Unahitaji kwanza kula Tembo mzima bila kumbakisha mfupa wala mkia. Sikiliza episode mpaka mwisho na ujifunze. Kula Tembo nzima Tumia mbinu ya SYSTEMATIC APPROACH
2024-02-28
08 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Ijue Kanuni Ya ATM Na Ubadili Maisha Yako...!
Hiyo siyo ATM ya kutoa Hela, ni tofauti na ATM unazozijua kwa sababu Kanuni ya ATM itakusaidia kujua maeneo matatu ya kuboresha Maisha Yako kwa asilimia 100% Sikiliza na ujifunze.
2024-02-21
09 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Jinsi Ya Kuacha Tabia Ya Kuwasema Watu Wengine Vibaya...!
Umekuwa na tabia ya kuwasema watu wengine kwa namna yoyote kwenye maisha yao? Hii ni tabia mbaya, lakini hujui ufanye nini ili uache tabia hii ya kimaskini na ni tabia mbaya. Inawezekana siyo wewe ila kuna watu wa karibu yako wana tabia hii, basi kupitia maarifa haya utaweza kuwa chachu ya kubadilika kwake. Huwezi kumbadilisha mtu ila unaweza kuwa sababu ya yeye kubadilika kama atakuwa tayari kubadilika. Kwahiyo... Unahitaji sana kuacha tabia ya kuwasema watu wengine vibaya kwa namna yoyote. Kwa sababu ni tabia ambavyo inafanya upoteze uaminifu na kuonekana ni mtu wa hovyo. Hata kuharibu mahusiano yako na watu...
2024-02-15
09 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Maswali Sita (06) Ya Kuepuka Kumuuliza Mtu Ambaye Hujakutana Nae Muda Mrefu...!
Uungwana ni kuangalia ni maswali gani hupaswi kumuuliza mtu ambaye hujakutana nae muda mrefu, kwa sababu ukiuliza moja maoja unaonakena mtu ambaye hujielewi na hujui nini uzungumze kutoka na eneo ambalo upo.
2024-02-10
15 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Jinsi Dada Wa Kazi (House Girl) Alivyoninywesha Sumu Ya Panya Ili Nife...!
Dada wa kazi alivyotaka kuniua kwa imani za kishirikina kwa kuninywesha sumu ya Panya nikidhani ni dawa. Sikiliza mkasa huu ujifunze kitu kuhusu dada wa kazi na vimbwanga vyao.
2024-02-07
11 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Kwanini Ulale Na Diary Kwenye Chumbani Au Kitandani Kwako..!
Ukiwa chumbani kwako ni sehemu pekee ya kuwa diary 📔 Au daftari ili uweze kuandika ndoto ambazo unaota na mawazo yako ili usiwe kusahau. Sikiliza episode hii ujifunze
2024-02-03
07 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Uchambuzi Wa Kitabu Cha WHO MOVED MY CHEESE? (Nani Kahamisha Jibini Yangu?)
Nani kahamisha jibini yangu? Ni kitabu ambacho kinakusaidia kukabaliana na mabadiliko ambayo hukutarajia wala kutegemea kwenye kazi na maisha. Kitabu kipo kwa mfumo wa stori ambao inahusisha wahusika wanne ambao ni 1. Sniff 2. Scurry 3. Hem 4. Hew Ni kitabu ambacho utajifunza namna ya kukabiliana na mabadiliko kwenye maisha. Naamini kupitia uchambuzi wa kitabu hiki utafurahia Sana.
2024-01-31
27 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Jinsi Ya Kuachilia Vitu Na Watu Ambao Wamekuumiza Na Hawatambui Thamani Yako...!
Kuachilia haijawahi kuwa jambo rahisi hasa kwa watu ambao umewathamani na kuamini wangekuwa na wewe maisha yako yote, lakini ghafla wanakuachia maumivu na kukuumiza kiakili, kimwili, kihisia. Inaumiza kuona hawatambui thamani yako na unashindwa kuachikilia na kuishia kuwa na roho ya kutaka kulipa kisasi, uchungu, hasira, msongo wa mawazo na kujichukia. Lakini... Kupitia episode hii utaweza kuachilia na kwa kujua nini ufanye ili uweze kuachilia na kuishi maisha ya furaha na amani ya moyo. Jifunze kuachilia.
2024-01-27
14 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Uchambuzi Wa Kitabu Cha MONEY FORMULA (Kanuni Za Fedha)...!
Elimu ya fedha isiyofundishwa shuleni wala vyuo vikuu imepelekea kushindwa kupiga hatua kwenye eneo la fedha. Kitabu cha MONEY FORMULA kinakupa mwongozo sahihi ni kwa namna gani unaweza kufanikiwa kifedha kupitia sheria, kanuni na mitazamo sahihi kuhusu fedha. Hakikisha unafanyia kazi ambayo unajifunza.
2024-01-24
29 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Uchambuzi Wa Kitabu Cha THE RICHEST MAN FROM BABYLON (Tajiri Kutoka Babeli) Kwa Lugha Ya Kiswahili..
Unataka kufanikiwa kifedha na kuwa tajiri basi kitabu cha THE RICHEST MAN FROM BABYLON kitakupa mwongozo na sheria za fedha. Uchambuzi wa sura 11 ambazo utapata kwenye episode hii. Hakikisha unaandika pembeni ambayo utajifunza rafiki.
2024-01-21
46 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Kwanini Unataka Kuongeza Au Kupunguza Maumbile Ya Mwili Wako...!
Umekuwa na fikra kuwa ukiongeza au ukipunguza maumbile ya mwili wako basi utakuwa umekamilika na hautakuwa na kasoro hata kidogo si ndiyo? Basi Sikiliza episode hii ujifunze madhara ya kutaka kuongeza au kupunguza maumbile yako.
2024-01-15
13 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Uchambuzi Wa Kitabu Cha "BIRD BY BIRD"
Ni kitabu mahususi kimeandikwa na Anne Lemmot ambacho utajifunza mambo mengi kuhusu uandishi wa vitabu na kuishi maisha yenye uhuru ndani yake. Hakikisha unaandika pembeni mambo ambayo utajifunza kupitia uchambuzi wa kitabu hiki kizuri cha BIRD BY BIRD yaani NDEGE KWA NDEGE. Katika uchambuzi wa kitabu hiki utajifunza sura tano ambazo mwandishi ametushirikisha kuhusu uandishi wa vitabu na ndani ya sehemu hizo zimegwanyikwa part ndogo ndogo. Ni kitabu kizuri kama unataka kuwa mwandishi mzuri wa Riwaya, Hadithi, Simulizi, Makala Na Vitabu Aina Yoyote basi uchambuzi ni mahususi kwako. Kitabu cha BIRD BY BIRD ni kitabu kizuri basi unahitaji sana kusoma...
2024-01-11
31 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Sababu 06 Za Kwanini Unaweza Kutimiza Malengo Yako Ya Mwaka 2024
Dakika 18 za kubadili kila kitu na uanze kuchukua hatua ili utimize malengo yako kwa kishindo. Utajifunza mambo 06 ili ufanikishe mwaka 2024 kwa matokeo chanya na mafanikip makubwa
2024-01-07
18 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Ufanye Nini Unapitia Hali Ya Kutoeleweka Katika Mapambano Au Utafutaji Wako?...
Usijisikie vibaya kuona watu wa karibu au wa mbali hawaelewi wala hawapo tayari kukuelewa kuhusu mapambano yako. Inaumiza kuona watu ambao unawapenda na kuamini inaweza kuwa, 📌 Wazazi wako, Ulitegemea ndiyo wangekuwa watu wa kwanza kukuelewa na kuamini unachofanya na imekuwa tofauti wanakukosoa na kukalaumu kwanini unafanya hicho. 📌 Marafiki zako, Marafiki ambao umeshindana nao muda mwingi wanakuwa hawaamini unachofanya na hawaelewi mapambano yako na kuona unapoteza muda au pengine unapoteza muda au hutopata matokeo. 📌 Viongozi au boss wako, Inawezekana ni watu ambao unataka waelewe juhudi na kujitoa tofauti ila inakuwa tofauti wanakuwa hawaelewi na zaidi wanaona hujielewi inaumiza sana. 📌 Ndugu zako, Ndugu wanaku...
