podcast
details
.com
Print
Share
Look for any podcast host, guest or anyone
Search
Showing episodes and shows of
Kocha Dr Makirita Amani
Shows
Ongea Na Kocha.
Ongea Na Kocha; Sell Like Crazy, Basil Danghalo.
Habari Mwanamafanikio?Karibu kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA ambapo kuna mambo mawili makubwa.Jambo la kwanza ni mjadala wa pamoja wa kitabu cha SELL LIKE CRAZY. Hiki ni kitabu kilichoandikwa na Sabry Subi ambacho kinatupa maarifa ya kuweza kujenga mfumo wa masoko na mauzo ambao unatuwezesha kuleta wateja wengi kwenye biashara na kufanya mauzo makubwa kuliko tulivyozoea. Haya ni maarifa muhimu sana kwa ukuaji wa biashara zetu. Kwenye mjadala huu wa kitabu, wanamafanikio mbalimbali wameshirikisha yale waliyojifunza kwenye kitabu na uzoefu wao katika kufanyia kazi mambo hayo. Sikiliza kipindi kujifunza zaidi.Jambo la...
2022-05-23
3h 06
Ongea Na Kocha.
Ongea Na Kocha; Exactly What To Say, Mrejesho Wa Tathmini Ya Robo Mwaka Na Lengo Jipya La Namba Ya Mauzo.
Habari mwanamafanikio?Karibu kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA ambacho kina mambo matatu makubwa.Jambo la kwanza ni mjadala wa kitabu cha EXACTLY WHAT TO SAY, kitabu chenye maneno 23 ya ushawishi ambayo ukiyatumia unakuwa na ushawishi mkubwa kwa wengine. Wanamafanikio wameshirikisha kwa mifano kuhusu maneno hayo. Sikiliza kipindi hiki kujifunza kutoka kwenye uzoefu wa wengine.Jambo la pili ni mrejesho wa tathmini ya robo mwaka ya pili kwenye mwaka wetu wa mafanikio 2021/2022. Kwa ujumla bado watu wanapata changamoto kuripoti sehemu kubwa ya namba zinazopimwa kwenye tathmini. Tutaendelea kueleweshana hatua kwa hatua ili kuweza kuzielewa...
2022-05-16
2h 51
Ongea Na Kocha.
Ongea Na Kocha; How To Live On 24 Hours A Day Na Mwongozo Wa Kufanya Tathmini Ya Robo Mwaka.
Habari Mwanamafanikio?Karibu kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA ambacho kina mambo mawili makubwa.Jambo la kwanza ni mjadala wa kitabu cha HOW TO LIVE ON 24 HOURS A DAY kilichoandikwa na Arnold Bennett. Kitabu hiki kifupi ambacho kimeandikwa zaidi ya miaka 100 iliyopita kina mengi ya kutufundisha kuhusu matumizi sahihi ya muda na jinsi ya kuishi vyema. Kwenye kipindi tumekuwa na mjadala wa kitabu ambapo wanamafanikio wameshirikisha yale waliyojifunza kwenye kitabu hicho.Jambo la pili ni mwongozo wa kufanya tathmini ya robo mwaka. Tunamaliza robo mwaka ya pili kwenye mwaka wa mafanikio 2021/2022. Ni wakati wa...
2022-04-25
3h 08
Ongea Na Kocha.
MWONGO WA KUFIKIA UBILIONEA (2020 – 2030).
MWONGO WA KUFIKIA UBILIONEA (2020 - 2030).Muongo wa 2020 - 2030 ni muongo wa kufikia kiwango cha utajiri cha UBILIONEA kwenye KISIMA CHA MAARIFA.Hiki ni kipindi ambacho kila mwanachama anapaswa kufikia uhuru wa kifedha kwenye maisha yake.Ni kupitia uhuru huo wa kifedha ndipo kila mwanachama anaweza kuwa huru na maisha yake.Katika kujenga uhuru huu wa kifedha na kufikia ubilionea, njia kubwa tatu zinatumika.👉Njia ya kwanza ni biashara.Kila mwanachama anajenga biashara zinazojiendesha zenyewe bila ya kutegemea uwepo wake moja kwa moja.Biashara ndiyo njia kuu ya...
2022-04-11
1h 11
Ongea Na Kocha.
Ongea Na Kocha; Kuongeza Kiwango Cha Faida, Mwongozo Wa Kufika Kwenye Ubilionea.
