Look for any podcast host, guest or anyone
Showing episodes and shows of

Mamlaka Ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)

Shows

TCRA TanzaniaTCRA TanzaniaMawasiliano ni Fursa: Gari la Mtambo (Mobile Monitoring Radio Frequency Station)Ungana nasi kufahamu juu ya kazi ya gari la mtambo wa usimamizi wa masafa kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).Unaweza kufuatilia kipindi cha Mawasiliano ni Fursa kupitia chaneli ya YouTube ya TCRA ili kufahamu kwa kina kuhusu majukumu ya gari hilo katika usimamizi wa huduma za mawasiliano nchini.TCRA inaendelea kutumia teknolojia na mifumo mbalimbali kusimamia sekta ya mawasiliano katika kuhakikisha ubora , usalama na upatikanaji wa huduma za mawasiliano.Kwa maoni na mapendekezo, tafadhali wasiliana nasi kupitia 0800008272 au tuandikie dawatilahuduma@tcra.go.tz #NiRahisiSana!2025-07-1715 minTCRA TanzaniaTCRA TanzaniaMatumizi ya Akili Unde (Artificial Intelligence) Katika Zama za KidijitiFahamu Matumizi ya Akili Unde (AI) Katika Zama za Kidijiti” kupitia ufafanuzi uliotolewa na Mtaalamu wa Masuala ya Akili Unde (Artificial Intelligence - AI) na Mwanzilishi Mkuu wa Mfumo wa AI wa Ghala Bw. Kalebu Gwalugano katika mahojiano aliyofanya na TCRAKwa maoni na mapendekezo, tafadhali wasiliana nasi kupitia 0800008272 au tuandikie dawatilahuduma@tcra.go.tz #NiRahisiSana!2025-06-3015 minTCRA TanzaniaTCRA TanzaniaDondoo za Kutambua Taarifa Feki MtandaoniTCRA imepata nafasi ya kujadiliana na Nuzulack Dausen, ambaye ni mwandishi wa habari mwenye tuzo nyingi kutoka Tanzania na Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Nukta Africa na Nukta Habari, akibobea katika ripoti za biashara, takwimu, na teknolojia. Yeye pia ni Mwandishi wa Thomson Reuters nchini Tanzania na mhadhiri wa Uandishi wa Habari za Takwimu na Fedha katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), ambapo alipata Shahada ya Uzamili ya Mawasiliano ya Umma. Hapa tutafahamu namna ya kutambua taarifa feki, vyanzo vyake, na namna ya kuthibitisha taarifa na vyanzo vyake. Katika kipindi hiki, tutazungumza pia kuhusu namna y...2025-06-0919 minTCRA TanzaniaTCRA TanzaniaUidhinishwaji wa Vifaa vya Mawasiliano ya KielektronikiTCRA huidhinisha vifaa vya Mawasiliano ya Kielektroniki kwa mujibu wa Sheria  Kifungu Na. 83 (1) na (2)  cha Sheria ya Mawasiliano ya Kieletroniki na Posta ya Mwaka 2010. Uidhinishwaji huo ni utaratibu maalum wa kuhakikisha kwamba Vifaa vya Mawasiliano ya Kielektroniki vinakidhi matakwa, mahitaji na viwango vya kitaifa na kimataifa kabla ya kuruhusu vifaa hivyo kuingia sokoni. Ungana nasi kufahamu zaidi kuhusu utaratibu, umuhimu na mlengwa wa utaratibu huu wa kuidhinisha vifaa vya mawasiliano ya kielektroniki.Kwa maoni na mapendekezo, tafadhali wasiliana nasi kupitia 0800008272 au tuandikie dawatilahuduma@tcra.go.tz #NiRahisiSana!2025-05-2613 minTCRA TanzaniaTCRA TanzaniaUsimamizi wa Huduma za Posta Tanzania (Sehemu ya Kwanza)TCRA inahakikisha uwapo wa huduma za posta zenye kuaminika, usalama, ufanisi na bei nafuu ndani ya Jamhuri ya Tanzania.Ungana nasi katika kipindi hiki kufahamu utaratibu na kanuni za utoaji wa huduma katika sekta ndogo ya Posta nchini Tanzania.Kwa maoni na mapendekezo, tafadhali wasiliana nasi kupitia 0800008272 au tuandikie dawatilahuduma@tcra.go.tz #NiRahisiSana!2025-05-2613 minTCRA TanzaniaTCRA TanzaniaUsimamizi wa Huduma za Posta Tanzania (Sehemu ya Pili)Katika sehemu ya pili ya kipindi hiki cha huduma za posta, TCRA inatoa elimu kuhusu haki na wajibu wa mtoa huduma na mtumiaji wa huduma za posta nchini.  