2023-12-31
14 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Kabla Ya Kuingia Mwaka 2024 Hakikisha Unafanya Haya..!
Umepanga kufanya maajabu mwaka 2024 na umejipanga vizuri kuanzia kupanga malengo yako, ndoto na maono yako. Lakini kuna vitu unapaswa kuzingatia kufanya leo hii kabla ya kuingia mwaka 2024. Utajifunza mambo 05 ambayo yatakusaidia kujua nini ufanye kabla ya kuingia mwaka 2024.
2023-12-17
16 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Jinsi Ya Kupata Nguvu Ya KIBALI Cha Kukubalika Machoni Pa Watu...!
Unahitaji kukubalika kwenye jambo lolote basi unahitaji sana NGUVU YA KIBALI. Mahali popote hakikisha unaishi vizuri na watu ndiyo maana wahenga wanasema "Mtaji wa mtu ni watu. Ufanye nini upate nguvu ya kibali cha kukubalika machoni pa watu? Sikiliza episode hii mpaka mwisho. Share | Like | Comment | Ask
2023-12-11
16 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Namna Rahisi Ya Kujenga Uwezo Wa Kujiamini Na Ujasiri...!
Zijue mbinu 07 za kuongeza uwezo wako wa kujiamini na mwenye ujasiri mkubwa kwa kushinda hofu, wasiwasi, uoga na kujitilia mashaka. Sikiliza episode hii mpaka mwisho na uwezo kujua mbinu za kuwa mtu mwenye kujiamini
2023-12-03
21 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
ISHI KAMA KINYONGA....!
Unajiuliza uishi kama kinyonga ni kwa namna gani si ndiyo? Ni kwamba unahitaji kuwa makini na kuishi kwa tahadhari kama kinyonga na watu wanakuzunguka hasa watu wa karibu yako. Hata wahenga wanasema “Adui hatoki mbali” Sikiliza dakika 9 zenye kukupa mwanga na mabadiliko kwenye Maisha yako. Ushindwe wewe tu rafiki.
2023-11-26
09 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Jinsi Kanuni Ya 80/20 Inavyokusaidia Kutoeleza Matatizo Yako Kwa Kila Mtu...!
Hivi unajua asilimia 80% ya watu unawaeleza matatizo yako hawajali kabisa na asilimia 20% wanafurahi kuona matatizo hayo yanakupata wewe hapo. Kanuni ya 80/20 itakusaidia kuchuja nani wa kuwaeleza matatizo yako na wapi kutowaeleza. Unajiuliza ni kwa namna gani Kanuni hii inafanya kazi si ndiyo? Basi Sikiliza episode hii mpaka mwisho ujifunze
2023-11-18
09 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Sababu 05 Zinazofanya Watu Wakudharau...!
Hakuna kitu kinaumiza kama watu kukudharau na kubeza uwepo wako si ndiyo? Dharau ina maana kwamba wanachukulia poa jambo au kitu fulani pasipo kukipa thamani inayostahili. Hivi unajua kwanini watu wanakudharau? Ukweli ni kwamba huwezi kuwa mwema na mzuri kwa kila mtu ila inakuwa inaumiza zaidi pale watu ambao umewapa nafasi kubwa kwenye maisha yako halafu wanakudharau. Inaumiza sana si ndiyo? Kuna baadhi ya sababu ambazo zinafanya watu wakudharau na ukiweza ku-deal nazo basi dharau zitatoweka na wataanza kukuthamani; 1. Furaha yako isiwategemee wao, Wanakudharau kwa sababu wanajua unawategemea wao ili uwe na furaha kwenye maisha yako, Anza sasa kujipa furaha...
2023-11-09
13 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Mambo 05 Ya Kuzingatia Kabla Ya Kumpenda Mtu Kimahusiano Ya Kimapenzi....!
Mahusiano siyo jambo la ulazima ila mahusiano ni jambo la utayari. Mapenzi siyo upofu, ila ni mtazamo wako Kuwa ni upofu wakati umepewa macho uone, akili ili uchanganue na hisia ili ujitathimini. Unajua nini uzingatie kabla ya kuingia/kuanzisha mahusiano ya kimapenzi, basi sikiliza episode hii mpaka mwisho ujifunze
2023-11-01
14 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Aina 10 Za Ujuzi Ambazo Zitakuingizia PESA (High Income Skills)...!
Unataka kuingiza pesa na kujikwamua kiuchumi? Kama jibu lako ni ndiyo, basi episode hii inakufaa kwa sababu utaenda kujua aina 10 za Ujuzi ambazo zitakuingizia pesa ni wewe kuchagua Ujuzi mmoja au miwili kisha weka nguvu hapo baada ya mwaka mmoja hadi mitano utaona unaingiza pesa ni uthubutu wako tu. Sikiliza kwa umakini sana
2023-10-22
16 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Mjue Leo Mchawi Wa Mafanikio Yako Ndani Ya Dakika 11...!
Hivi unajua kwamba wewe ni mtabiri wa maisha yako? Wahenga wanasema “Every human is magician” wakiwa na maana kila mtu ni mchawi Unajiuliza ni kwa namna gani? Sikiliza episode hii ujue mchawi wa mafanikio yako.
2023-10-09
11 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Ijue Nguvu Ya Mchakato..!
Ukijua nguvu ya mchakato kwenye maisha yako utapata kuelewa upata kuhusu mafanikio, maendeleo, ukuaji, mabadiliko na kila kitu kinahitaji mchakato. Unataka kujua mchakato haupukeki ni lazima mchakato upitie. Sikiliza episode hii mpaka mwisho ujue nguvu ya mchakato.
2023-09-27
09 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Mambo 05 Ya Kufanya Ili Ubadili Maisha Yako Kwa Asilimia 100%...!
Kila mtu anataka kupata mabadiliko chanya ambayo yanafanya anapiga hatua na pengine hata wewe kuna mabadiliko ukifanya utaweza kupiga hatua. Swali la kujiuliza unajua ni mambo gani ufanye ili upate mabadiliko unayoyataka kwenye maisha Yako? Sikiliza episode hii mpaka mwisho ujifunze.
2023-09-22
11 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Kwanini Unahitaji Kusoma Kitabu Cha Sayansi Ya Malengo...!
Kitabu cha sayansi ya malengo ni kitabu bora ambacho kitakusaidia Kutimiza Malengo yako mara 10X zaidi ya unavyotimiza sasa. Wasiliana na mimi 0674698347 kupata kitabu chako cha Sayansi ya malengo
2023-09-13
13 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Jinsi Ya Kuonyesha Kipaji Chako Hadi Kukupa Matokeo Makubwa...!
Hivi unakijua kipaji chako au kikubwa ni uhai? Pasipo kujali unajua au hujui kipaji chako ila tambua una zawadi ya kipaji ambayo ulipewa na Mungu hata kabla ya kuzaliwa kwako. Kwahiyo... Kuzaliwa kwako Ina maana una kipaji ndani yako. Swali la kujiuliza. Je, unakijua kipaji chako? Hongera kwa kujua kipaji chako cha .... (Taja kimoyomoyo) Ina maana tayari umeshajua kusudi la kuzaliwa kwako. KIPAJI = KUSUDI. Lakini... Kujua kipaji chako haitoshi ni lazima uonyeshe kipaji chako kwa ulimwengu yaani dunia itambue na kunufaika na kipaji chako. Kwa sababu... Kipaji siyo kwa ajili yako bali ni kwajili ya kuwatumikia wengine. Unajiuliza ni kwa...
2023-08-26
12 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Namna Rahisi Ya Kunoa Kipaji Chako Na Kukupa Mafanikio Makubwa...!
Kipaji ni kama msuli kadiri unavyofanya mazoezi ndiyo msuli unakuwa mkubwa na wenye nguvu si ndiyo? Basi episode hii utajua namna rahisi ya kunoa kipaji chako kiwe kikubwa na kukupa mafanikio makubwa...!
2023-08-18
14 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Njia 04 Za Kugundua Kipaji Chako...!