Habari mwanamafanikio?Karibu kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA ambacho kina mambo mawili makubwa.Jambo la kwanza ni mjadala wa sehemu ya mwisho ya kitabu cha INSTANT CASHFLOW inayohusu kuongeza kiwango cha faida. Wanamafanikio wameshirikisha njia tano walizochagua kufanyia kazi kwenye biashara zao ili kuweza kuongeza kiwango cha faida. Ni njia nzuri na zinazowezekana kwa kila aina ya biashara.Jambo la pili ni MWONGOZO WA KUFIKIA UBILIONEA. Nimeshirikisha mwongozo kamili tunaokwenda kufanyia kazi kwenye huu muongo (2020 – 2030) ili kila mmoja wetu aweze kufikia ubilionea na uhuru wa kifedha. Mkakati una hatua za kupiga kwenye kila mw...
2022-04-11
3h 04
Ongea Na Kocha.
ONGEA NA KOCHA; HELL YEAH, BOSCO MLOMO.
Habari Mwanamafanikio?Karibu kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA ambapo kuna mambo matatu makubwa.Jambo la kwanza ni uchambuzi wa kitabu cha HELL YEAH OR NO kilichoandikwa na Derek Sivers. Kwenye kitabu hiki mwandishi ametushirikisha falsafa yake fupi ya kuchagua nini afanye. Anatuambia kama kitu hukipi NDIYO kubwa basi unapaswa kukipa HAPANA. Ni kitabu kifupi, chenye mambo ya kawaida ila yenye nguvu kubwa sana kwenye safari yetu ya mafanikio.Jambo la pili ni mahojiano na mwanamafanikio mwenzetu Bosco Mlomo ambaye anatushirikisha safari yake ya kibiashara. Bosco anatushirikisha alivyoanza kama msaidizi kwenye duka la vifaa...
2022-03-28
3h 02
Ongea Na Kocha.
Ongea Na Kocha; Instant Cashflow – Kuongeza Idadi Na Kiwango Cha Manunuzi.
Habari Mwanamafanikio?Karibu kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA ambapo tumeendelea na uchambuzi wa kitabu cha INSTANT CASHFLOW kilichoandikwa na Bradley Sugars.Kitabu hiki ni mwendelezo wa msingi mkuu tuliojifunza kwenye kitabu cha BILLIONAIRE IN TRAINING cha mwandishi huyo huyo.Kwenye BILLIONAIRE IN TRAINING tulijifunza ngazi tano za ujasiriamali ambazo ni kama ifuatavyo;Ngazi sifuri; mwajiriwa, hapa chanzo cha kipato ni ajira tu.Ngazi ya kwanza; kujiajiri, hapa unafanya kila kitu mwenyewe.Ngazi ya pili; meneja, hapa umeajiri wengine kukusaidia, ila bila uwepo wako hakuna kinachoenda....
2022-03-21
3h 07
Ongea Na Kocha.
Ongea Na Kocha; Kisima, Tathmini, Rejoyce Otaru.
ONGEA NA KOCHA; KISIMA, TATHMINI, REJOYCE OTARU.Karibu mwanamafanikio kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA ambacho kina mambo makubwa manne ya kujifunza kwenye safari yetu ya mafanikio.Jambo la kwanza ni mambo ya muhimu na ya msingi ya kuzingatia kwenye KISIMA CHA MAARIFA. Kwa sasa tunapotia mageuzi makubwa kwenye KISIMA kutoka kuwa kundi la kujifunza na kwenda kuwa jumuia za wanamafanikio. Katika mageuzi haya KISIMA kinataka kila mmoja kujitoa zaidi ili kuweza kufanikisha lengo la pamoja ambalo wote tunalo. Nimeshirikisha dhana nzima ya KISIMA CHA MAARIFA NI JESHI, adui yetu mkuu tunayemkabili na ushindi ambao tunataka...
2022-03-14
3h 19
Ongea Na Kocha.
ONGEA NA KOCHA; Instant Cashflow Sehemu Ya Pili.
Habari Mwanamafanikio?Karibu kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA ambapo tunapata uchambuzi wa kitabu cha INSTANT CASHFLOW sehemu ya pili.Kwenye sehemu hii ya pili tunaangalia maeneo mawili kati ya matano ya kukuza biashara.Eneo la kwanza ni kutengeneza wateja tarajiwa kupitia masoko. Hapa tunaziangalia njia mbalimbali za masoko unazoweza kutumia kwenye biashara yako na ukawafikia wateja wengi wapya. Masoko ni sehemu muhimu sana ya biashara, isipofanyiwa kazi vizuri na kwa uhakika, biashara haiwezi kufanikiwa.Eneo la tatu ni kuwageuza wateja tarajiwa kuwa wateja kamili. Unaweza kuwafikia wateja kwa njia za masoko...
