podcast
details
.com
Print
Share
Look for any podcast host, guest or anyone
Search
Showing episodes and shows of
Uongoziwakiroho
Shows
The Uongozi Wa Kiroho Podcast
Tulee Wengine Wawe Nasi Katika Uongozi
Mchungaji Cyprian Michael anatushauri juu ya uongozi wa familia na uongozi kanisani katika podcast hii. Badala ya kuongoza tukiwa peke yetu, anatuhimiza kulenga watu wenye sifa na uwezo wa kuongoza na kuwaandaa ili wawe bega kwa bega pamoja nasi katika uongozi na wawe tayari kushika uongozi wa huduma siku zijazo.
2023-05-18
08 min
The Uongozi Wa Kiroho Podcast
Tufanye Uanafunzi!
Mchungaji Emmanuel Mwankasole kutoka Dodoma, Tanzania anatukumbusha juu ya umuhimu wa kufanya uanafunzi. Baada ya kujibu swali la msingi "Kwa nini tufanye?" yeye anaendelea kutoa mafunzo mazuri sana kwa ajili ya viongozi, namna ya kufanya uanafunzi na faida tutakazoziona tukifanya uanafunzi kwa uaminifu. Bila shaka utabarikiwa na kujengwa na podcast hii.
2023-03-20
20 min
The Uongozi Wa Kiroho Podcast
Afya Ya Kiroho
Kiongozi D. Kitang'wa anatushauri kuhusu afya katika mwili wa Kristo. Ili afya ya kiroho iwe nzuri, inabidi sisi tulio viongozi wa kiroho tufundishe watu wetu vizuri. Haitoshi tu kuwafundisha kuepukana na dhambi ambazo zimekatazwa na Mungu katika Neno lake, lakini tunapaswa kuwafundisha kutii na kutenda tuliyoamriwa naye vilevile.
2023-02-05
09 min
The Uongozi Wa Kiroho Podcast
Kanuni Muhimu - Seh. 1
Sisi sote tuna mawazo yetu juu ya kanisa na uongozi katika kanisa, lakini mawazo yetu siyo sawa. Ni kwa sababu tumeathiriwa na mila na utamaduni pamoja na uzoefu wetu tangu utoto. Kuna aina mbalimbali za makanisa na namna tofauti tofauti za uongozi katika kanisa. Je, zote zinakubalika? Zote ni za kibiblia? Podcast hii na zingine zifuatazo zitahusu mada hii ya kanuni muhimu kutoka Neno la Mungu zinazotuongoza tuwe na kanisa la kibiblia na uongozi unaokubaliwa na Bwana.
2022-12-03
16 min
The Uongozi Wa Kiroho Podcast
Kulea Viongozi Wengine
Mzee Smith anazungumza na mchungaji ambaye, pamoja na kuongoza kanisa na kufanya huduma nyingine nyingi, anaweka mkazo katika kazi muhimu ya kulea viongozi wengine. Sikiliza mashauri yake namna ya kutambua viongozi wa siku zijazo na jinsi ambavyo mchungaji anaweza kuwafundisha na kuwalea katika kanisa.
2022-10-15
12 min
The Uongozi Wa Kiroho Podcast
Mauti Imemezwa
Tunapoomboleza kifo cha ndugu zetu, viongozi wenzetu, hebu tukumbuke mambo haya.
2022-08-11
07 min
The Uongozi Wa Kiroho Podcast
Uzazi Bora
Tuko na mkurugenzi wa Huruma Children’s Home katika podcast ya leo. Mzee Smith alikaa naye ili kumhoji juu ya ulezi wa watoto na vile ambavyo tunaweza kuwa wazazi bora katika ulezi wetu wa watoto. Usikose podcast hii ambayo imejaa hekima na mashauri mazuri kwa ajili yetu sisi tulio wazazi.