Umebarikiwa zawadi ya kipaji ndani yako pasipo kujali unajua au hujui, lakini una kipaji umebeba ndani yako. Kwahiyo Ondoa mtazamo kuwa hauna kipaji na Upo Upo tu au kuna kundi la watu wachache ndiyo wana vipaji na wewe hauna. Hii episode itakusaidia kujibu swali Muhimu “Nitajuaje kipaji changu” kwa sababu njia hizi 04 ni uhakika kujua na kugundua kipaji chako kwa asilimia 100% nakutakia Safari njema ya kuanza kukiishi kipaji chako baada ya kukigundua.
2023-08-09
12 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Jinsi Ya Kuwa Na Muendelezo (Consistency) Ya Kumaliza Kile Kitu Ulichokianzisha...!
Utajifunza Siri 04 za kuwa muendelezo kwenye kitu unachofanya pasipo kuishia njiani. Utaweza kujua kwanini kuanza ni Muhimu ila kumaliza kile ulichoanzisha ndiyo Muhimu zaidi. Episode hii Ina kila kitu cha kufanya wewe uwe na muendelezo na siyo kuwa mghairishaji sugu kwa kutomiza kile ambacho umekianzisha. Muendelezo ni mama na baba wa Mafanikio ya watu wote duniani
2023-08-02
14 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Tumia Kanuni Ya 80/20 Ili Utimize Malengo Yako Kwa Kishindo....!
Ijue kanuni yenye maajabu ambayo itakusaidia kutimiza malengo yako makubwa pasipo kuwa na kisingizo chochote, dakika kumi na mbili za kuijua kanuni hii kazi kwako.
2023-07-24
12 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Njia 04 Za Kugundua Kusudi La Kuzaliwa Kwako Hapa Duniani...!
Kabla ya kuona hauna thamani au umezaliwa kwa bahati mbaya, ukweli ni kwamba wewe umezaliwa na kusudi ndani yako, Je unajua kusudi la kuzaliwa kwako?
2023-07-19
14 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Siri 04 Za Kujua Leo Ili Uishi Maisha Ya Furaha Na Amani Ya Moyo...!
Kabla ya kutaka watu wengine wakupe furaha kwenye maisha yako, tambua mtu pekee wa kukupa furaha halisi ni wewe hivyo ni wajibu wako asilimia 100% kujua nini ufanye ili uwe na furaha na amani ya moyo.
2023-07-12
09 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Sababu 04 Za Kwanini Unahitaji Ujuzi Wa “Copywriting” Kama Unataka Kuuza Kwenye Mitandao Ya Kijamii.
Ujuzi wa Copywriting ni ujuzi Muhimu kuwa nao kama unataka kufanya vizuri kwenye mitandao ya kijamii. Unajiuliza kwanini Netflix wanauza movies zao kuliko makampuni mengine? Unajua kwanini kampuni ya Apple inaongoza kwa mauzo makubwa ya bidhaa zao? Unajua kwanini unanunua bidhaa na kusoma tangazo kwenye mitandao ya kijamii? Ni kwa sababu... Ujuzi wa Copywriting ambao unauza chochote kupitia maandishi pasipo kufungua mdomo na kuongea neno moja... ....hata video ambazo unatazama kuna script inaandikwa ambayo ujuzi wa Copywriting inafanya kazi yake. Kusikiliza muziki tambua ni Ujuzi wa Copywriting unatumia kuandika nyimbo ya msanii. Kwahiyo.... Upende au usipende unahitaji sana Ujuzi huu...
2023-07-05
12 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Jinsi Ya Kuwa Mvumilivu Na Kuishinda Hali Ya Kukata Tamaa, Ili Utimize Malengo Yako...!
Hata upate sababu milioni za kukata tamaa kwenye maisha yako, jitahidi kutafuta sababu moja ya kusonga mbele pasipo kukata tamaa. Kwa sababu... Kukata tamaa haifanyi maisha kuwa rahisi hata kidogo, ni lazima upambane kwa asilimia 100% kutimiza malengo yako, maana ingekuwa rahisi basi kila mtu anagetimiza malengo yake si ndiyo? Unakumbuka mwaka mpya ulisema huu ndiyo mwaka wa kupiga hatua na kutimiza malengo kwa kishindo. Swali la kujiuliza, Je, umetimza malengo yako kwa asilimia ngapi? Jibu baki nalo. Kutimiza mlengo ni mchakato na siyo tukio la usiku mmoja, ndiyo sababu ya watu wengi kukata tamaa kirahisi na kukosa uvumilivu wa kusubiri...
2023-06-29
11 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Aina 05 Za Marafiki Wa Kuwapiga Chini Ili Uishi Maisha Ya Furaha...?
Kuna marafiki ukiwa nao unapoteza furaha ya maisha na unadumaa kwa kutopiga hatua, inawezekana wewe ni shahidi wa hili si ndiyo? Vizuri kwa kujibu ndiyo. Kwahiyo... Una haki ya kuwapiga chini aina fulani ya marafiki siyo ubaya, lakini kwa kujali furaha ya moyo wako na shauku ya kupiga hatua zaidi kwenye maisha yako Hivi... Unajisikiaje rafiki yako wa karibu anakusema vibaya wakati haupo na kukutangaza kwa mabaya kwa watu wengine? Utajisikia vibaya si ndiyo? Kwa sababu... Utamuona ni snitch na mtu mnafiki ambaye hapaswi kuwa rafiki yako kabisa na kuwa tayari kumpiga chini maana siyo rafiki mzuri kabisa. Hata ingekuwa...
2023-06-24
13 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Siri 05 Za Kujua Ili Uwe Bora Mara 10X Zaidi Ya Ulivyo Sasa...!
vuta picha unakuwa bora mara kumi zaidi ya ulivyo sasa ukuwaje? hiyo picha unayopata unaweza kuwa hivyo ni suala la uthubutu na kufanyia kazi ambayo utajifunza kupitia episode hii. kuwa na uhakika utakuwa bora mara 10X zaidi kwa kujua siri ambazo nimekushirikisha siku ya leo.
2023-06-20
15 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Njia 04 Za Kujua Ili Kuacha Tabia Ya Kuwaridhisha Watu Wengine...!
Tabia au hali ya kutaka kuwaridhisha watu wengine imekuwa sababu kubwa ya kutoishi maisha ya furaha na amani ya moyo. Na unajua hakuna faida yeyote unapata kwa kuridhisha watu wengine si ndiyo? Basi dakika 10 kutoka sasa baada ya Kusikiliza episode hii utaenda kuwa mtu wa kitofauti.
2023-06-14
10 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Jinsi Ya Kuacha Tabia ya Kujilinganisha Na Watu Wengine....!
Hivi kuna faida yeyote unapata kwa Kujilinganisha Na kutaka kuwa kama watu wengine jinsi walivyo kwenye maisha yako? Kwa sababu... Kujilinganisha ndio sababu ya kupoteza furaha, kukosa amani ya moyo, kuona umechelewa na Hakuna cha maana umefanya. Kumbuka kuwa... Ukitaka kuishi maisha ya mtu mwingine kwenye maisha yako, Je maisha yako atayaishi nani? Umeshapata jibu si ndiyo? Kuna sababu nyingi za kwanini una tabia ya kulinganisha na watu wengine: 1. Wana ushawishi mkubwa katika mitandao ya kijamii, 2. Kuvaa nguo nzuri na kutumia “Luxury things”, 3. Wana mafanikio makubwa kukuzidi, 4. Wana kibali cha kukubalika zaidi kuliko wewe kwenye kitu unachofanya. 5. Maarifa na hekima kubw...
2023-03-30
13 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Mambo 05 Ya Kufanya Ili Uwe Na Matumizi Mazuri Ya Muda Wako...!
Tuna masaa 24 ambayo yanatutofautisha kati ya mtu mmoja na mwingine kwa namna ambavyo tunatumia muda. Huna muda wa kupoteza kwa kufanya mambo yasiyo Muhimu na msingi kwako na kuacha kufanya mambo ya msingi na Muhimu kwenye maisha yako. Kwani hujui muda ukienda umeenda na hauna mbadala? Kwani hujui future yako inajengwa na nini unafanya kwenye dakika tano zijazo? Kwani hujui wewe ndiyo unapaswa kutumia masaa 24 vizuri Ili upige hatua kwenye maisha yako? Ndio maana unahitaji kuwa na nidhamu ya muda ila unajua faida ya Kutumia muda wako vizuri, lakini unapuuzia si ndiyo? Lakini... Leo utajua mambo matano ambayo ukizingatia basi...
