podcast
details
.com
Print
Share
Look for any podcast host, guest or anyone
Search
Showing episodes and shows of
MezaHuru
Shows
Meza Huru
Mezani na MANDOJO NA DOMOKAYA #18
Usichofahamu ni majina yao halisi Joseph Francis Michael Ong'oso na Precious Juma Mkoma maarufu kama Man'Dojo na Domokaya. Wanamuziki mashuhuri sana wa kizazi cha jana na leo. nani asiyepende kusikia sauti nzuri na za kuvutia zikisindikizwa na Guitar lao(wenyewe wanaliita Banjo)? Nani asiyetambua uwezo wa miamba hawa wa muziki katika kuweka viitikio na vionjo makini katika nyimbo mbalimbali za Muziki wa Kibongo? Hawa ni marafiki waliogeuka ndugu, wenyewe wanadai wamepitia mpaka kuvaa nguo sare 😁 Meza Huru imekaa nao na kupata simulizi ya maisha yao ya muziki na amini kwamba, inavutia sana. Jumuika nasi mezani kuwasililiza 😊, Karibu #MezaniNaMandojoNaDomokaya #MezaHuru
2022-11-25
2h 30
Meza Huru
Mezani na KIBACHA Part II
Sehemu ya pili ya maongezi yetu na KBC, ambaye wengi wanamfahamu kama Kibacha Huyu ni mojawapo wa mwamba muhimu wa Hip Hop ya Tanzania. Unaambiwa zama zake, Kipaza kilimuogopa kama ukoma, Rafiki wa mashairi na mchenguaji mashuhuri. Gwiji wa mtindo huru na Battle Emcee haswaaa. Kibacha ni miongoni mwa waanzilishi wa Kundi kongwe na mahiri la KWANZA UNIT. Ametupa heshima kubwa ya kukaa nasi na kutupa historia ya muziki wake tangu miaka ya 80 mpaka hapa tulipo. Mwamba huyu hapa 😊 #MezaniNaKBC #MezaHuru
2022-11-22
1h 41
Meza Huru
Mezani na KIBACHA Part I
Anaitwa KBC, wengi wanamfahamu kama Kibacha Huyu ni mojawapo wa mwamba muhimu wa Hip Hop ya Tanzania. Unaambiwa zama zake, Kipaza kilimuogopa kama ukoma, Rafiki wa mashairi na mchenguaji mashuhuri. Gwiji wa mtindo huru na Battle Emcee haswaaa. Kibacha ni miongoni mwa waanzilishi wa Kundi kongwe na mahiri la KWANZA UNIT. Ametupa heshima kubwa ya kukaa nasi na kutupa historia ya muziki wake tangu miaka ya 80 mpaka hapa tulipo. Jumuika nasi mezani kumsikiliza Mwamba huyu hapa 😊 #MezaniNaKBC #MezaHuru
2022-11-18
1h 39
Meza Huru
Mezani na DOLO #15
Anaitwa DOLOMOI FRANCIS, kwa jina maarufu anafahamika kama DOLO. Ni moja ya waasisi wa kundi la Wachuja Nafaka na Wanaume TMK. Kutoka maeneo ya TEMEKE. Tumepata bahati ya kukaa naye mezani na ametupitisha kwenye safari yake ya muziki. Kuanzia akiwa hajawa Dolo, mpaka hivi sasa akiwa bado anapeperusha vyema bendera ya TMK. #MezaniNaDolo #MezaHuru
2022-11-11
2h 09
Meza Huru
Mezani na KR MULLAH #14
KR Mullah ,miongoni mwa waasisi wa GWM (Gangstaz With Matatizo), Wachuja Nafaka, TMK Wanaume family Mwamba huyu kutokea Temeke Dar es Salaam amefanya makubwa sana katika muziki wetu kabla haujaanza kuwa rasmi Amefanya kazi na wakongwe kama Boniluv, Master Jay na P Funk. Ametupatia heshima kubwa ya kutupa simulizi yake tangu akiwa kijana mdogo katika muziki mpaka sasa bado anawakilisha Temeke popote pale alipo Muite KR Mullah Jibaba Muziki Mkubwa CD Mia Saba Njoo kichwa kichwa akupe za uso saba. #MezaniNaKakaRashidi #MezaHuru
2022-11-04
1h 30
Meza Huru
Mezani na RAS INNO #13
Ras Innocent Nganyagwa ni miongoni mwa wanamuziki nguli katika kizazi cha tatu cha muziki wa Reggae kutoka Tanzania. Muziki wa Reggae Afrika ulianza kushamiri baada ya Uhuru wa Zimbabwe mwaka 1980, Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizokuwa za mwanzo kupata mapokeo ya muziki huo. Tumezungumza na Ras Inno kuhusu imani ya RastaFari, muziki wa Reggae Ras Innocent Richard Nganyagwa ni shule haswa, Ana ufahamu mkubwa sana wa maisha ya asili ya mwafrika na anaamini kila mtu mweusi ni Rastafarian. Ras Inno ni mtetezi wa haki za binadamu na za wasanii pia, Jumuika n...