Kipindi hiki hujadili pia anuani makazi (post codes) zinatotumika kutambulisha maeneo mbalimbali nchini Tanzania pamoja na matumizi yake katika huduma za mawasiliano ya posta.Kwa maoni na mapendekezo, tafadhali wasiliana nasi kupitia 0800008272 au tuandikie dawatilahuduma@tcra.go.tz #NiRahisiSana!2025-05-2612 minTCRA TanzaniaTCRA TanzaniaTCRA Zanzibar: Majukumu ya Mamlaka ya Mawasiliano, Ofisi ya ZanzibarSheria Na. 12 ya mwaka 2003 iliyoianzisha TCRA inaipa Mamlaka wajibu katika majukumu mbalimbali ikiwemo; kukuza ushindani bora na uchumi wenye tija; kulinda maslahi ya watumiaji; kulinda mitaji ya Watoa Huduma wenye ufanisi; kukuza upatikanaji wa huduma zinazodhibitiwa kwa watumiaji wote wakiwamo wenye kipato kidogo, walioko vijijini na watumiaji walio na walioko katika mazingira magumu; pamoja na kuimarisha Elimu kwa Umma, uelewa na ufahamu  wa huduma zinazosimamiwa na TCRA.Meneja wa TCRA, Ofisi ya Zanzibar anatueleza utekelezaji wa majukumu haya kwa kina katika ofisi za TCRA.Kwa maoni na mapendekezo, tafadhali wasiliana nasi kupitia 0800008272 au tuandikie dawatilahuduma@t...2025-05-0515 minTCRA TanzaniaTCRA TanzaniaTaarifa ya Sekta ya Mawasiliano: Januari - Machi, 2025Karibu katika wasaa wa kusikiliza ripoti hii inayowasilisha takwimu za sekta ya mawasiliano za robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2024/2025. Kwa ujumla, ripoti inatoa takwimu za mawasiliano ya simu, pesa mtandao kupitia simu za mkononi, intaneti, utangazaji, posta na usafirishaji wa vifurushi na vipeto. Takwimu hizi zimeandaliwa kwa kuzingatia viwango vya Shirika la Umoja wa Mawasiliano Duniani (ITU) vya kukusanya na kuandaa takwimu za huduma ya mawasiliano/TEHAMA. Kwa maoni na mapendekezo, tafadhali wasiliana nasi kupitia 0800008272 au tuandikie dawatilahuduma@tcra.go.tz #NiRahisiSana!2025-05-0215 minTCRA TanzaniaTCRA TanzaniaWasichana katika TEHAMA, 2025: Mageuzi Jumuishi ya KidijitiSiku ya Kimataifa ya Wasichana katika TEHAMA (International Girls in ICT Day) huadhimishwa kila Alhamisi ya nne ya mwezi Aprili kila mwaka. Hii inafuatia makubaliano ya nchi wanachama wa Shirika la Mawasiliano Duniani (ITU),  kuhimiza wasichana kupenda kusoma masomo ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati, kwa kifupisho cha kiingereza –STEM, yaani Science, Technology, Engineering and Mathematics. Nchi wanachama wa ITU pia zilikubaliana kuhamasisha Wasichana na Wanawake kushiriki kwenye kazi za taaluma ya STEM. TCRA, kama mwanachama na mjumbe wa baraza la utendaji la ITU, inaendeleza jitihada na huratibu maadhimisho haya kila mwaka. Hii ni  namna mojawapo ya ya ku...2025-05-0215 minTCRA TanzaniaTCRA TanzaniaJamii Yetu: Zanzibar - Mawasiliano na Maendeleo ya KilimoMawasiliano huleta faida mbalimbali katika maisha ya kila siku. Kipindi hiki kinaelezea yaliyojiri katika kilimo cha karafuu na namna mawasiliano huchochea kilimo hiki katika kisiwa cha Zanzibar.Kwa maoni na mapendekezo, tafadhali wasiliana nasi kupitia 0800008272 au tuandikie dawatilahuduma@tcra.go.tz #NiRahisiSana!2025-03-0320 minMsasaonlineMsasaonlineCLOUDS TV NA REDIO ZAFUNGIWA KWA SIKU 7.MAMLAKA ya Mwasiliano Tanzania (TCRA) imeagiza Clouds TV na Redio kusitisha matangazo yao kwa muda wa siku saba kuanzia kesho Ijumaa 28 Agosti hadi 3 Septemba 2020 kwa kosa la kukiuka kanuni za utangazaji na kanuni ndogo za utangazaji za uchaguzi. Pia, mamlaka hiyo imevitaka Clouds TV na Redio kuomba radhi siku nzima ya leo Alhamisi tarehe 27 Agosti 2020 kwa kosa hilo. Akizungumza na waandishi wa habari makamo makuu ya mamlaka hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, James Kilaba amesema, adhabu hiyo inatokana na kukiuka kanuni mbalimbali za utangazaji na kanuni ndogo za wakati wa uchahuzi za mwaka 2015. Kilaba amesema, Clouds TV na Redio walikiuka...2020-08-2902 min