2023-03-20
13 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Aina Tano (05) Ya Marafiki Ambao Hupaswi Kuwapoteza...!
Hivi unajua kuna Marafiki ukiwa nao ni zaidi ya Baraka kubwa maishani pia kuna aina ya Marafiki ukiwa nao ni mwanzo wa kukaribisha majanga. Unajua kwamba... Wewe ni wastani wa Marafiki sita ambao unashinda nao muda mwingi. Hata kama hupendi au hauna marafiki, lakini bado unahitaji watu si ndiyo? Na watu hawa wakiwa na sifa fulani fulani ni Muhimu kuwatunza maana tupo zama tumezungukwa na Marafiki au watu ambao ni wanafiki sana... ...kuna aina tano za Marafiki ambao ukiwa nao ni zaidi ya Baraka kutoka wa Mungu maana ni Adimu zaidi ya Dhahabu kwenye machimbo ya Chunya pale Mbeya. Ha...
2023-03-07
15 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Sababu Kuu 04 Za Kwanini Unachepuka...?
Hivi unajua kwamba asilimia 20% watu wanachepuka kwenye mahusiano yao, asilimia 30% wapo katika mahusiano ambayo wameyachoka tayari... Asilimia 20% wapo kwenye mahusiano na mume au mke wa mtu, asilimia 15% wapo single lakini wanachepuka na Ex wako. Asilimia 5% wapo single na asilimia 10% tu ndiyo wanafurahia mahusiano yao. Tatizo la kuchepuka ni tatizo kubwa sana ambalo si wanawake au wanaume kiwango cha kuchepuka kinaongezeka siku hadi siku. Swali la kujiuliza... Kwanini unachepuka? Kuna sababu nyingi ambazo zinafanya watu kuchepuka ukiachana na suala la fedha, kuna sababu zifuatazo; 1. Kukosa tendo la ndoa (Sex) kwa muda mrefu Labda mwanaume ana changamoto ya nguvu za kiume au...
2023-02-22
14 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Faida Za Kuandika ‘TO DO LIST’ Ya Kutimiza Malengo Yako.
Umekuwa unashindwa kutimiza malengo yako na kuishia kupoteza hamasa ya kuendelea kupambana kwa kuona haiwezekani? Una malengo makubwa sana ambayo unaona haiwezekani kuyatimiza? Sio kosa lako. Kwa sababu siyo wewe pekee yako ambaye unashindwa kutimiza malengo yako. Lakini... Tatizo kubwa kwa kushindwa kutimiza malengo yako inafanya watu wengi inawezekana Hata wewe unaweka visingizio kuwa siyo mwaka wako labda mwakani ndiyo wako, unalalamika kila wakati kutafuta huruma ya watu wengine. Ukweli haisaidii zaidi unakaribisha UMASKINI na MAJUTO. Umeamua kabisa kughairisha na kusema mwakani ndiyo utapambana, kwani haujui kesho siyo yako na yako sio kesho? Habari njema ni kwamba... Hata kama umepoteza...
2023-02-15
12 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Jinsi Akili Yako Inavyofanya Kazi Na Namna Inaweza Kuboresha Maisha Yako.
Akili yako inawajibika kupokea, kutunza na kuchakata TAARIFA ambazo zinatoka sehemu mbalimbali za mwili. Akili haipimwi kwa alama za darasani. Akili haipimwi kwa cheo ambacho mtu anapata. Akili haipimwi kwa umri ambao unao. Akili haipimwi kwa kukubalika na watu. Kwa bahati mbaya.... Hakuna sehemu ambayo wanaeleza jinsi gani akili inafanya kazi zaidi ya kukueleza kuwa na fikra au mawazo chanya si ndiyo? Kumbe akili yako ni zaidi ya wewe unavyofikiria kuwa una akili, hebu jiulize ni kitu gani kinaonyesha una akili? Majibu yako utajua sahihi au siyo kwa kuendelea kusoma. Lakini akili yenyewe inafanyia kazi TAARIFA ambazo zinakuwa zipo katika...
2023-01-31
17 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Sababu Nne (04) Za Kwanini Unashindwa Kutimiza Malengo Yako.
Unaweza kutimiza malengo yako, kama utajua mbinu sahihi ambazo ni chachu ya kutimiza malengo yako. Lakini... Kuna sababu ambazo zinafanya watu wengi washindwe kutimiza malengo yako, inawezekana hata wewe mwaka 2022 ulishindwa kutimiza malengo yako kwa sababu fulani fulani si ndiyo? Kutimiza malengo siyo ajali bali ni mchakato mtalaamu. Kati ya sababu hizi inaweza kuwa chachu ya kushindwa kutimiza malengo yako; 1. Kutojua umuhimu wa kuwa na malengo, Unaishi kwa mazoea kutojua umuhimu wa malengo, kwa sababu Hakuna shule au chuo inafundisha umuhimu wa kuishi kwa malengo katika maisha yako, na kuishia kuwa na ndoto na matamanio tu. 2. Kutojua umuhimu wa kupanga...
2023-01-23
18 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Tabia Tano (05) Za Kuepuka Ili Utimize Malengo Yako.
Tabia Ina nafasi ya moja kwa moja ya wewe kutimiza au kutotimiza malengo yako, kwa bahati mbaya watu wengi wanachukulia poa sana suala la tabia. Ukitazama elimu kuhusu tabia gani zinaleta mafanikio na kutimiza malengo yako kwa kishindo haitolewi kwa ukubwa zaidi katika mazingira ambayo tupo. Unauliza “Innocent” ni kwa namna gani? Swali zuri Mtaalamu. Ni hivi.... Kuna tabia ambazo zilifanya utimize malengo yako ya mwaka 2022? Kuna tabia ambazo zilifanya ushindwe kutimiza malengo yako ya mwaka 2022? Vizuri, kwa kupata majibu na umeanza kuona tabia Ina nafasi kubwa ya kutimiza au kutotimiza malengo yako. Kwa mifano; Mfano wa kwanza. Je mtu ataw...
2023-01-16
19 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Jinsi Kanuni Ya 3K’s Inavyojenga Hatima Ya Maisha Yako.
Watu ni hodari wa kupanga mipango kikubwa si ndiyo? Watu ni hodari sana wa kupanga malengo makubwa si ndiyo? Una Kumbuka hata siku ya mwaka mpya ulipanga malengo makubwa na kusema huu ni mwaka wako si ndiyo? Lakini... Watu wengi licha ya kujua kupanga, wanashindwa sehemu mbili ambazo ni; 1. Kuamua/kuthubutu. 2. Kutenda. Hebu fikiria ukiamua kupambania mipango na malengo yako utakuwa wapi? Haitoshi si ndiyo... Ni lazima utende kwa maana kuchukua hatua (To take take actions) baada ya kuamua kupambania malengo yako si ndiyo? Kwahiyo.... Leo utaenda kujua kanuni ya 3K’s ambayo itaenda kubadili hatima yako na kuwa mtu mw...
2023-01-09
13 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Hatua Saba (07) Za Kuzingatia Wakati Unapanga Malengo Ya Mwaka 2023.
Kabla ya kusema mwaka 2023 ni mwaka wa wewe kupiga hatua na kufanikiwa kwa kiwango cha juu kwa kutimiza malengo yako. Jiulize mpaka sasa, umeshapanga malengo yako ya mwaka 2023? Au. Unataka kupiga hatua lakini Hakuna hata malengo ambayo umeandika kwenye diary yako, nikuambie haupo “Serious” kabisa. Hebu kuwa Serious kidogo basi... Sababu unakuwa bado hauna malengo, badala yake unakuwa na matamanio na ndoto za kutaka kitu fulani pasipo kujua namna ya kupata. Ni hivi... Kupanga malengo yako kiusahihi na kuyaandika malengo yako unaongeza nafasi ya kufanikiwa kwa asilimia 42% kuliko ambaye hajaandika kabisa malengo yake. Kwahiyo... Kama Unataka mwaka 2023 Uwe mwaka wa kupi...