2022-06-02
14 min
The Uongozi Wa Kiroho Podcast
Mafunzo Jangwani, Seh. ya 2
Katika podcast hii tunaendelea kujifunza kutoka kwa mfano wa Musa aliyepelekwa na Bwana jangwani kwa ajili ya mafunzo. Wakati ulipowadia atoke jangwani na kuingia katika huduma alikataa, akiona hawezi. Pengine wewe unatoa udhuru kama Musa. Tuone Mungu anasemaje juu ya kiongozi aliyeweza kutumiwa naye kutenda makuu.
2022-05-04
11 min
The Uongozi Wa Kiroho Podcast
Mafunzo Jangwani, Seh. ya 1
Je, kiongozi mkuu ni yule ambaye ni mnenanji mzuri, ana talanta na vipaji vya pekee, na anasifiwa na watu? La, hasha. Katika mfano wa Mtumishi Musa tunaona kwamba mara nyingi ni kinyume. Kiongozi mkuu ambaye Mungu hupenda kumtumia ni yule ambaye amepita katika jangwa na kujifunza kuwa mwaminifu katika madogo, akimtegemea Bwana kwa unyenyekevu.
2022-04-06
10 min
The Uongozi Wa Kiroho Podcast
Awamu Mpya
Tunamkaribisha Mzee Vernon Smith ambaye anajiunga na huduma ya podcast ya Uongozi wa Kiroho na atakuwa akichangia podcast mara kwa mara.
2022-03-04
11 min
The Uongozi Wa Kiroho Podcast
Agizo Kuu na Wajibu Wetu
Wajibu wa kila mwamini na kila kanisa ni kutii Agizo Kuu la Yesu. Lakini kweli inawezekana katika mahali ambapo kanisa ni maskini kiuchumi na vikwazo ni vingi? Kwa njia gani mtu anayesikia wito wa kupeleka Injili kwa wasiowahi kusikia Habari Njema anaweza kujiandaa na kuenda? Maswali kama hayo ni mada ya podcast hii tunapoendelea na mahojiano na Dr. Richard Lewis.
2022-01-28
16 min
The Uongozi Wa Kiroho Podcast
Agizo Kuu na Kanisa la Afrika
Dr. Richard Lewis anaeleza vile ambavyo mustakabali wa huduma ya umisionari umo mikononi mwa kanisa la Marekani ya Kusini, Asia na Afrika na anatoa changamoto kwa ajili ya wasikilizaji wa podcast tuwe tayari kujibu wito wa Bwana pasipo hofu na kuongoza makanisa yetu kufundisha, kutuma na kusapoti wamisionari wanaopeleka injili kwa watu wasiowahi kusikia habari njema ya wokovu katika Yesu.
2021-12-30
16 min
The Uongozi Wa Kiroho Podcast
Sifa za Kiongozi 4 - Msingi Wako
Inawezekana kiongozi wa mambo ya kiroho asisome Neno la Mungu kwa uaminifu? Ndiyo. Katika podcast hii kuna mashauri na mapendekezo kwa ajili ya kiongozi wa kiroho ambaye ana moyo wa kujenga maisha na huduma yake juu ya msingi ulio bora.
2021-11-27
15 min
The Uongozi Wa Kiroho Podcast
Sifa za Kiongozi 3 - Fedha ya Aibu
Kila kiongozi wa kiroho anapaswa kujiuliza swali: “Kwa nini ninamtumikia Bwana?” Amini, usiamini, kuna viongozi wengi ambao wamesahau wito wao na maana yake na wameanza kufanya huduma kwa ajili ya mapato. Katika podcast hii tutaangalia Neno la Mungu kwa viongozi kupitia waraka wa Paulo kwa Timotheo. Je, unatamani fedha ya aibu?
2021-10-27
15 min
The Uongozi Wa Kiroho Podcast
Sifa za Kiongozi 2 - Kauli Moja
Katika podcast hii tunaendelea kukazia sifa muhimu za Kiongozi wa Kiroho. Lazima atawale ulimi wake na kutunza maneno yake na asiwe mtu wa kusengenya watu. Kiongozi awe mtu anayesema wazi, bila kuficha ficha maana yake, na asiwe mtu wa kuwasema watu wengine.
