podcast
details
.com
Print
Share
Look for any podcast host, guest or anyone
Search
Showing episodes and shows of
Authentic Swahilians
Shows
SISINISISI PODCAST
SISINISISI S01 E09 - KUISHI MAISHA NJE YA NCHI UKIWA MBALI NA WAZAZI NDUGU NA JAMAA
KUISHI MAISHA NJE YA NCHI UKIWA MBALI NA WAZAZI NDUGU NA JAMAA
2025-06-19
1h 08
SISINISISI PODCAST
SISINISISI S01 E08 - JE UNAWEZA KUSAFIRI KUMFUATA MPENZI WAKO ALIE MBALI?
Kwenye episode hii Bad Man na The Road wanachambua committments ambazo zinajitokeza kwenye mahusiano hasa yale mahusiano ya mbali yaan long distance. Je unaweza kusafiri na kumfuata mpenzi wako alie mbali na wewe
2025-06-07
1h 02
SISINISISI PODCAST
SISINISISI S01 E07- MTAZAMO WA FURSA ZA KUSOMA NCHINI TAIWAN
Story na Bienvenu kutoka Burundi kuhusiana na fursa mbalimbali za kusoma nchini Taiwan. Ndani ya podcast hii tumechambua maswala na experience ya maisha ya Taiwan, huku Bien akiwasilisha uzoefu wake kwenye kazi alizowahi kuzifanya hapo awali kwenye mashirikika makubwa alivyokuwa Burundi
2025-05-24
49 min
SISINISISI PODCAST
SISINISISI S01EP06 - MAISHA YA TAIWAN, KAZI ZA PARTTIME KWA MWANAFUNZI
Interview hii imefanyika kati ya Yuba na Dauphin ambae ni mwanafunzi kutoka Burundi. Ameelezea experience yake tangu afike Taiwan na mambo mengi ambae amepitia kwenye safari yake ya maisha nchini Taiwan.
2025-05-10
50 min
SISINISISI PODCAST
SISINISISI S01EP05 - NINI KINAPELEKEA VIJANA WANAOISHI NJE YA NCHI AMA DIASPORA KUWA MACMUGA?
MacMuga ni Jina lilitumiwa na msanii wa Bongo Flava almaarufu kama King Kiba " Alikiba" kwenye wimbo uitwao MacMuga lengo la wimbo huo ulikua ni kutoa funzo kwa Vijana wanaotafuta maisha nje ya nchi, pindi wanapofanikiwa na kutojisahau kwa kuendekeza starehe na matumizi mabaya ya kile walichokichuma bila kuwekeza hasa nyumbani walikutoka.
2025-05-03
1h 17
SISINISISI PODCAST
SISINISISI S01EP04 -TAMADUNI ZA KIAFRICA NA ASIA NI ZIPI?
Katika episode hii, tunajadili baadhi ya tamaduni za Taiwan na Tanzania. Mgeni wetu, Jane ambaye ni Mtaiwan, anashiriki nasi kwa kuelezea maoni na uelewa wake kuhusu Afrika na Watanzania. Karibu ufurahie mazungumzo yetu ya kuvutia.
2025-04-26
26 min
SISINISISI PODCAST
SISINISISI S01EP03 - TOFAUTI YA MAHUSIANO YA MAPENZI KATI YA TANZANIA NA TAIWAN
🎙️ SISINISISI - Episode 03:Leo tunazungumzia mapenzi na mahusiano kati ya Taiwan na Tanzania ❤️Mpanga the Road na Yuba the Bad Man wanachambua tofauti, changamoto, na vichekesho vinavyotokea kwenye mapenzi ya pande hizi mbili.Usikose burudani, ukweli na ushauri wa mapenzi kutoka kwa SISINISISI ! 😄#Sisinisisi #MapenziTaiwanNaTanzania #SwahiliPodcast
2025-04-19
1h 03
SISINISISI PODCAST
SISINISISI S01EP02 - KAZI ZA TAIWAN KWA INTERNATIONAL STUDENTS, CHANGAMOTO VS EXPERIENCE
Katika episode hii ya pili, Mpanga the Road na Yuba the Bad Man wanaingia deep kwenye mada ya maisha ya kazi kwa vijana wa Kiafrika wanaoishi Taiwan. Je, ni rahisi kupata kazi? Changamoto zipi zinawakumba? Na vipi kuhusu uzoefu wao binafsi kazini – kuanzia viwandani hadi kwenye ofisi?
2025-04-13
1h 28
SISINISISI PODCAST
SISINISISI S01EP01- TOFAUTI KATI YA MAISHA YA NJE(TAIWAN) NA TANZANIA
YUBA the BadMan na Mpanga the Road wanajadili maisha ya Taiwan katika vipindi tofauti na kuyalinganisha na maisha ya Tanzania. Podcast hii imejaa burudani, ikiwakilisha simulizi zenye hisia na hadithi zenye mvuto wa kipekee.