2023-01-02
21 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Mambo Manne (04) Muhimu Ya Kufanya Mwaka 2023 Ili Uwe Mwaka Wa Mafanikio.
Fanya yote siku ya leo, lakini hakikisha unasikiliza episode hii. Unajua ni kwanini nakuambia hivyo? Kwa sababu sitaki uwe kwenye kundi la watu ambao mwaka 2023 unakuwa msindikizaji wa watu wengine. Eeeh! Unashangaa ni hivi... Nimezungumzia kitu kinaitwa “High income skills” ambayo ni Muhimu kuijua na utaijua baada ya wewe kusikiliza. Utaelewa “Smart Goals” yaani malengo smart unayajua, utajua kwa Kusikiliza episode hii sababu unaweza sema una malengo kumbe hauna badala yake una matamanio na ndoto. Unajua umuhimu wa kufanya “Self analysis” kwa maana tathimini binafsi, utaelewa kwa kina baada ya kusikiliza. Hii episode maalamu kwa ajili ya mafanikio yako ya mwaka 2023 B...
2022-12-28
17 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Maeneo Matano (06) Ya Kuzingatia Ili Ujitambue Kwa Kiwango Cha Juu Kwenye Maisha Yako.
Kujitambua ni nini? Kujitambua, ni uwezo wa kujifahamu/kujijua wewe ni nani unapaswa kufanya nini na kwa wakati gani. Usipojitambua wewe ni nani tambua watu ambao wamejitambua kukutumia wewe kutimiza malengo yao, ndoto zao pamoja na maono yao. Kwahiyo... Kujitambua ni wajibu wako wa asilimia 100% siyo kujitambua tu badala yake kujitambua kwa kiwango cha juu. Dhana potofu kudhani kujitambua ni kuwa na umri mkubwa, cheo kikubwa, nyazifa fulani, kiwango cha elimu n.k hii siyo ishara kuwa unajitambua kwa kiwango cha juu. “Usipogundua kusudi lako, bado hujaanza kuishi maisha ambayo unapaswa kuishi hapa duniani”- Lolo_facts. Swali ya kujiuliza.... 1. Unaj...
2022-12-21
18 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Sababu Sita (06) Za Kwanini Unaweza Ku-move On Kwenye Mahusiano Ambayo Siyo Sahihi.
Unajisikiaje mtu ambaye unampenda kwa moyo wote anakusaliti na anakupa visingizio kuwa shetani alimpitia. Hakuna usaliti unafanywa kwa bahati mbaya. Kila siku ni mtu wa kupasha viporo na ex wake kwa kusema toka tuachane umekuwa na umbo namba nane la kibantu... ...toka muachane amekuwa mkaka “Handsome” unasema hapa ndiyo penyewe. Unajua kabisa siyo mtu sahihi kabisa kwako lakini kila siku unang’ang’ania kusema labda kuna siku atabadilika Swali la kujiuliza... Toka lini mtu akaweza kumbadilisha mtu mwingine? Jibu ni hapana badala yake ni unaweza kuwa daraja la yeye kubadilika. Lakini... Una uwezo mkubwa wa ku-move on kwenye mahusiano ambayo siyo sah...
2022-12-02
23 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Mambo Matano (05) Ambayo Hupaswi Kulazimisha Kwenye Mahusiano.
Mahusiano hayawahi kuwa mabaya hata siku moja, shida ni watu ambao wanaingia kwenye mahusiano. Hivi Mahusiano ni nini? Lakini... Hakuna maana rasmi ya mahusiano kwa sababu kila mtu ana tafsiri yake, lakini tafsiri yako ni sahihi au ya kufuata mkumbo. Leo hii imekuwa ni kawaida... Kusema wanaume wote ni mbwa kwa sababu ya mwanaume mmoja kukusaliti kwenye mahusiano. Kusema wanawake wote ni malaya kwa sababu ya mwanamke mmoja kukufanyika tafrani kwenye mahusiano kiasi unawachukia wanawake wote. Umewahi kusikia Tanga wanasema “Mahusiano ni matamu kama asali mkiwa mnapendana”... ...vijana wanasema “Tanga ndiyo mapenzi yaliyokazaliwa” wana maneno sana, hahaha! Ngoja nikuambie ukweli tu... Ma...
2022-11-23
16 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Jinsi Ya Kushinda Roho Ya Kukata Tamaa Hata Pale Unapopata Hali Ya Kukata Tamaa.
Je, umekuwa unakata tamaa kirahisi? Je, umekuwa una pata roho ya kukata tamaa kwenye maisha yako? Je, unaamini huwezi kuendelea tena kwenye kitu unachofanya (Taja kimoyo moyo) na kuona ni bora uache kwa kukatatamaa? Lakini... Kumbuka kukata tamaa haifanyi maisha yako kuwa rahisi hata kidogo. Episode hii itaenda kuvunja kila kitu na roho ya kukata tamaa haitakuwa sehemu ya maisha yako tena. Kukata tamaa ni dhambi mbaya sana lakini unaweza kushinda roho ya kukata tamaa pasipo kujali nini unapitia kwa sasa kwenye maisha yako.... ....na kuwa na hamasa kubwa kutoka ndani, ujasiri pamoja na uvumilivu kwa kuamini unaweza kupiga hatua...
2022-11-04
22 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Mambo Matano (05) Ya Kufanya Ili Ujenge Nidhamu Ya Fedha Kwenye Maisha Yako.
Safari ya kuelekea uhuru wa kifedha unahitaji kuwa na msingi wa nidhamu fedha; Je unataka kuwa na nidhamu ya fedha Ili uongeze kiwango cha kufanikiwa kwa maana ya mafanikio ya eneo la fedha. Sikiliza kisha fanyia kazi ambayo utapata kwenye episode hii utaona matokeo baada ya muda kwenye maisha yako.
2022-10-28
16 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Hatua Nne (04) Ambazo Maono Yako Yatapita Hadi Kukupa Mafanikio.
Maisha yako yapo ndani ya dakika tano ambazo unazo, swali la kujiuliza unaishi kwa maono au ilimradi tu unavuta pumzi? Maisha mahali popote yanaongozwa na maono hata mafanikio yako yanategemea sana maono yako. Unajua hatua ambazo maono yako itapitia kabla ya kukupa mafanikio basi hii ni episode muhimu sana kwako sikiliza mpaka mwisho.
2022-10-21
16 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Jinsi Ya Kuacha Tabia Ya Kuwahukumu Watu Wengine.
Tabia ya Kuwahukumu watu wengine ni tabia ya kiumaskini kwa sababu wewe siyo Mungu mpaka uwe unatoa hukumu kwa mabaya ya wengine, inaweza kuwa ni madhaifu, mapungufu, kasoro, makosa yao n.k lakini tambua kusikiliza episode hii utaweza Kuacha tabia ya hukumu watu wengine kwenye Maisha yako.
2022-10-04
21 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Sababu Saba (07) Za Kwanini Unaweza Kukabiliana Na Msongo Wa Mawazo Kwenye Maisha Yako. Part 02
Njia pekee ya kutatua tatizo ni kutafuta suluhu ya tatizo si ndiyo? Hata msongo wa mawazo ni lazima ujue namna gani unaweza kukabiliana ili uwe mtu mwenye furaha, kujiamini, afya nzuri ya akili na mwili. Episode hii itakupa maarifa na taarifa za kina ni kwa namna gani unaweza kukabiliana na msongo wa mawazo kwa kupitia uzoefu, takwimu na ushauri kutoka kwa watu wenye maarifa ya kutosha na wataalamu(Wanasaiokolojia); hutochoka sababu ina mifano mingi ipo, pia ina mtiririko ni Mzuri kuanzia sababu ya kwanza hadi ya saba na kuweza kuelewa si hivyo tu! Utapata kuburudika na kueleimika vya kutosha kwa...
2022-09-26
22 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Tambua Dalili Nane (08) Za Mtu Anayesumbuliwa Na Msongo Wa Mawazo Na Athari Zake. Part 01
Tafiti za shirika la American Psychology la Marekani inaonyesha mwaka 2020 zaidi ya watu milioni 190 wanasumbuliwa na msongo wa mawazo mkubwa sana duniani kote na zaidi ya watu milioni 284 wanasumbuliwa na hofu kubwa. Msongo wa mawazo unaiba furaha kwa kujua au kutokujua. Je unajua visababishi, dalili na athari za kuwa na msongo wa mawazo? Basi sikiliza episode hii upate kujifunza na kuwa balozi kwako na wengine kwenye kukabiliana na msongo wa mawazo.