2022-02-28
3h 06
Ongea Na Kocha.
ONGEA NA KOCHA; Tathmini Ya Robo Mwaka, Kigawe Kikuu Cha Mafanikio, Instant Cashflow.
Karibu kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA ambacho kina mambo yafuatayo.Moja ni mrejesho wa tathmini za robo mwaka ya kwanza kwenye mwaka wa mafanikio 2021/2022. Nimeshirikisha yale muhimu kutoka kwenye tathmini hizo na namna ya kujiandaa vyema kwa tathmini ijayo.Mbili ni andiko la KIGAWE KIKUU CHA MAFANIKIO (THE COMMON DENOMINATOR OF SUCCESS) ambalo linaelezea siri kuu ya mafanikio ambayo wote waliofanikiwa wameijua na kuifanyia kazi. Siri hiyo ni watu waliofanikiwa wamejijengea tabia ya kufanya vitu ambavyo walioshindwa hawapendi kuvifanya. Utajifunza kwa kina kutoka kwenye andiko hilo.Tatu ni uchambuzi wa kitabu cha INSTANT...
2022-02-21
3h 05
Ongea Na Kocha.
ONGEA NA KOCHA; Miminalist Entrepreneur, Tathmini Ya Robo Mwaka, Changamoto Ya Siku 100.
Habari mwanamafanikio?Karibu kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA ambapo kuna mambo makubwa matatu.Moja ni uchambuzi wa kitabu kinachoitwa MINIMALIST ENTREPRENEUR kilichoandikwa na Sahil Lavingia.Hiki ni kitabu ambacho Sahil ameshirikisha safari yake ya kujenga biashara kwa kuzingatia yale ya msingi badala ya kuhangaika na sifa zisizo na tija.Kwenye kipindi hiki tumejadili mambo nane ya msingi ambayo Sahil ameshirikisha kwenye kitabu kama ifuatavyo;1. Msingi mkuu wa kuzingatia kwenye biashara ni THAMANI na FAIDA. Toa thamani kwa wateja na hakikisha biashara inaingiza faida.2. Anza na jumuia uliyopo. Waangalie wa...
2022-02-07
3h 08
Ongea Na Kocha.
Ongea Na Kocha; Mjadala Wa Kitabu Billionaire In Training.
Habari Mwanamafanikio?Kwenye KISIMA CHA MAARIFA, tupo kwenye muongo (2020 - 2030) wa kufanya makubwa.Katika muongo huu kila mmoja wetu anapambana kufikia uhuru wa kifedha, ambapo ni kuweza kuwa na njia za kuingiza kipato kisichotegemea uwepo wa moja kwa moja (passive income) pamoja na kuwa na uwekezaji mkubwa unaokua thamani na kuzalisha faida inayoweza kukidhi gharama za kuendesha maisha.Katika kufanyia kazi lengo hilo, tuna kitabu ambacho ndiyo mwongozo wetu kwa kipindi hiki chote. Kitabu hicho ni BILLIONAIRE IN TRAINING ambacho kimeandikwa na Bradley Sugars.Kitabu hiki kimeelezea njia tatu za kufika kwenye...
2022-01-31
3h 40
Ongea Na Kocha.
Ongea Na Kocha; Billionaire In Training, Helanane Ilomo.
Habari Mwanamafanikio?Karibu kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA ambapo kuna mambo makubwa mawili.Jambo la kwanza ni uchambuzi wa kitabu cha BILLIONAIRE IN TRAINING. Hiki ni kitabu muhimu sana kwenye safari yetu ya kuelekea kwenye uhuru wa kifedha. Na ndiyo kitabu kitakachokuwa mwongozo mkuu kwetu.Kwenye uchambuzi huo tutajifunza kuhusu utajiri na ukwasi na njia tatu za kupata utajiri na ukwasi. Na pia tutajifunza ngazi tano za ujasiriamali, kuanzia sifuri ambayo ni kuajiriwa, kisha kujiajiri, umeneja, umiliki, uwekezaji na hatimaye ujasiriamali.Huu ni uchambuzi muhimu sana ambao pia utaendelea kwa kina...
2022-01-24
3h 19
Ongea Na Kocha.