2025-04-05
1h 02
TEN OVER TEN PODCAST
EP10 TENOVERTEN- Mafanikio ya Kiroho na Kiakili- Authentic Swahilians
Episode 10: Mafanikio ya Kiroho na Kiakili: Je, Maendeleo ni ya Kiuchumi Pekee? Katika kipindi hiki cha TEN OVER TEN Podcast, tunazama katika mjadala wa kipekee unaozungumzia mafanikio yanayozidi mipaka ya kiuchumi. Je, kweli maendeleo yanapimwa tu kwa pesa na mali? Jackson na mgeni wake Kefa Victor wanajadili umuhimu wa mafanikio ya kiroho na kiakili kwa maisha yenye utulivu na maana. Kwa Nini Usikilize? Sehemu ya Kwanza: Fahamu jinsi utulivu wa kiroho unavyochangia afya ya kiakili na hata kusaidia kufanya maamuzi bora ya kifedha. Sehemu ya Pili: Pata mbinu za kujenga mafanikio ya kiakili kupitia...
2024-12-23
1h 07
TEN OVER TEN PODCAST
EP09 TENOVERTEN- Kujenga Nidhamu na Maadili Imara: Msingi wa Ukuaji- Authentic Swahilians
Katika episode hii ya 9 Jackson na Kefa wanachambua umuhimu wa nidhamu, wakitumia mifano halisi kama Cristiano Ronaldo, ambaye nidhamu yake ya hali ya juu kwenye mazoezi na maisha ilimfikisha kilele cha mafanikio ya kimataifa. Wanashiriki pia mbinu madhubuti za kujenga nidhamu, kama kuweka malengo wazi, kujifunza kusema hapana kwa vishawishi, na kufuatilia maendeleo yako kwa ukaribu. Mambo Muhimu Utakayojifunza: Nidhamu ni injini ya maisha na ufunguo wa kufanikisha ndoto zako. Maadili hufanikisha uaminifu, ambao ni muhimu kwa mafanikio ya kudumu. Mbinu za vitendo za kujenga nidhamu na kudumisha maadili katika mazingira magumu.
2024-12-16
1h 00
TEN OVER TEN PODCAST
EP08 TENOVERTEN-"Rafiki au Adui? Watu Wanaokuzunguka na Ukuaji Wako"-Authentic Swahilians
Katika episode hii ya 08 Jackson na Kefa Victor wanazungumzia jukumu muhimu la watu wanaokuzunguka katika safari yako ya mafanikio. Wanajadili jinsi ya kuchagua marafiki kwa busara ili kukuza uhusiano wenye afya na unaosaidia ukuaji wako wa binafsi na kitaaluma.
2024-12-09
1h 12
TEN OVER TEN PODCAST
EP07 TENOVERTEN-Ubunifu na Kujiajiri: Fursa za Ukuaji Katika Ulimwengu wa Kisasa-Authentic Swahilians
Katika episode hii ya saba cha TEN OVER TEN Podcast, tunazungumzia mada ya kuchochea fikra na vitendo: Ubunifu na Kujiajiri. Katika ulimwengu unaobadilika kwa kasi, ubunifu ni silaha ya kufanikisha ndoto na kutengeneza nafasi mpya za ajira. Tukiongozwa na Jackson na Kefa Victor, Pamoja na mgeni Mr Saad tunachambua kwa kina: Umuhimu wa ubunifu katika soko la kisasa la kazi na biashara. Fursa zilizopo kwa wale wanaotaka kujiajiri na jinsi ya kuzitumia. Changamoto zinazowakumba vijana na mbinu za kuzikabili. Jinsi teknolojia inavyoweza kuwa chombo kikuu cha ubunifu na ajira. Njia za kukuza biashara za kibunifu...
2024-12-02
1h 41
TEN OVER TEN PODCAST
EP06 TENOVERTEN-Kujifunza Kutoka kwa Changamoto: Kutokata Tamaa- Authentic Swahilians
Katika episode hii ya sita, Jackson na Kefa wanajadili umuhimu wa changamoto katika maisha na jinsi ya kuzigeuza kuwa fursa za ukuaji. Wanatoa mifano hai, kama safari za Nelson Mandela, J.K. Rowling, na Elon Musk, zikionyesha jinsi changamoto zinavyoweza kukuimarisha kiakili, kimaadili, na hata kufanikisha ndoto zako. Kwa mazungumzo yenye maarifa na hamasa, utajifunza mbinu za kushinda changamoto kwa ubunifu, kuendelea mbele, na kutumia uzoefu wako kuhamasisha wengine.