2022-09-18
21 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Sababu Sita (06) Za Kwanini Unapaswa Kuacha Tabia Ya Kulalamika Kwenye Maisha Yao.
Je una tabia ya kulalamika kwenye maisha yako? Inawezekana unalalamikia wazazi, walezi, ndugu, marafiki, mpenzi, serikali, mfumo wa elimu, majirani zako n.k kuwa sababu ya wewe kuwa hapo. Lakini kumbuka hakuna faida ya wewe kulalamika kwa maana hiyo hii episode ni sahihi kwako na kuwa daraja kwa watu wenye tabia ya kulalamika kuacha na kuanza kuwajibika. Sikiliza na ujifunze...
2022-09-08
18 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Tumia Kanuni Ya 60/30/10 Kwenye Mgawanyo Wa Watu Kuambatana Nao.
Watu ambao unaambatana nao wana nafasi kubwa ya wewe kufanikiwa au kutofanikiwa. Je unajua kanuni ya 60/30/10 itakusiadia Kuambatana na watu wa faida? Majibu yote utapata kwa Kusikiliza episode hii. Usishau kushare link kwa marafiki wajifunze na subscribe kupitia app ya castbox, Apple podcast, audiomack, afripod, google podcast, spotify, anchor fm n.k.
2022-08-30
12 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Jinsi Ya Kujenga Ujasiri Wa Kuzungumza Mbele Ya Watu.
Ujuzi wa kungumza mbele ya watu ni muhimu sana kuwa nao pasipo kujali upo wapi na unafanya nini, Unajiuliza ni kwa namna gani si ndiyo eeh! Hebu jiulize hapo ulipo si umezungukwa na watu pia kitu unachofanya kinahusisha watu? Ikiwa jibu lako ni NDIYO! Basi hakikisha unasikiliza hii Podcast ili na ujuzi na ujasiri wa kuongea mbele ya watu.
2022-08-23
15 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Sababu Sita (06) Za Kwanini Unaweza Kujenga Uwezo Wa Kujiamini Kwa Kushinda Hofu/Uoga.
Unaweza Kujiamini kwa kiwango cha juu maishani ikiwa utasikiliza episode hii yenye dakika 15 za mabadiliko na kuweza kuwa mtu wa kujiamini, chukua hatua sasa.
2022-08-15
15 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Nguzo Sita (06) Za Ukweli Ambazo Zitabadili Maisha Yako..!
Ukweli ambao watu wengi hawapendi kusikia, Sikiliza ukweli ambao utabadili mtazamo wako pamoja na maisha yako; Sikiliza kisha ufanyie kazi ambayo umejifunza kwenye episode hii Kisha utaweza kuona unapiga hatua kwenye maisha yako.
2022-08-14
11 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Sababu Sita (06) Za Kwanini Unapaswa Kujipenda Pasipo Kujichukia.
Je unajipenda kwa kiwango gani? Lakini tambua kujipenda ni wajibu wako was asilimia 100% tofauti na hivyo tambua hujipendi.
2022-06-27
14 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Mambo Manne (04) Ya Kufanya Unapo Pitia Hali Ya Kukataliwa Kwenye Maisha Yako.
Moja ya changamoto iliyokatisha ndoto za watu wengi, ni ile ya kukataliwa ama kupingwa. Watu wengi wamekutana na hali hii, kuna ambao wameweza kuishinda, pia kuna ambao imekuwa kikwazo kwao. Jambo moja muhimu la kufahamu ni kwamba kukataliwa ni suala la kawaida, hata uwe bora kwa namna gani sio kila mtu atakubaliana wewe. Watu watakukataa kwa sababu zao wenyewe, wapo ambao watakukataa kwa sababu ya hofu yao juu yako, lakini pia kwa sababu kile ulichonacho wao hawana. Sasa unapokutana na hali hii hakuna haja ya kukata tamaa ama kupoteza muda wako kubishana nao. Kuna mambo muhimu unayopaswa kufanya; 1. Ongeza kujiamini. ...
2022-05-18
10 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Kanuni Tatu (03) Za Kuzingatia Ili Uwe Msomaji Mzuri Wa Vitabu
Je unataka kufaidika na usomaji wa vitabu? Basi Sikiliza episode hii ujifunze mambo muhimu ambayo yatafanya uwe msomaji mzuri zaidi wa vitabu na kupata matokeo chanya kwenye kusoma vitabu.Hakikisha una subscribe Castbox na Apple Podcast na turn on notifications Ili uwe kwanza kusikiliza.
2022-05-07
08 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Mambo Manne (04) Ya Kufanya Ili Kurudisha Hamasa Iliyopotea...!
Sikiliza episode hii ujue nini ufanye kurudisha hamasa iliyopotea na kuwa na morali ya kuendelea kupambania malengo, ndoto na maono yako.
2022-04-07
12 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Makosa Matano (05) Ambayo Unapaswa Kuepuka Ili Usipoteze Fedha Zako...!
Je umekuwa unapoteza fedha zako kirahisi? Umekuwa unataka kufanikiwa kwenye eneo la fedha lakini huoni hatua yoyote unapiga. Kupitia episode hii utaweza kujua makosa gani ambayo unapaswa kuepuka ili ufanikiwe kwenye eneo la fedha. Sikiliza episode hii kisha fanyia kazi ambayo utajifunza baada ya muda kupita utanipa ushuhuda kuwa hii episode imekupa matokeo chanya kwenye eneo la fedha
2022-03-26
14 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Siri Tatu (03) Za Kuzingatia Ili Uwe Mwekaji Mzuri Wa Akiba Ya Fedha Zako.
Kufanikiwa kwenye eneo la fedha inategemea sana na maarifa ambayo unayo juu ya fedha kwa maana hiyo ukiwa unataka kupiga hatua zaidi basi unapaswa kujenga tabia ya kuweka akiba ya fedha zako (Saving). Je unajua ufanye nini ili uweze kuweka akiba fedha zako? Basi Sikiliza episode hii upate kujua siri 3 ambazo zitakusaidia kujua namna gani uwe mwekaji mzuri wa akiba ya fedha zako
2022-03-19
08 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Sababu Saba (07) Za Kwanini Unapaswa Kujua Nguvu Ya Mabadiliko Kwenye Maisha Yako.
Je Unataka kubadili mfumo mzima wa maisha yako, mtazamo wako, aina ya marafiki, namna unavyofanya, mahusiano yako, biashara yako, Huduma yako n.k? Basi episode hii itakupa ufahamu wa nguvu wa mabadiliko kwenye maisha yako na kuweza kuchukua hatua Ili upate mabadiliko . Sikiliza mpaka mwisho upata kujua kwanini unaweza kupata mabadiliko kwenye eneo lolote ambalo upo
2022-03-10
16 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Mambo Matatu (03) Ambayo Hupaswi Kumshirikisha Kila Mtu Kwenye Maisha Yako
Muda mwengine unashindwa kupiga hatua kwenye maisha yako Kwa sababu ya kushirikiana watu baadhi ya mambo ambayo hayapaswi kabisa kuwashirikisha lakini kwa kuchukulia poa imekuwa inagharimu sana watu wengi, hivyo unapaswa kuwa makini kujua mambo gani unapaswa kutoshirikisha kabisa watu na mambo gani ambayo unaweza kushirikisha watu kwa maana hiyo maisha ni kuwa na kiasi kujua nini ufanye na nini usifanye kwahiyo Podcast hii itakusaidia kujua jinsi ya kuweza kuwa na kiasi/mipaka kwenye kushirikisha watu mambo yako, enjoy to listen podcast don’t forget to subscribe on Castbox and Apple podcast
2022-02-22
08 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Maswali Matano (05) Ambayo Yatakusaidia Kugundua Kusudi La Kuzaliwa Kwako.