Ongea Na Kocha; Breakfast With Seneca (Falsafa Ya Ustoa)
Habari Mwanamafanikio?Karibu kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA ambapo tumepata nafasi ya kujadili kwa kina uchambuzi wa kitabu kinachoitwa Breakfast With Seneca.Ni kitabu kinachoelezea vizuri falsafa ya Ustoa kwa namna inavyoweza kutumika kwenye zama tunazoishi sasa.Mwandishi amekusanya pamoja kazi za Seneca kwa namba ambayo zinajibu changamoto nyingi tunazokabiliana nazo kwa sasa.Baadhi ya changamoto kubwa ambazo kitabu hiki kimeziangalia ni;Hasira.Hofu na wasiwasi.Utajiri na Umasikini.Magumu na changamoto mbalimbali.Muda.Kwa ujumla, kitabu kizima kinatusaidia...
2022-01-17
1h 58
Ongea Na Kocha.
ONGEA NA KOCHA; Safari Ya Maisha Ya Farhia Omar.
Habari wanamafanikio?Karibuni kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA ambapo tumefanya mahojiano na mwanamafanikio mwenzetu Farhia Omar aliyetushirikisha safari yake ya maisha.Farhia ametushirikisha historia fupi ya maisha yake tangu kuzaliwa.Ametushirikisha kusoma na kufanya kazi kabla ya kusafiri kwenda nje ya nchi.Ametushirikisha sababu zilizomsukuma kwenda nje ya nchi na maisha ya huko.Ameshirikisha kazi mbalimbali ambazo amewahi kufanya, ikiwepo kwenye kampuni ya Amazon na yale aliyojifunza kwenye kila kazi.Ametushirikisha pia biashara mbalimbali ambazo amewahi kufanya na jinsi zimekuwa na changamoto kubwa kwake.Na...
2022-01-10
2h 56
Ongea Na Kocha.
Ongea Na Kocha; Uwajibikaji, Tribe Na Isaack Zake.
Habari mwanamafanikio?Karibu kwenye kipindi hiki cha ONGEA NA KOCHA ambapo unakwenda kujifunza yafuatayo.Kwenye somo la juma utajifunza umuhimu wa kuwa kwenye jamii ambayo inakuwajibisha ili kuweza kufanya makubwa. Kwa asili sisi binadamu ni wavivu na huwa tunapenda kufanya vitu rahisi. Lakini hivyo haviwezi kutufikisha kwenye mafanikio. Tunahitaji sana kuwa kwenye jamii zinazotusukuma kufanya makubwa ili tuweze kufanikiwa.Kwenye kitabu cha juma tunajifunza kutoka kitabu kinachoitwa Tribe: On Homecoming and Belonging kilichoandikwa na Sebastian Junger. Sisi binadamu ni viumbe wa kijamii na hivyo tunafanya vizuri sana tunapokuwa ndani ya jamii inayotuelewa, kututegemea na...
2022-01-07
3h 13
Ongea Na Kocha.
Ongea Na Kocha; Andika, Dedicated, Selemani Mbwambo.
Habari Mwanamafanikio?Karibu usikilize kipindi cha ONGEA NA KOCHA ambacho kina mambo makubwa na muhimu kama ifuatavyo;Kwenye somo la juma utajifunza umuhimu wa Kuandika vitu ili uweze kufikiri vizuri na kuweza kuvikamilisha. Unapofikiria tu vitu huvipi msisitizo mkubwa kama ukiviandika chini. Hivyo unapaswa kujijengea utamaduni wa kuyaandika malengo yako kila siku, kuandika mipango yako ya siku, kuandika yale uliyojifunza na kuandika tathmini zako binafsi. Sikiliza kipindi kujifunza hilo kwa kina.Kwenye kitabu cha wiki utapata uchambuzi wa kitabu Dedicated: The Case for Commitment in an Age of Infinite Browsing kilichoandikwa na Pete Davis...
2021-12-20
3h 32
Ongea Na Kocha.
ONGEA NA KOCHA; Kupata Hamasa Isiyoisha, Kitabu cha Four Thousand Weeks na Mahojiano na Regina Panga.
Karibu mwanamafanikio kwenye kipindi hiki cha ONGEA NA KOCHA.Kwenye kipindi hiki unakwenda kujifunza mengi kwa kina kama ifuatavyo.Kwenye somo la juma tunajifunza jinsi ya kupata hamasa isiyoisha ili uweze kuyafanyia kazi malengo yako bila kurudi nyuma. Hapa utajifunza hatua tano za kuchukua kwenye kila siku yako ili kuchochea hamasa yako.Kwenye kitabu cha juma utajifunza dhana kuu ya udhibiti na usimamizi mzuri wa muda wako ambayo ni muda tayari una ukomo huku mambo ya kufanya yakiwa mengi. Kwa kukubali ukomo huo wa muda na kuchagua yapi unafanya na yapi hufanyi itakusaidia sana...