2021-09-02
12 min
The Uongozi Wa Kiroho Podcast
Maisha ya Umisionari
Mmisionari ambaye amekubali wito wa Bwana na kutumwa kwa watu wa lugha na utamaduni tofauti hupaswa kuzoea maisha mapya. Kuna changamoto nyingi, lakini pia kuna baraka kwa sababu ya kutii sauti ya Bwana na kumtegemea Yeye aliyemwita. Katika podcast hii tunaendelea na maongezi yetu na Mmisionari Daudi Likama na kusikia ushuhuda wake juu ya maisha na huduma yake Msumbiji. Bwana atumie ushuhuda wake ili kutuhimiza sisi sote na kufanya masikio yetu tayari kusikia wito wa Bwana kwa ajili yetu.
2021-08-02
18 min
The Uongozi Wa Kiroho Podcast
Kuitikia Wito wa Umisionari
Wengi walisema “haiwezekani!” Walidai kwamba Tanzania ni nchi maskini na kuna haja ya wamisionari kuja Tanzania na kuleta Injili. Lakini Mmisionari Mtanzania kutumwa na kanisa la Tanzania na kupeleka Injili nje si rahisi. Lakini Bwana aliita na Ndugu Likama aliitika. Jiunga nasi katika podcast hii na ijayo ili kusikia ushuhuda wa Ndugu Daudi Likama aliyetumwa na kanisa lake kupeleka habari njema ya wokovu Msumbiji.
2021-07-02
18 min
The Uongozi Wa Kiroho Podcast
Sifa za Kiongozi 1- Msimamo
Walio viongozi kweli kweli si viongozi wa jina tu, bali ni viongozi waliostahili kuongoza kutokana na msimamo wao na uaminifu wao mbele za Mungu na mbele ya watu. Katika podcast hii ya na podcast zifuatazo tutaangalia sifa za muhimu ambazo humfanya mtu awe kiongozi mwaminifu aliyetumiwa na Bwana kuongoza wengine vema.
2021-02-15
17 min
The Uongozi Wa Kiroho Podcast
Hekima Kutoka Kwa Kiongozi Mwanamke
Sikiliza mashauri na hekima ya mwanamke mwaminifu ambaye amekuwa kiongozi wa kiroho siku nyingi. Katika podcast hii tunamwuliza juu ya familia yake, huduma yake, baraka na changamoto anazoziona katika uongozi wake n.k. Podcast hii si tu kwa ajili ya akina dada. Kiongozi mwanamume, sisi pia tunahitaji hekima hii kutoka kwa Mama Moses. Karibu tusikilize!
2021-01-30
13 min
The Uongozi Wa Kiroho Podcast
Ubora wa Viongozi Wanawake
Je, ni lazima mwanamke awe nyuma ya mwanamume katika ulimwengu wa uongozi? Wanawake wanafaa tu kusaidia waume zao na wanaume wengine, au wanawake wanafaa kuongoza wenyewe katika mambo ya kiroho? Katika podcast hii tunaongea na wanawake waaminifu walio viongozi wenyewe. Ni wake wa wachungaji na wasaidizi wa waume zao katika huduma. Lakini hawa wanawake ni zaidi ya wasaidizi. Wenyewe wanaongoza katika huduma na wao wenyewe ni viongozi katika mambo ya kiroho.
2021-01-15
22 min
The Uongozi Wa Kiroho Podcast
Tafakari Njia Yako
Heri ya Mwaka Mpya! Siku za kwanza za mwaka mpya ni wakati mzuri wa kutathmini juu ya maisha yetu, huduma yetu, na hali yetu ya kiroho kama viongozi. Podcast hii ni ujumbe maalum nilioandaa kwa ajili yako tunapoanza mwaka 2021. Kama umeanza kuchoka, kushuka moyo, au kukosa maono katika huduma, naomba usikilize podcast hii na kutiwa moyo. Tutaangalia mfano wa watu wa Mungu waliochoka na kupoteza furaha katika huduma, lakini kupitia ujumbe wa nabii wa Mungu walisaidiwa sana na hatimaye kuona mafanikio, ridhaa, na furaha katika huduma yao mbele za Bwana.
