Look for any podcast host, guest or anyone
Showing episodes and shows of

Jeremiah Paul Wandili

Shows

SAUTI-SIKIKASAUTI-SIKIKASauti Ya Matumaini-Amos Mwijonge.Usipofuta kibao, huwezi jua kwanini gari la taka linaoshwa hili liweze kubeba taka tena. Maana cha muhimu kwetu sio miaka uliyoishi katika maisha yako, cha muhimu kwetu ni thamani ya maisha yako katika miaka uliyoishi. Kumbuka mito hainywi maji yake na miti haili matunda ya mti wake. Sikiliza sauti ya Amosi.... kumbuka hautakumbukwa kwa ulichojifunza, utakumbukwa kwa ulichofundisa wengine duniani. Fuatilia kazi nzuri za Amosi hapa Maisha ni mchezo wa kupona...... 2020-06-1204 minSAUTI-SIKIKASAUTI-SIKIKASauti Ya Dr Mipango-Waziri wa Fedha na Mipango, TanzaniaMh, Waziri Dr. Phillip Mipango, anasikika moja kwa moja kutoka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akipaza sauti kulelezea Mpango wa Maendeleo wa Mwaka 2020/21 na hali ya Uchumi wakatika wa Bunge la Bajeti Tarehe 11/06/2020. Je, unajua sekta zenye kuwekewa kipaumbele kwa Mwaka 2020/21 na je, unajua #Covid19 imetikisa Uchumi... sikiliza upate kujua mpango wa Serikali katika kuimarisha Afya, Miundombinu, Elimu na Maendeleo kwa ujumla. 2020-06-1159 minSAUTI-SIKIKASAUTI-SIKIKASauti Ya Joel Nanauka-Lijue Kusudi LakoKila siku unapo amka unapaswa kujiuliza maswali haya; Je, ni maswali gani na kuna sauti gani katika kujiuliza maswali hayo ili uweze kujua kusudi lako. Fuatilia Dakika 3 katika mfululizo wa Sauti Sikika, isikilize Sauti ya Joel Nanauka. Pia unaweza kumfuatilia Joel katika Mitandao ya Kijamii, Instagram; https://www.instagram.com/joelnanauka_/ na Facebook; https://web.facebook.com/jnanauka/ pia katika Channel yake ya Youtube; https://bit.ly/Joel-Nanauka-Youtube  2020-06-1003 minSAUTI-SIKIKASAUTI-SIKIKASauti Ya Theresia- Sauti yake akizungumzia Mabadiliko Chanya wakati wa Covid-19.Theresia anasimulia namna ambavyo Covid19 imekuwa ni changamoto chanya kwake. Maana Theresia amechukulia covid19 katika uhalisia wake zaidi yeye alijiepusha kuishi kwa hofu. Anasisitiza umuhimu wa kuchukua tahadhali na kufuata maelekezo ya wataalamu wa Afya. Amezungumza mengi, ikiwemo swala zima la kujenga mahusiano mazuri na familia, kutumia muda mzuri pia kujiendeleza. Hongera sana Theresia kwa Sauti yako katika Mabadiliko Chanya. Kumbuka unaweza kushare Sauti yako kwa namba +255758044443. 2020-06-0920 minSAUTI-SIKIKASAUTI-SIKIKASauti Ya MabadilikoUnajua, mabadiliko ni mchakato, ni hatua.. lakini je unajua Mabadiliko ni gharama? na ili kufikia mabadiliko lazima ulipe gharama. Podcast hii inakupa nafasi ya kufahamu sauti ya mabadiliko ili uweze kujiandaa kuisikiliza na kulipa gharama katika kufikia mabadiliko. Ahsante sana, karibu. Tuma maoni yako na sauti yako ya Mabadiliko katika namba hii ilisajiliwa Whats App +255758044443 nasi tutashare podcast yako. Ahsante sana, furahi sauti ya mabadiliko.  2020-06-0925 minSAUTI-SIKIKASAUTI-SIKIKASauti Ya Sheila-Changamoto za Kutafuta Ajira kipindi cha #Covid-19Unajua changamoto wanazopitia wasichana katika kutafuta Kazi pindi tu wakiwa wametoka Chuo? Aiseee ni kisanga, msikilize Sheila hapa akipaza Sauti katika Mtaa huu #Sauti-Sikika hautojutia mazee..... 2020-06-0814 minSAUTI-SIKIKASAUTI-SIKIKASauti Ya Husna-Sikiliza Sauti ya MudaKatika mfululizo wa kukusanya SAUTI-SIKIKA, tunaisikiliza Sauti ya Husna, akituelezea umuhimu wa kuisikiliza sauti iliyo ndani ya Muda. Je wajua Muda una-ongea, na je, wajua Muda una Sauti. Karibu kusikiliza..... Uache Muda uongee! 2020-06-0702 minSAUTI-SIKIKASAUTI-SIKIKASauti Ya Balozi Angelo-Vijana na UKIMWIBalozi anasema, UKIMWI-Umekaa kimya, lakini upo... anawaomba Wazazi, walezi, mashirika yasiyo ya kiserikali kuchukua hatua za kuwapa Vijana Fursa hili SAUTI ZAO zisikike katika Mapambano dhidi ya UKIMWI. Msikilize Balozi katika leo; SAUTI-SIKIKA. 2020-06-0704 minSAUTI-SIKIKASAUTI-SIKIKASikiliza Sauti Ya Ndani-Sauti Ya SophieRafiki, karibu katika mfululizo wa Sauti Sikika. Msikilize Mgeni Sophie akizungumza nawe. Ni kweli watu wengi wanatamani kujua namna wanavyoweza kuisikiliza na kuitii sauti yao ya ndani. Sasa utawezaje kujua ni wakati sahihi kwa Sauti ya Ndani kusikika. Sikiliza Sauti ya Sophie akikuelezea namna anavyofanya kuisikiliza sauti yake ya ndani. Ahsante sana. 2020-06-0702 minSAUTI-SIKIKASAUTI-SIKIKAKaribu-Sauti SikikaNi muhimu sana kutambua Sauti iliyo ndani yako. Kazi kubwa ni kuhakikisha unatoa nafasi ya kuamini na kuisikiliza Sauti iliyo ndani yako. 2020-06-0703 min