2021-12-06
3h 09
Ongea Na Kocha.
ONGEA NA KOCHA; Wewe Ni Mshindi, Third Door na Ernest Paschal.
Karibu mwanamafanikio kwenye kipindi cha juma cha ONGEA NA KOCHA.Kwenye kipindi hiki unakwenda kupata yafuatayo;Moja ni somo la wewe ni mshindi, ambapo nimekushirikisha kwa kina namna ya kufikiri kama mshindi, kufuta kabisa mbadala na kupambana mpaka ufanikiwe.Mbili ni uchambuzi wa kitabu cha Third Door ambapo mwandishi ameshirikisha njia mbadala ambayo wale waliofanikiwa sana walizitumia katika kuanza safari yao ya mafanikio.Tatu ni mahojiano na mwanamafanikio mwenzetu Ernest Paschal ambaye anatushirikisha safari yake ya mafanikio aliyopitia maanguko mengi ila akawaza kuinuka na kuendelea na mapambano.Nne ni mjadala...
2021-11-29
3h 36
Ongea Na Kocha.
ONGEA NA KOCHA; Kisima Ni Jeshi, Amri 21 Za Maisha na Godfrey Mbise.
Habari Mwanamafanikio?Karibu usikilize kipindi cha ONGEA NA KOCHA ambapo kwa juma hili kuna mambo makubwa matatu.Moja ni mafanikio ni vita, KISIMA CHA MAARIFA ni jeshi na wewe ni mwanajeshi kwenye hii vita. Hapa utajifunza kwa ufupi sifa za wanajeshi wa Sparta na mambo muhimu ya kuzingatia kwenye jeshi hili la KISIMA.Mbili ni uchambuzi wa kitabu kinachoitwa Musashi's Dokkodo (The Way of Walking Alone) ambacho kina Amri 21 za maisha ya kishujaa. Katika amri hizo 21 kuna mengi sana ya kujifunza katika kuishi maisha ya kijeshi.Tatu ni mahojiano na mwanamafanikio mwenzetu...
2021-11-22
3h 19
Ongea Na Kocha.
ONGEA NA KOCHA; Nguvu Ya Fikra, The Prophet, Sebastian Kalugulu.
Karibu kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA ambapo unakwenda kujifunza mambo matatu makubwa.Moja ni Nguvu ya fikra kwenye safari ya mafanikio. Hapa utajifunza jinsi fikra zako zilivyo na nguvu ya kuumba na jinsi ya kujenga fikra sahihi na kuzilinda.Mbili ni uchambizi wa kitabu cha The Prophet ambapo utajifunza mambo mengi kuhusu maisha, makubwa yakiwa Upendo, Kazi na Thamani.Tatu utajifunza kutoka kwa mwanamafanikio mwenzetu Sebastian Kalugulu kwenye safari yake ya mafanikio ambayo ina mafunzo mengi ya mapambano bila ya kukata tamaa.Karibu sana usikiliza kipindi hiki ili uweze kujifunza na...
2021-11-08
3h 25
Ongea Na Kocha.
Ongea Na Kocha; Kuanza Mwaka Wa Mafanikio 2021/2022.
Habari mwanamafanikio?Karibu kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA cha kuuanza mwaka mpya wa mafanikio 2021/2022.Kwenye kipindi hiki nimeeleza kwa kina mwongozo wetu ambao tutakwenda nao kwa mwaka huo mzima wa mafanikio.Nimetoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali, ikiwepo lengo la thamani ya utajiri, kwa kuzidisha mara mbili ya ile thamani uliyonayo sasa.Pia kumekuwa na michango mizuri ya wanamafanikio wengine walioshiriki kipindi moja kwa moja.Mwisho kabisa nimejibu maswali ya wanamafanikio waliyouliza kuhusu mambo mbalimbali.Karibu sana usikilize kipindi hiki ili upate uelewa mzuri way ale tunayokwenda kufanyika...
2021-11-01
2h 58
Ongea Na Kocha.
ONGEA NA KOCHA; HILLARY CHUWA, SAFARI YA BIASHARA.
This is a public episode. If you would like to discuss this with other subscribers or get access to bonus episodes, visit mafanikio.substack.com
2021-09-19
2h 01
Ongea Na Kocha.