Je unataka kujua kwanini umezaliwa? Kabla ya kujua umezaliwa kufanya nini basi tambua kuwa wewe hujazaliwa kwa bahati mbaya, hujazaliwa kwa bahati nasibu, hujazaliwa kwa miujiza, hujazaliwa kwa kuwa wazazi wako walitaka mtoto. Lakini tambua kwamba wewe umezaliwa kwa kusudi hivyo haupo duniani kwa bahati mbaya. Ili maisha yako yawe yenye maana ni kujua kusudi la kuzaliwa kwako. Sikiliza Episode hii itakupa majibu ya KWANINI umezaliwa na hatimaye kuongeza thamani ya maisha yako kwa kuliishi kusudi lako
2022-02-15
17 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Onyo! Hata Usifikirie Kushinda Tabia Ya Kughairisha Malengo Yako Mpaka usikilize Hii...
Sababu kuu tano (05) za kwanini unapaswa kushinda tabia ya kughairisha malengo yako kwenye maisha yako...! Sikiliza mpaka mwisho utajifunza mengi
2022-02-06
13 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Mambo Matano (05) Ya Kufanya Ili Uboreshe Mahusiano Yako
Je unajua jinsi ya kuboresha mahusiano yako yadumu kwa muda mrefu? Mahusiano ni zaidi ya kupendana kwa maana upendo hautoshi kufanya mahusiano yadumu, ni mahusiano mangapi yamevunjika japokuwa watu bado wanapendana? Ni kwa sababu ya kutojua namna gani wanaweza kuboresha mahusiano yako Basi Podcast hii Itakusaidia kujua namna gani unaweza kuboresha mahusiano yako na kuweza kudumu kwa muda mrefu. Subscribe kisha niandikie maoni yako umejifunza nini kwenye Podcast hii
2022-01-30
11 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Hatua Saba (07) Za Kuzingatia Wakati Unapanga Malengo Yako.
Je unataka kutimiza malengo yako kwa asilimia ngapi? Unajua kwamba kutimiza malengo yako inategemea sana namna ya kupanga malengo yako kwa bahati mbaya changamoto kubwa watu wengi hawajui namna gani wanapanga malengo vizuri na kwa ufanisi. Sikiliza Podcast hii mpaka mwisho utaweza kujua hatua saba za kuzingatia wakati unapanga maalengo yako, Kutimiza malengo ipo ndani ya uwezo wako ni wewe kujua hatua saba za kuzingatia wakati unapanga malengo yako. Usisahau ku- Subscribe kwenye Apple Podcast na kuweka Nyota 🌟 5.
2022-01-22
11 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Jinsi Ya Kubadili Mtazamo Hasi Na Kuwa Na Mtazamo Chanya.
Mtazamo Chanya ndio kila kitu maishani, bahati mbaya mtazamo hasi ndio hutawala akili zaidi kutokana na sababu mbalimbali kama vile jinsi unavyojitazama, sehemu ambazo unashinda, aina ya marafiki ambao unao, maneno ambayo unajiambia, tabi zako n.k. lakini Podcast hii itakusaidia mbinu sita rahisi za kuwa na mtazamo chanya kwenye maisha yako. Sikiliza Podcast hii kisha Subscribe kwenye platform ambayo unasikiliza.
2022-01-15
13 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Gundua Maajabu Ya Kutumia Kioo Kubadili Maisha Yako.
Je unajua kioo kinaweza kubadili maisha yako? Kioo ni zaidi ya kujitazama kwa maana kwamba Kioo kina faida na matumizi mengi zaidi unavyojitazama. Sikiliza episode hii mpaka mwisho ujue maajabu ya kutumia kioo.
2022-01-09
13 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Jinsi Ya Kupanga Bajeti Ya Fedha Zako Kupitia Kanuni Ya 40/30/10/10/10.
Hii ni kwa watu wanaotaka kujua Kupanga bajeti ya fedha zao kwa usahihi lakini hawajaanza bado, Sikiliza mpaka mwisho utaweza kupanga bajeti ya fedha zako na Kanuni ya 40/30/10/10/10 ambayo ni rahisi sana. Kazi kwako kusikiliza madini haya kisha fanyia kazi ili mwaka 2022 uwe mwaka wa kufanikiwa wewe kwenye eneo la fedha
2022-01-02
10 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Jinsi Ya Kutimiza Malengo Yako Ya Mwaka 2022 Kwa Kishindo...
Je unataka kutimiza malengo yako? Je unajua namna gani unaweza kutimiza malengo yako...? Usijali Sikiliza Podcast hii mpaka mwisho utaweza kujua ufanye nini Ili utimize malengo yako kwa kishindo mwaka 2022
2021-12-26
15 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Kanuni Mbili (02) Za Kupangilia Muda Wako Vizuri (Time Management.)
Muda ndio rasimali ya pekee ambayo haina mbadala, masaa 24 ambayo unayo unapaswa kuyatumia vizuri kwa kufanya mambo ya Muhimu na kuacha kufanya mambo yasiyo na umuhimu na ambayo yanakupotezea Muda wako, Hivyo kutumia Muda wako vizuri ni lazima ujue Kupangilia Muda wako vizuri kwa maana hiyo podcast hii ni Maalumu kwa ajili ya kukusaidia wewe kuwa na matumizi mazuri ya muda wako. Sikiliza Podcast hii mpaka mwisho pia subscribe channel hii Ili Uwe wa kwanza kupata Podcast mpya kila wiki
2021-12-19
11 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Mambo Sita (06) Ambayo Unapaswa Kufanya Ili Upate Kibali Machoni Pa Watu.
Nguvu ya Kibali imebeba Mafanikio yako na mtaji wa mtu ni watu, ili watu wewe mtaji wako ni lazima uwe na nguvu ya Kibali Ili uweze kukubalika zaidi; Sikiliza episode hii mpaka mwisho baada ya kusikiliza utagundua jinsi gani ulikuwa unakosea na kushindwa kupata Kibali kwa watu. Karibu sana kusiliza episode kwenye channel hii ya “Maisha Ni Kuthubutu”
2021-12-12
14 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Usikate Tamaa Kama Kweli Unataka Kupiga Hatua Kwenye Maisha Yako.
Usikate tamaa sababu umezaliwa kufaniwa kwa maana hiyo Sikiliza episode hii mpaka mwisho itakupa nguvu ya kupambania malengo yako na ndoto zako pasipo kukata tamaa na kuweza kusonga mbele kwenye maisha yako
2021-12-05
10 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Makosa Matano (05) Ambayo Unafanya Na Kupelekea Kupoteza Fedha Zako.
Kufanikiwa kwenye eneo la fedha unahitaji sana kuwa na maarifa sahihi juu ya fedha, kupitia podcast hii kuwa na uhakika utaweza kusahihisha makosa haya ambayo hupelekea kupoteza fedha zako ikiwa tu utaweka utekelezaji kwenye maarifa haya kazi kupitia Podcast hii na kuweza kupiga hatua kwenye eneo la fedha
2021-11-28
15 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Mambo Sita (06) Ya Kufanya Ili Uwe Msomaji Mzuri Wa Vitabu
Kusoma vitabu ni tabia, maarifa ni nguzo ya mafanikio kwenye maisha yako kama utafanyia kazi kwa maarifa ambayo unajifunza; maarifa mengi yapo kwenye vitabu kwa maana hiyo kupitia episode hii utaenda kuwa msomaji mzuri wa vitabu.
2021-11-21
14 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Lugha Tano (05) Za Upendo Kwenye Mahusiano (The 5 Language Of Love)
Mahusiano yanajengwa na mawasiliano, bahati mbaya mahusiano mengi wana wasiliana kwa namna ambayo sio sahihi kwa sababu kila mtu mtu kwenye mahusiano ana lugha yake ya upendo ambayo akionyeshwa lugha hiyo anaona anapendwa, anathaminiwa na kujaliwa kwa maana hiyo ni vema sana kujua lugha ya upendo ya mpenzi wako, mchumba wako, mume wako au mke wake na uweze kuwasiliana nae kupitia lugha ya upendo ambayo unayo na kuweza kudumisha mahusiano yako/yenu. Sikiliza mpaka mwisho wa episode hii ujifunze na kuongeza maarifa kuhusu mahusiano. Usisahau subscribe na kuandika maoni yako.
