podcast
details
.com
Print
Share
Look for any podcast host, guest or anyone
Search
Showing episodes and shows of
Tanzania National Parks (TANAPA)
Shows
TANAPA PODCAST
TANAPA PODCAST EPISODE 13 - Mila na Tamaduni zilizohusisha mizimu katika kuhifadhi Maliasili
Episodi hii inakuletea mazungumzo ya kina kuhusu mila, tamaduni na makatazo ya Kabila la Wagongwe lililopo mkoani Katavi na jinsi taratibu hizo zilivyochangia kulinda maliasili na vyanzo vya maji. Mathalani; ilikuwa hairuhusiwi kukata miti iliyokuwa katika vyanzo vya maji kutokaana na imani ya kuwepo kwa nyoka mkubwa wala kuua mnyamapori hadi upewe kibali na pepo au jini Katabi anayepatikana katika Hifadhi ya Taifa Katavi. Sikiliza simulizi hii ya kuvutia katika epsodi ya 13.Eneo: Hifadhi ya Taifa KataviMwongoza kipindi: Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Catherine Mbena Wageni:1. Moses Edward Tende ( Mtemi Sigulu) Chifu wa Kabila la Wagongwe.2. Lukas Moses Msaga - Mtoto wa...
2025-10-20
54 min
TANAPA PODCAST
TANAPA PODCAST EPISODE 12 - Zoezi la Uhamishaji Tembo kutoka Misenyi kwenda Hifadhi ya Taifa Burigi - Chato.
Episodi hii imeangazia zoezi endelevu la kuwahamisha tembo walowezi kutoka maeneo ya karibu na wananchi kwenda hifadhini na zoezi zima la kuwaswaga tembo waliotoka hifadhini kuvamia maeneo ya wananchi na kuwarudisha hifadhini.Sikiliza Episodi hii kwa taarifa hiyo na mengine mengi kupitia Epsode ya 12.Eneo: Misenyi - Bukoba.Host: Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Catherine MbenaGuests: Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi Dkt. Fredrick Mofulu - Mkuu wa Hifadhi Ibanda - Kyerwa. NaKamishna Msaidizi wa Uhifadhi...
2025-10-16
50 min
TANAPA PODCAST
TANAPA PODCAST EPISODE 11 - Nyumba ya Kumbukizi ya Mwl. Nyerere na Historia ya Taifa letu.
Kuelekea Kumbukizi ya Kifo cha Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere Oktoba 14, TANAPA PODCAST tunakueletea uchambuzi kuhusu historia ya harakati za uhuru wa Tanganyika zilizoongozwa na Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere. Hapa utapata kujifunza mengi kuhusu harakati za Uhuru wa Tanganyika na Afrika kwa ujumla.Ikumbukwe historia hii imehifadhiwa katika Nyumba ya Kumbukizi ya Mwl. Nyerere iliyopo Magomeni Usalama jijini Dar es Salaam. Fuatilia uhondo huo katika Epsode ya 11.Eneo: Dar es salaamHost: Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, C...
2025-10-13
41 min
TANAPA PODCAST
TANAPA PODCAST EPISODE 10 - MAANDALIZI YA TWENZETU KILELENI 2025 NA PROF. KAMUZORA
Episodi hii inaangazia mazungumzo ya kina kuhusu zoezi la upandaji wa Mlima Kilimanjaro ambapo Profesa Kamuzora anaeleza uzoefu wake katika kupanda mlima kwa muda mrefu.Fahamu faida ya kushiriki kampeni ya “Twenzetu Kileleni katika kuadhimisha kumbukumbu ya uhuru wa Taifa letu, kuhamasisha utalii pamoja na utunzaji wa mazingira.Host: Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Catherine Mbena - Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano - TANAPAGuest: Prof. Faustin Kamuzora - Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi UTT AMIS.
2025-10-09
44 min
TANAPA PODCAST
TANAPA PODCAST EPISODE 09 - YAFAHAMU MAENEO YA MALIKALE YALIYOKASIMISHWA TANAPA
Episodi hii inaangazia maeneo ya Malikale yanayosimamiwa na TANAPA na faida zake. Maeneo hayo yamebeba historia za kale, biashara ya utumwa, utawala wa machifu, ukoloni na uhuru wa Taifa letu. Sikiiiza TANAPA PODCAST Epsode 09 upate elimu ya kina kuhusu historia ya Taifa letu, asili na umuhimu wa kutunza tamaduni zetu. Eneo: Dar es Salaam. Host: Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Catherine Mbena. Guest: Afisa Uhifadhi Mkuu Malikale, Neema Mbwana.
2025-10-06
56 min
TANAPA PODCAST
TANAPA PODCAST EPISODE 08 - MAANDALIZI YA TWENZETU KILELENI 2025 NA CDF (Mst.) GEORGE WAITARA
Katika Episode hii tunaangaIa mazungumzo ya kuhusu Kampeni ya Twenzetu Kileleni 2015 inayofanyikaga Desemba 09 kila mwaka kukumbuka mashujaa wetu waliopigania uhuru wa Tanganyika ambapo kwa mwaka huo huo bendera ya Taifa ilipandishwa Mlima Kilimanjaro wenye kilele kirefu kuliko vyote Barani Afrika chenye urefu wa mita “5985 asl” kuangazia nuru ya Uhuru ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.Sikiliza TANAPA PODCAST Epsode 08 kwa habari za kweli na uhakika kuhusiana na historia ya Taifa letu, Uhifadhi na Utalii.Eneo: Dar es Salaam.Host: Kamishna Msai...
