podcast
details
.com
Print
Share
Look for any podcast host, guest or anyone
Search
Showing episodes and shows of
John Waicua
Shows
Chimbuko la Tamaduni - Maasai
EPISODE 12 | CHIMBUKO LA TAMADUNI – MABADILIKO KATIKA TAMADUNI YA MAA – PODCAST
Katika Maisha, uwezo wa kustahimili mabadiliko kadri muda unavyosonga ni moja ya vipengee ambavyo huashiria udhibiti na ukomavu. Mila na tamaduni ya Kimaasai, ni mojawapo ya tamaduni zilizoweza kustahimili mabadiliko kwa miaka na mikaka na kusalia imara hadi katika ulimwengu wa sasa. Hata hivyo kuna baadhi ya mambo ambayo yalishindwa kustahimili joto la mabadiliko, na...
2023-03-23
10 min
Chimbuko la Tamaduni - Maasai
EPISODE 11 | CHIMBUKO LA TAMADUNI – TAMADUNI YA KUWEKA FIMBO AU MKUKI NJE YA BOMA – PODCAST
Kutokana na hali ya jamii hii ya Maa kuegemea sana taasubi za kiume, kulikuwa na njia maalum ya kutangaza uwepo wa mwanume katika boma Fulani. Wanaume walitumia fimbo au mikuki hasa kwa vijana wa Morani, kuashiria uwepo wao katika boma, ili kumjulisha mwanaume mwingine kwamba kuna mwanaume mwingine kabla hajafika mlangoni. Katika tamaduni ya kimaasai,...
2023-03-02
10 min
Chimbuko la Tamaduni - Maasai
EPISODE 10 | CHIMBUKO LA TAMADUNI – MCHAKATO WA KUPATA MKE KATIKA JAMII YA MAA – PODCAST
Baadhi ya wanaume waliochukuliwa kama mashujaa walikua na nafasi rahisi kwani wazazi wengine waliwaleta wana wao ili waolewe na shujaa huyu. Wazazi wengine pia walijishughulisha kwa kiwango kikubwa katika kuwatafutia wana wao wake.
2023-02-23
10 min
Chimbuko la Tamaduni - Maasai
EPISODE 9 | CHIMBUKO LA TAMADUNI – MAISHA YA MORANI WA KIMAASAI – PODCAST
Morans hurejelea vijana ambao wamepitia desturi ya kutoka ujana hadi utu uzima. Hii ni hatua muhimu katika utamaduni wa Wamasai.
2023-02-22
09 min
Chimbuko la Tamaduni - Maasai
EPISODE 8 | CHIMBUKO LA TAMADUNI – SHEREHE YA KUPASHWA TOHARA (PART 2) – PODCAST
Katika jamii ya kimaasai, hafla yoyote iliyoashiria mwanzo mpya, iliandamana na shughuli za kunyoa nywele na kubadili mavazi, ishara kamili kwamba mmoja amekubali kuyaacha yale ya zamani na kukumbatia Maisha mapya.
2023-01-11
12 min
Chimbuko la Tamaduni - Maasai
EPISODE 7 | CHIMBUKO LA TAMADUNI – SHEREHE YA KUPASHWA TOHARA (PART 1) – PODCAST
Baadhi ya mambo mengine ambayo vijana hawa walipaswa kutekeleza, yalitokana na mafunzo waliyopokea au kwa kutazama yale wazee na wanaume wengine katika jamii hii walikua wakitenda.
2023-01-11
09 min
Chimbuko la Tamaduni - Maasai
EPISODE 6 | CHIMBUKO LA TAMADUNI – MALEZI YA WANA KATIKA JAMII YA MAA – PODCAST
Jukumu la malezi ya Watoto katika tamaduni na jamii ya kimaasai, lilikua jukumu la wanajamii wote, kuanzia kwa wazazi wa mtoto, jamaa wa karibu, Watoto wenzake na hata jamii nzima kwa ujumla.
2023-01-11
10 min
Chimbuko la Tamaduni - Maasai
EPISODE 5 | CHIMBUKO LA TAMADUNI – MFUMO WA MAJINA KATIKA JAMII YA MAA – PODCAST
Katika siku ya kupewa jina kwa mtoto, familia ya mtoto ilitafuta msimamizi wa mwana wao, aliyekuwa wa jinsia moja na mtoto mwenyewe aliyefaa kutoka katika familia au ukoo tofauti na mtoto mwenyewe. Msimamizi huyu alifaa kuwa mtu mwenye maadili mema na aliyekuwa wa kupigiwa mfano na wanajamii wenzake, na ndiye alitekeleza jukumu hili katika hafla iliyojumuisha pia kumchinja kondoo.
2023-01-11
13 min
Chimbuko la Tamaduni - Maasai
EPISODE 4 | CHIMBUKO LA TAMADUNI – HESHIMA YA MAMA MJAMZITO KATIKA JAMII YA MAA – PODCAST
Ili kuwa na kizazi cha siku za usoni, Watoto huwa kiungo muhimu katika kila jamii. Katika jamii ya kimaasai, Watoto walianza kulindwa wakiwa katika tumbo la mama, na hivyo kina mama wajawazito waliangaziwa kwa njia tofauti wakilinganishwa na wanajamii wengine. Baada ya kujifungua, jamii ya wamaasai ilikua na njia ya kipekee ya kuwakaribisha Watoto katika...
2022-10-27
08 min
Chimbuko la Tamaduni - Maasai
EPISODE 3 | CHIMBUKO LA TAMADUNI – NAFASI YA WANAWAKE KATIKA JAMII YA MAA – PODCAST
Uwezo wa wanawake katika jamii hii, ulidunishwa sana, kwani jamii ya wamaasai iliwainua wanaume zaidi na hivyo kuwaona wanawake kama wasio na uwezo wa kuwa viongozi
2022-10-13
08 min
Chimbuko la Tamaduni - Maasai
EPISODE 2 | CHIMBUKO LA TAMADUNI – PODCAST
Chanzo cha kila jamii kote ulimwenguni huwa Familia. Ni kutokana na familia ndipo tunapata jamii na hata taifa. Katika awamu ya leo, tunaangazia muundo wa familia ya Kimaasai
2022-10-06
09 min
Chimbuko la Tamaduni - Maasai
EPISODE 1 | CHIMBUKO LA TAMADUNI – PODCAST
Sikiliza makala haya ili upate kuelewa bayana kuhusu Chimbuko la Jamii ya Maasai na jinsi walifika katika taifa la Kenya na maeneo mengine wanakopatikana.
2022-09-23
09 min