2021-11-14
12 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Jinsi Ya Kugundua Kusudi La Kuzaliwa Kwako.
Utajiri mkubwa haupo kwenye machimbo ya almasi na dhahabu, utajiri mkubwa upo makaburini kwa maana hiyo usikubali kufa na kusudi ndani yako na nafasi pekee ya kuanza kuliishi na kutimiza kusudi lako ni sasa; kupitia episode hii utaweza kugundua kusudi la kuzaliwa kwako hapa duniani na unapaswa kufanya nini (Your Purpose). Sikiliza episode hii mpaka Mwisho pia usisahau ku-subscribe na kuandika comment yako hapo chini✍🏾
2021-11-06
12 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Jinsi Ya Kujitofautisha Na Watu Wengine Bila Kupoteza Uhalisia Wako
Wewe umezaliwa na upekee ndani yako na upekee wako ndio utambulisho wako kwa maana hiyo wewe ni wa kitofauti sana hivyo anza kuishi uhalisia wa maisha yako Ili uweze kujitofautisha na watu wengine kwenye maeneo tofauti tofauti ambayo upo kwa sababu ndani yako umebeba kusudi maalumu ambalo halifanani na mtu yeyote hapa duniani
2021-10-25
11 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Aina Tano (05) Za Nguvu Zinaleta Mafanikio Kwenye Maisha Yako...
Je unajua umebeba nguvu na uwezo mkubwa ndani yako? Lakini kwa bahati mbaya unatumia sehemu ndogo ya uwezo wako na kupelekea kushindwa kufanikiwa kwa kiwango cha juu kwenye malengo yako, maono yako, ndoto zako n.k kwa maana hiyo unahitaji sana kujenga nguvu hizi Ili uweze kupiga hatua kwenye maisha yako na kufanikiwa kwa sababu Unastahili kufanikiwa na Inawezekana. Usisiahau kuniandikia maoni yako hapo chini kisha subscribe channel hii kwenye Apple Podcast na platform zengine. kauli mbiu: “Maisha Ni Kuthubutu”
2021-10-14
24 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Jitambue Wewe Ni Nani?
Elimu ya kujitambua haifundishwi shuleni na vyuo vikuu na kupeleka watu wengi kujitambua kwa kiwango kidogo, ili uishi Maisha yenye furaha msingi wa kwanza ni kujitambua wewe ni nani kwa maana hiyo episode hii inakupa uwezo wa kujitambua kwa kiwango cha juu baada ya kusikiliza mpaka mwisho episode hii...! Usisahau ku subscribe kwenye Apple Podcast pia niandike maoni yako muhimu sana ✍🏾. Kauli Mbiu: “ Maisha Ni Kuthubutu”
2021-10-02
17 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Mambo Matano (05) Ya Kufanya Ili Uweze Kutimiza Malengo Yako
Hii ni kwa watu wanaotaka kutimiza malengo yao pasipo kujali umeanza au bado hujaanza, unaweza kutimiza malengo yako ukijua sifa za malengo sahihi na kujua siri muhimu za kutambua Ili uweze kutimiza malengo yako; kinachohitajika ni uteyari wako pamoja na uthubutu wa kufanyia kazi ambayo utajifunza kupitia episode hii. Usisahau ku subscribe na kuanndika comment yako umejifunza nini kupitia episode hii. Kauli Mbiu: “MAISHA NI KUTHUBUTU”
2021-09-22
16 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Mambo Matano (05) Ya Kufanya Ili Uweze Kutimiza Malengo Yako
Hii ni kwa watu wanaotaka kutimiza malengo yao pasipo kujali umeanza au bado hujaanza, unaweza kutimiza malengo yako ukijua sifa za malengo sahihi na kujua siri muhimu za kutambua Ili uweze kutimiza malengo yako; kinachohitajika ni uteyari wako pamoja na uthubutu wa kufanyia kazi ambayo utajifunza kupitia episode hii. Usisahau ku subscribe na kuanndika comment yako umejifunza nini kupitia episode hii. Kauli Mbiu: “MAISHA NI KUTHUBUTU”
2021-09-21
00 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Sababu Tano (05) Za Kwanini Za Kwanini Unapaswa Kuepuka Majuto Kwenye Maisha Yako
Je unajua kwamba majuto ni adui wa maisha yako? Ndio adui ni adui mkubwa sana furaha yako, mahusiano yako, malengo yako, ndoto zako n.k hivyo ukichelewa kuchukua hatua kuyaepuka majuto kwenye maisha yako tegemea kupata msongo mkubwa wa mawazo (stress) na kutopiga hatua sababu majuto mara zote hupoteza hamasa pamoja na kutokuwa mwenye ufanisi kwenye kitu unachofanya hivyo njia sahihi ya kuepuka na kuyashinda majuto ni kusikiliza episode hii mpaka mwisho. Usisahau ku Subscribe na kuandikia maoni yako✍🏾
2021-09-15
10 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
TABIA TANO (05) ZA KUEPUKA ILI UFANIKIWE KWENYE MAISHA YAKO
Kiwango cha mafanikio yako inategemea sana na muenendo wa tabia zako za kila siku, tabia ina nafasi kubwa ya kufanya ufanikiwe au usifanikiwe kwenye maisha yako hivyo unahitaji maarifa haya ambayo yatakusaidia kuepuka tabia zuizi ili ufanikiwe kutimiza malengo yako, ndoto zako pamoja na maono yako. Kumbuka unastahili kufanikiwa ndio maana umezaliwa......! Sikiliza mpaka mwisho podcast hii Usisahau kuniandikia maoni yako na subscribe ili uwe wa kwanza kupata Episode mpya kwenye channel hii.
2021-09-05
15 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Sifa Sita (06) Za Mtu Anayetaka Mafanikio.
Kiwango cha mafanikio kinategemea sana kiwango chako cha kujitambua, unatamani kufanikiwa kwenye kitu unachofanya lakini hujui nini ufanye Ili ufanikiwe kwenye kitu unachofanya kwa maana kutimiza malengo yako, ndoto zako pamoja na maono yako; Lakini tafiti zimefanyika kuna sifa sita ambazo mtu akizijenga anavuta mafanikio kwenye maisha yake, kupitia podcast jiandaee kuwa mtu mwenye mafanikio makubwa baada ya kusikiliza Podcast hii mpaka mwisho na kujua sifa ambazo mtu anataka mafanikio anapaswa kuwa nazo. Kauli Mbiu: “MAISHA NI KUTHUBUTU”
2021-08-07
20 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Mambo Matano (05) Ya Kufanya Ili Uongeze Uwezo Wa Kujiamini
Hofu na uoga imekuwa kizuizi cha kushindwa kutimiza malengo yako pamoja na ndoto zako? Kupitia Podcast hii utakuwa mtu mwenye kujiamini kwa kujua nini ufanye ili uweze kushinda na Kutawala hofu na uoga kwenye maisha yako; kujiamini ni matokeo ya kushinda hofu na uoga ili upate matokeo makubwa hakikisha unafanyia kazi uliyojifunza kupitia Podcast hii na uanze kuwa mtu mwenye kujiamini inawezekana sana kutimiza malengo yako, ndoto zako pamoja na maono yako. kauli Mbiu: “MAISHA NI KUTHUBUTU”
2021-07-31
13 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Mambo Matano (05) Ya Kufanya Kabla Ya Kutumia Fedha Yako
Elimu ya fedha haifundishwi shuleni na vyuo vikuu na kupeleka watu wengi kupoteza fedha zao kirahisi kwa sababu ya kukosa maarifa sahihi ya fedha; Leo nimekuandalia mambo matano ya kufanya kabla ya kutumia fedha au pesa yako Ili uweze kufanikiwa kwenye eneo la fedha kwa kupata maarifa sahihi ambayo shuleni wala vyuo vikuu hukufundishwa. Kauli Mbiu: “MAISHA NI KUTHUBUTU”
2021-07-22
20 min
Maisha Ni Kuthubutu Podcast
Mambo (07) Ya Kuzingatia Ili Uongeze Thamani Ya Maisha Yako Leo.
Jifunze kupitia Lolo Facts Podcast kila wiki podcast za maisha na maendeleo binafsi
2021-06-18
15 min