2025-10-02
40 min
TANAPA PODCAST
TANAPA PODCAST EPISODE 07 - Uchambuzi wa maneno yenye mkanganyiko katika Sekta ya Uhifadhi na Utalii
Episodi hii inaangazia uchambuzi wa kina kuhusu maneno mbalimbali yanayoleta mkanganyiko wa maana na matumizi yake katika jamii.Katika Episode 07 Mtopezi wa lugha ya Kiswahili kutoka Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) Ndugu Oni Sigala anachambua na kudadavua maneno kadha wa kadha yenye utata katika sekta ya uhifadhi na utalii.Eneo: Dar es salaamMwongozaji: Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Catherine MbenaMgeni: Oni Sigala - Mhariri Mwandamizi Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA)Usikose kila Jumatatu kupitia Platifomu za TANAPA P...
2025-09-29
43 min
TANAPA PODCAST
TANAPA PODCAST EPISODE 06 - Mila, Desturi na Tamaduni katika Uhifadhi wa Maliasili
Sikiliza Episode 06 uchambuzi wa kina katika mwendelezo wa mada inayoeleza elima ya Uhifadhi ikihusisha Mila, Desturi, Tamaduni na Miiko iliyozuia uharibifu wa Maliasili za Taifa ambapo moja ya maeneo hayo kwa sasa ni Hifadhi za TaifaHost: Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Catherine MbenaGuest: Naibu Kamishna wa Uhifadhi na Maendeleo ya Biashara, Massana Mwishawa.
2025-09-22
37 min
TANAPA PODCAST
TANAPA PODCAST EPISODE 05 - Mila, Desturi na Tamaduni katika Uhifadhi wa Maliasili
TANAPA Podcast Episode 05 inaangazia mwendelezo wa mada inayoeleza elimu ya Uhifadhi iliyohusisha Mila, Tamaduni, Desturi na Miiko anuwai iliyozuia baadhi ya wanyamapori kuuwawa lengo likiwa ni kuhifadhi maliasili zilizokuwa ndani ya maeneo yaliyohifadhiwa ambayo baadhi yake kwa sasa ndio Hifadhi za Taifa tunazozishuhudia zikitiririsha nyomi ya watalii nchini.Eneo: Hifadhi ya Taifa SerengetiMwongozaji: Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Catherine MbenaWageni: Barnabas Murigo, Kenyatta, Musoka na Stanslaus MayaniUsikose kila Jumatatu saa 11:00 jioni kupitia TANAPA Podcast.TANAPA...
2025-09-15
1h 33
TANAPA PODCAST
TANAPA PODCAST EPISODE 04 Mila, Desturi na Tamaduni zilizotumika katika Uhifadhi wa Maliasili
Episode hii inaangazia mazungumzo kati ya Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano TANAPA, Catherine Mbena na Mzee Fanuel Mbise, Eliona Miley na Elikesia Akyoo kuhusu elimu ya Uhifadhi kupitia mila, desturi na tamaduni zilizotumika katika kusheshimu na kutunza maliasili zilizokuwa zimehifadhiwa.
2025-09-08
57 min
TANAPA PODCAST
TANAPA PODCAST EPISODE 03 Chimbuko la Uhifadhi
Sikiliza TANAPA Podcast, Episode 03 uelimike kuhusuChimbuko la UhifadhiUanzishaji wa Hifadhi mpya na malengo yakeMaeneo matano ya Malikale yaliyokasimishwa TANAPA naUzalendo katika kutembelea Hifadhi za Taifa.Mgeni maalum: Nakaaya Sumari (Tanzania Safari Channel)Host: ACC Catherine Mbena, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano TANAPAFuatilia mfululizo huu wa elimu ya uhifadhi, utalii na mirindimo iliyojaa burudani na maarifa tele.
2025-08-25
43 min
TANAPA PODCAST
TANAPA PODCAST EPISODE 02 - Kazi mbalimbali zinazofanywa na TANAPA
Katika episode ya pili ya mfululizo huu, Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano TANAPA, Catherine Mbena anaelezea kwa kina kazi mbalimbali zinazofanywa na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) katika kuhakikisha maliasili zilizopo ndani ya hifadhi za Taifa zinaendelea kulindwa na kuhifadhiwa kwa faida ya kizazi hiki na vizazi vijavyo.
2025-08-17
19 min
TANAPA PODCAST
TANAPA PODCAST EPISODE 01 Utangulizi kuhusu TANAPA na majukumu yake
Katika episode hii ya kwanza, tunazungumzia kwa kina kuhusu Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) – kuanzia majukumu yake makuu, muundo wa utendaji kazi, hadi maeneo ya hifadhi yanayosimamiwa chini ya sheria. Ni programu endelevu inayokufahamisha nafasi muhimu ya TANAPA katika kulinda maliasili na kukuza mapato yatokanayo na shughuli za utalii.
2025-08-11
17 min