2024-11-25
1h 03
TEN OVER TEN PODCAST
EP05 TENOVERTEN -Kubadilisha Makazi au Nchi – Je, Kunaweza Kuleta Maendeleo Binafsi?- Authentic Swahilians
Katika episode hii ya 5 tunajadili mada inayogusa maisha ya wengi: Kubadilisha Makazi au Nchi – Je, Kunaweza Kuleta Maendeleo Binafsi? Jackson Lusagalika na Kefa Victor wanaangazia faida, changamoto, na mbinu za kufanikiwa unapochukua hatua ya kuhamia nchi au makazi mapya. Tutashuhudia mifano hai ya watu maarufu kama Elon Musk, Lupita Nyong’o, na Chimamanda Ngozi Adichie, ambao walifanikiwa kutumia fursa za kubadilisha nchi kuendeleza ndoto zao. Pia, changamoto kama utambulisho wa kitamaduni, umbali na familia, na changamoto za kisheria zinajadiliwa kwa kina.
2024-11-18
57 min
TEN OVER TEN PODCAST
EP04 TENOVERTEN-Mahusiano ya Mapenzi na Maendeleo ya Kibinafsi-Authentic Swahilians
Katika episode hii, Jackson na Kefa wanazungumzia jinsi mahusiano ya mapenzi yanavyoweza kuchangia ama kudhoofisha maendeleo binafsi. Wanachambua faida za kuwa na mahusiano yenye afya kama msaada wa kisaikolojia na utulivu, huku wakionya juu ya athari za mahusiano yenye migogoro kwa malengo na nidhamu binafsi. Pia wanajadili umuhimu wa kuweka uwiano kati ya mapenzi na malengo ya kibinafsi na kujua wakati wa kuachana na mahusiano yenye sumu ili kuweka mbele afya ya kiakili na mafanikio binafsi
2024-11-11
1h 04
TEN OVER TEN PODCAST
EP03 TENOVERTEN-Kufanikisha Mafanikio: Tofauti ya Mafanikio Kati ya Mtu na Mtu-Authentic Swahilians
Katika Episode hii ya tatu TEN OVER TEN Podcast, tunachambua mada ya "Kufanikisha Mafanikio" na tofauti zake kati ya watu. Tunaanza kwa kuuliza, mafanikio yanamaanisha nini kwako binafsi? Na ni vigezo gani hutumika kuamua kama mtu amefanikiwa? Tunalenga kuelewa kama juhudi binafsi zinatosha au msaada wa watu wengine pia ni muhimu katika safari ya mafanikio. Tunaangazia zaidi tofauti za mafanikio kati ya mtu mmoja na mwingine, na iwapo mali na pesa ndizo kigezo pekee cha mafanikio. Pia tunagusia dhana za mafanikio ya kiroho na kiakili, na jinsi furaha ya ndani inavyoweza kuwa kipimo muhimu...
2024-11-04
47 min
TEN OVER TEN PODCAST
EP02 TENOVERTEN-Njia za Kutimiza Ndoto:Mipango na Mikakati - Authentic Swahilians
Katika Episode hii ya 02 TEN OVER TEN Podcast, tunazungumzia "Njia za Kutimiza Ndoto" na jinsi unavyoweza kupanga na kutekeleza mikakati bora ili kufikia malengo yako. Tutajadili mambo muhimu ya kuzingatia unapopanga ndoto zako, mikakati bora ya utekelezaji, na jinsi ya kuweka vipaumbele vyako. Pia, tunachambua vikwazo vikubwa vinavyoweza kukwamisha safari yako na mbinu za kushinda hofu ya kushindwa. Kwa kutumia mifano halisi, tunazungumzia umuhimu wa kuwa na mshauri au mentor, kugawa muda vizuri kati ya ndoto na majukumu mengine, na jinsi kushirikisha watu wengine kwenye mipango yako kunavyoweza kusaidia kufanikisha ndoto zako. Mwisho, tunagusia...
2024-10-28
35 min
TEN OVER TEN PODCAST
EP01 TENOVERTEN-Changamoto za Kijamii Katika Safari ya Ukuaji -Authentic Swahilians
TEN OVER TEN ni podcast yenye nguvu inayojikita katika maendeleo binafsi, fikra muhimu, na safari ya kufikia ubora. Imezalishwa na Authentic Swahilians na inaendeshwa na Jackson Lusagalika pamoja na msimamizi mwenza Kefa Victor. Wanaendesha mijadala ya kina, wakitoa mikakati ya kujiboresha, kufanikisha malengo, na kufanya maamuzi yenye kufikirika. Kila kipindi kinachambua mada za vitendo—kutoka kubadili mitazamo na kuweka malengo, hadi kutatua changamoto na kufanikisha mafanikio ya muda mrefu. Ikiwa unatafuta motisha, mitazamo mipya, au ushauri wa maana, TEN OVER TEN inaleta mazungumzo yenye nguvu yanayokusudia kukuinua kiakili na kufungua uwezo wako. Jiunge nasi katika safari ya ku...
2024-10-20
1h 25