ONGEA NA KOCHA; MREJESHO WA TATHMINI ZA AGOSTI 2021
This is a public episode. If you would like to discuss this with other subscribers or get access to bonus episodes, visit mafanikio.substack.com
2021-09-19
2h 02
Ongea Na Kocha.
ONGEA NA KOCHA; MWONGOZO WA KISIMA CHA MAARIFA
This is a public episode. If you would like to discuss this with other subscribers or get access to bonus episodes, visit mafanikio.substack.com
2021-09-19
2h 02
Ongea Na Kocha.
ONGEA NA KOCHA; TUMAINI JONAS, CHANGAMOTO KWENYE UCHENJUAJI MADINI.
This is a public episode. If you would like to discuss this with other subscribers or get access to bonus episodes, visit mafanikio.substack.com
2021-09-19
2h 01
Ongea Na Kocha.
ONGEA NA KOCHA EP 20; EMMANUEL SALUM, SAFARI YA BIASHARA.
This is a public episode. If you would like to discuss this with other subscribers or get access to bonus episodes, visit mafanikio.substack.com
2021-09-19
2h 13
Ongea Na Kocha.
Mjadala wa kitabu ZERO TO ONE cha Peter Thiel
This is a public episode. If you would like to discuss this with other subscribers or get access to bonus episodes, visit mafanikio.substack.com
2021-09-19
1h 54
Ongea Na Kocha.
Mjadala; Smart People Should Build Things.
This is a public episode. If you would like to discuss this with other subscribers or get access to bonus episodes, visit mafanikio.substack.com
2021-09-19
2h 08
Ongea Na Kocha.
Mjadala; How To Win Friends.
This is a public episode. If you would like to discuss this with other subscribers or get access to bonus episodes, visit mafanikio.substack.com
2021-09-19
2h 16
Ongea Na Kocha.
MJADALA; THE WEALTHY GARDENER
This is a public episode. If you would like to discuss this with other subscribers or get access to bonus episodes, visit mafanikio.substack.com
2021-09-19
2h 00
Ongea Na Kocha.
MJADALA; ANYTHING YOU WANT cha DEREK SIVERS
This is a public episode. If you would like to discuss this with other subscribers or get access to bonus episodes, visit mafanikio.substack.com
2021-09-19
2h 20
Ongea Na Kocha.
Mjadala wa kitabu Secrets of Millionaire Mind cha T. Harv Eker
This is a public episode. If you would like to discuss this with other subscribers or get access to bonus episodes, visit mafanikio.substack.com
2021-09-19
2h 05
Ongea Na Kocha.
Johnbosco Boniphace; Safari ya Kibiashara.
Habari wanamafanikio?Karibuni kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA ambapo mwanamafanikio mwenzetu Johnbosco Boniphace anatushirikisha safari yake ya biashara.Kwenye kipindi hiki utajifunza yafuatayo;Jinsi alivyoweza kukusanya mtaji kupitia fedha ya kujikimu chuoniJinsi alivyoweza kutumia changamoto kuona fursa ya kuanzisha biashara.Jinsi alivyokuwa king'ang'anizi mpaka kupata eneo zuri la kufanyia biashara.Nidhamu yake ya hali ya juu katika kuendesha biashara yake.Upinzani kutoka kwa wengine kutokana na mafanikio anayoanza kupata.Kuzushiwa imani za kishirikina kutokana na hatua za tofauti anazopiga.Msukumo...
2021-08-12
2h 18
Ongea na Coach Makirita Amani's show
AUDIO; PATA MASAA MAWILI YA ZIADA KILA SIKU.
Muda umekuwa ni changamoto na kikwazo kwa wengi kufikia malengo yao ya kimaisha. Kila siku tumekuwa tunasema kama ningekuwa na muda wa ziada ninge.... Lakini siku zinakwenda na hatuoni kupatikana kwa muda huo wa ziada. Tunaamua kuzika ndoto zetu kwa sababu hatukupata muda wa kuzifanyia kazi. Vipi leo nikikuambia kwamba unaweza kupata masaa mawili ya ziada kila siku? Ndiyo namaanisha masaa mawili, dakika 120 za ziada kwenye siku yako ya kawaida? Ni mangapi makubwa utaweza kuyafanya na kubadili kwenye maisha yako kwa nyongeza ya masaa mawili kila siku? Kwenye kitabu hiki siyo tu ninakuambia ya kwamba unaweza kupata masaa mawili ya...
2017-02-03
14 min