2021-01-01
13 min
The Uongozi Wa Kiroho Podcast
Kiongozi na Timu Yake 2
Si watu wote wanaofaa kufanya huduma katika timu. Kiongozi lazima awe na tabia fulani na wanatimu pia wawe watu wa namna ya pekee. Sikiliza podcast hii tunapoendelea na mada ya "timu" na kuzungumzia ubora wa kufanya huduma pamoja na watu wengine wanaofaa.
2020-11-30
12 min
The Uongozi Wa Kiroho Podcast
Kiongozi na Timu Yake 1
Mhubiri alisema, "Afadhali kuwa wawili kuliko mmoja; kwa sababu wana tuzo njema kwa kazi yao." (Mhubiri 4:9). Katika podcast hii na podcast ijayo tutasikia kutoka kwa kiongozi wa kiroho ambaye amekuwa akiongoza timu katika huduma siku nyingi, katika mahali ambapo ardhi ni ngumu na nguvu ya timu ni muhimu. Anatushauri namna gani tunaweza kuwekeza katika watu wengine na kuona manufaa na matunda kwa kufanya huduma pamoja.
2020-11-15
16 min
The Uongozi Wa Kiroho Podcast
Kuishi Kama Mfu
Sisi tulio viongozi wa kiroho mara nyingi huathiriwa na sauti za watu waliotuzunguka. Sauti za sifa, na sauti za malalamiko hufuatana na kiongozi yeyote siku zote. Lakini Biblia inasema nini juu ya sauti zile? Kama wafuasi wa Yesu Kristo, sisi tunapaswa kuishi kama watu waliosulibiwa. Kwa maneno mengine, tumtegee Mungu sikio letu na kutosikiliza sana sauti za watu aidha wanapotusifu au wanapolalamika juu yetu.
2020-10-30
11 min
The Uongozi Wa Kiroho Podcast
Kufikia Vijana Wasiookoka
Katika podcast hii ya tatu tunamaliza mkazo wetu juu ya Huduma ya Vijana na kusikia kutoka kwa Ndugu Abraham Stanslaus kuhusu kuwafikia vijana wasiookoka. Haitoshi kuandaa huduma nzuri kanisani na kukaribisha vijana. Ni juu yetu kutafuta vijana wanaohitaji habari njema na kuwapelekea Injili popote walipo. Kwa njia gani? Kiongozi huyu anatushirikisha vile wanavyofanya kanisani kwao.
2020-10-15
20 min
The Uongozi Wa Kiroho Podcast
Kwa Njia Gani Tulenge Vijana?
Tumeisha ona kwamba tusipolenga vijana na kuwafikia na Injili tutapoteza nafasi ya kufikia kizazi kijacho na kushindwa kuona mafanikio kanisani. Vijana ni muhimu. Lakini vijana wana mahitaji ya pekee na kuna majaribio mengi sana yanayowavuta siku hizi. Kwa njia gani tunaweza kuwahudumia na kuwafikia kama viongozi kanisani? Katika podcast ya leo na ijayo tutapata mashauri kutoka kwa Mchungaji Abraham Stanslaus na tutaendelea kuhimizwa kuwalenga vijana katika huduma zetu.
2020-09-30
16 min
The Uongozi Wa Kiroho Podcast
Kwa Nini Tulenge Vijana?
Tusipolenga kuwafikia vijana, tutapoteza kizazi cha sasa, tutakosa nguvu katika huduma, na tutashindwa kuendeleza Injili popote tulipo. Katika podcast hii tunazungumza na mtu ambaye ana moyo wa kuhudumia vijana na amefanya huduma ya vijana kwa mafanikio ya juu kwa siku nyingi. Sikiliza anapoeleza umuhimu wa huduma ya vijana na kutusihi kuwalenga vijana katika huduma zetu ndani na nje ya kanisa.
2020-09-15
19 min
The Uongozi Wa Kiroho Podcast
Tuwe Radhi Kuumizaana
Kila Kiongozi wa Kiroho anahitaji watu wa namna mbili katika maisha yake. Anahitaji maadui wanaosema ukweli na anahitaji marafiki waaminifu wasemao ukweli. Na yeye kama kiongozi anapaswa kuwa tayari kusema ukweli na watu wengine hata ingawa maneno yake yatawaumiza. Ndiyo maana ya podcast hii, kwamba tuwe tayari kuumizaana kwa kusema maneno ya ukweli na kufanya kwa upendo.
2020-08-30
14 min
The Uongozi Wa Kiroho Podcast
Familia ya Kiongozi: Utunzaji wa Familia
Kwa njia gani kiongozi anaweza kutunza familia yake ili wawe na furaha na amani nyumbani na kuwa baraka na msaada katika huduma badala ya mzigo? Katika podcast hii tunaendelea na maongezi yetu na Mchungaji Onesimus Kibera juu ya familia ya kiongozi wa kiroho. Anatupa mashauri mazuri juu ya familia na namna gani kiongozi anaweza kuwaongoza familia ili wamfuate Bwana kwa pamoja na kwa moyo.
2020-08-15
16 min
The Uongozi Wa Kiroho Podcast
Familia ya Kiongozi: Umuhimu wa Familia
Pasipo familia yenye ushuhuda mzuri na sifa njema, kiongozi atakosa nguvu na msaada unaotakiwa katika huduma yake. Mchungaji Onesimus Kibera anashiriki nasi katika podcast hii akieleza umuhimu wa familia katika maisha na huduma ya kiongozi wa kiroho.
2020-07-30
18 min
The Uongozi Wa Kiroho Podcast
Nidhamu za Kiroho 2: Utunze Hali Yako ya Kiroho
Adui wetu hufurahi sana akiona kiongozi anayeacha nidhamu za msingi za kiroho na kuanza kujitegemea nguvu zake na hekima yake. Katika podcast hii tunaendelea na maongezi yetu na Mzee Vernon Smith juu ya maisha ya kiroho ya kiongozi. Mgeni wetu anatupa mashauri mazuri juu ya utunzaji wa hali yetu ya kiroho na umuhimu wa kutembea na Yesu kwa karibu siku zote.
2020-07-15
15 min
The Uongozi Wa Kiroho Podcast
Nidhamu za Kiroho 1: Maisha ya Kibinafsi ya Kiongozi
Mzee Vernon Smith yuko nasi katika podcast hii, akijibu maswali yangu juu ya Nidhamu za Kiroho katika maisha ya kiongozi. Katika podcast hii ya kwanza anatoa ushauri wake juu ya mambo ya lazima yaliyopaswa kuwemo katika maisha ya kiongozi wa kiroho ili adumu katika huduma na awe na ushuhuda mwema kama mtu wa Mungu.
2020-06-30
18 min
The Uongozi Wa Kiroho Podcast
Kiongozi Katika Jamii: Kinachoathiri Jamii Yetu
Ni nini inayoweza kubadilisha maisha ya watu na kuleta athari katika jamii? Ni Neno la Mungu. Mgeni wetu, Mchungaji Ngunjiri, anatoa mashauri juu ya nguvu ya Neno kubadili maisha ya watu na tunasihiwa kupanda Neno la Mungu katika huduma zetu na kumwachia Bwana afanye kazi na kuleta matunda kupitia Roho wake na Neno lake.
2020-06-15
13 min
The Uongozi Wa Kiroho Podcast
Kiongozi Katika Jamii: Huduma Yenye Maana
Huduma ya kiongozi inaweza kuwa na nguvu na kutumiwa na Bwana kuathiri jamii yake. Mchungaji Ngunjiri anasisitiza umuhimu wa kiongozi kushirikiana vizuri na majirani na watu wa eneo lake, na kuandaa huduma ambazo zinabariki jamii na kuwasaidia katika maisha yao ya kila siku. Kwa njia hiyo, Neno la Mungu linahubiriwa na watu wanaguswa.
2020-05-30
16 min
The Uongozi Wa Kiroho Podcast
Kiongozi Katika Jamii: Ushuhuda wa Familia
Mchungaji Stephen Ngunjiri anaeleza umuhimu wa kiongozi wa kiroho kuwa na sifa njema na ushuhuda mzuri katika jamii, na sio tu ushuhuda wake bali ni ushuhuda wa mkewe na watoto wake pia.
2020-05-15
15 min
The Uongozi Wa Kiroho Podcast
Kukabidhi Wengine Huduma Kwa Mafanikio
Tusipotumia hekima katika ugawaji wa huduma, badala ya kuona baraka na huduma kusonga mbele, tunaweza kujuta kwa nini nilimpa mtu fulani kazi. Katika episode hii ya mwisho katika mfululizo huu, kuna ushauri kuhusu kukabidhi wengine huduma kwa njia ambayo huleta mafanikio katika huduma na upevu katika maisha ya viongozi wa baadaye.
2020-04-30
15 min
The Uongozi Wa Kiroho Podcast
COVID 19 na Wewe
Daktari Robert Byemba ana mashauri kwa ajili yetu kuhusu virusi vya Korona (COVID 19) na kuhusu wajibu wetu kama viongozi wa kiroho. Sio wakati wa kuogopa na kuacha kufanya huduma, bali ni wakati wa kuchukua fursa ya hudumia wengine kwa ujasiri.
2020-04-10
21 min
The Uongozi Wa Kiroho Podcast
Kwa Njia Gani Nianze?
Uko tayari kushiriki mzigo wa huduma na wengine na kuwakabidhi wengine kazi. Unaanzaje? Katika episode hii tunajifunza hatua kwa hatua jinsi ya kuwashirikisha wengine katika huduma.
2020-03-31
15 min
The Uongozi Wa Kiroho Podcast
Jibu Letu Wakati wa Janga
Tunaishi katika wakati ambao ulimwengu haujawahi kuona. Watu wako katika hali ya woga na mashaka kutokana na virusi vya Korona 19. Kama viongozi wa kiroho, je, tunapaswa kujibu namna gani? Je, Mimi na wewe tunatakiwa kuishi namna gani katika wakati huu wa historia?
2020-03-20
13 min
The Uongozi Wa Kiroho Podcast
Kwa Nini Hatushiriki Kazi?
Kabla ya kujifunza kwa njia gani tunaweza kuwagawia wengine huduma, ni bora kuangalia sababu mbalimbali kwa nini viongozi wengine wanaona ni vigumu kuwashirikisha wengine kazi.
2020-02-29
13 min
The Uongozi Wa Kiroho Podcast
Upekee wa Uongozi
Kama kiongozi, una majukumu ya kipekee. Unapokabidhi huduma kwa wengine, kuna mambo kadhaa ambayo lazima uwe mwangalifu kufanya mwenyewe kama kiongozi.
2020-02-15
12 min
The Uongozi Wa Kiroho Podcast
Sababu ya Uchovu
Viongozi wengi wamechoka na wengine wamekata tamaa. Kwa nini? Katika episode hii ya kwanza tutaangalia mfano wa kiongozi wa Biblia aliyekuwa na shida hii na akapata ushauri kutoka kwa Mungu.
2020-01-30
13 min
The Uongozi Wa Kiroho Podcast
Karibu Usikilize!
Karibu usikilize podcast hii mpya inayohusu Uongozi wa Kiroho. Imeandaliwa maalum kwa ajili ya Viongozi wa Kiroho kanisani, nyumbani, au popote walipo wakiongoza wengine katika mambo ya kiroho. Katika kila episode kuna ushauri wa kiutendaji na mafundisho ya Biblia kusaidia kukidhi mahitaji ya viongozi wa kiroho.
2020-01-01
03 min