2022-10-28
2h 06
Meza Huru
Mezani na CAROLA KINASHA #12
Carola Kinasha, ukimuona huwezi kuamini ana miongo sita duniani. First lady wa Bene Bene na baadaye Shada. Msomi wa chuo kikuu aliyechagua kufanya muziki kama kazi. Mwanaharakati wa mwanzo kabisa wa stahiki na haki za utunzi, na moja walioupeleka mbali sana muziki wa asili ya Afrika. Ni mcheshi na mwenye maarifa mengi sana kuhusu maisha na safari ya muziki wetu tangu miaka ya themanini mpaka leo hii. Unajua kisa chake na Remmy Ongala kilichozaa kibao maarufu cha Karola? Unajua nini maana ya segese? Unajua kwamba yeye ni mtu aliyekuwa nyuma ya chorus nzuri...
2022-10-21
2h 17
Meza Huru
Mezani na MIKE TEE #11
Wengi wanamjua kwa jina la Mnyalu, Mike Tee, The Dangerous Emcee ila jina lake kamili ni Mike Francis Mwakatundu. Mike Tee alianza kuimba mwanzoni mwa miaka ya 90, akiimba kwaya kanisani na taratibu akaanza kujifunza kuandika na kuimba mistari kupitia mashairi ya gazetini baada ya kukutana na Ntwa mmoja wa waanzilishi wa WWA (Wagumu Weusi Asilia). Amefanya kazi na watayarishaji kama P Funk na Master Jay, amefanya hits na wasanii kama Juma Nature, Q Chief, Mad Ice na Komando Jide Unajua kuhusu ugomvi wa Mr. Nice na Dudu Baya? Mike Tee amenyoosha taarifa. Sitaki k...
2022-10-14
1h 58
Meza Huru
Mezani na UNCLE JOHN KITIME #10
Mzee Kitime ama Ango "Uncle" Kitime kama mwenyewe anavyojitanabaisha kwenye mitandao. Ni mwanamuziki nguli wa Muziki wa Dansi kutoka Kilimanjaro Band maarufu kama "Wana Njenje", mmoja wa wanakamati ya kutetea muziki wa dansi na tasnia ya muziki kwa ujumla, Mtangazaji wa Radio, Muigizaji wa Filamu, Mchekeshaji na Mtunza historia ya Music wa Tanzania. Tumekaa naye na kupata historia ya muziki wake na harakati zake tangu mwaka 1967 hadi leo akiwa na JFK BAND. Jumuika nasi mezani tumsikilize Gwiji huyu wa Tasnia yetu, Karibu. #MezaniNaJOHNKITIME #MezaHuru Anchor - https://anchor.fm/meza-huru Go...
2022-10-07
2h 17
Meza Huru
Mezani na MASTER JAY Part II
Sehemu ya pili ya maongezi na Master Jay. Kama hujasikiliza nyimbo alizotengeneza (naamini ni vigumu), utakuwa umemuona kwenye mashindano ya kusaka vipaji Joachim Marunda Kimaryo ni Gwiji kabisa katika tasnia ya muziki wetu Amehusika katika Hip Hop, Bongofleva, Dansi mpaka nyimbo za Dini 😁 Tumepata nafasi ya kuzungumza naye na ametupa simulizi ambazo zinaweza kutumika kama chanzo rasmi cha historia za muziki wetu kuanzia mwanzo mpaka tulipo. Jumuika nasi mezani, tusikilize PART II ya MTABE huyu wa sanaa 😉 Karibu. #MezaniNaMasterJay #MezaHuru Anchor - https://anchor.fm/meza-h...
2022-09-30
58 min
Meza Huru
Mezani na MASTER JAY Part I
Nani asiyemfahamu Master Jay? Kama hujasikiliza nyimbo alizotengeneza (naamini ni vigumu), utakuwa umemuona kwenye mashindano ya kusaka vipaji Joachim Marunda Kimaryo ni Gwiji kabisa katika tasnia ya muziki wetu Amehusika katika Hip Hop, Bongofleva, Dansi mpaka nyimbo za Dini 😁 Tumepata nafasi ya kuzungumza naye na ametupa simulizi ambazo zinaweza kutumika kama chanzo rasmi cha historia za muziki wetu kuanzia mwanzo mpaka tulipo. Jumuika nasi mezani, tusikilize PART I ya MTABE huyu wa sanaa 😉 Karibu. #MezaniNaMasterJay #MezaHuru Anchor - https://anchor.fm/meza-huru Google podcast...
2022-09-23
1h 26
Meza Huru
Mezani na BONILUV #TheGodfather Part II
Sehemu ya pili na Kaka Boniphace Kilosa a.k.a #Boniluv. Kati ya wale magwiji wawili wanaotajwa sana, huyu ni Kaka yao na hatajwi sana pengine kwa makusudi ama bahati mbaya na hilo halijatuzuia kufanya naye mazungumzo na kumpatia maua yake. Boniluv ni Baba, Kaka, Rafiki na mwanafamilia. Ni mtu wa Muziki haswa. Ni mtu wa old school jams, akianza story za 80's hatumshiki!! Amefanya kazi na Ma-Pioneer wote wa muziki wa kizazi kipya. Amekuwepo kabla ya Bongo Fleva hivyo anastahili HESHIMA ya kuwa #TheGodFather wa muziki wa Bongofleva Ametupa heshima kubwa Sana na historia ya safari yake ya mu...
2022-09-16
1h 19
Meza Huru
Mezani na BONILUV #TheGodfather Part I
Boniphace Kilosa a.k.a #Boniluv Kati ya wale magwiji wawili wanaotajwa sana, huyu ni Kaka yao na hatajwi sana pengine kwa makusudi ama bahati mbaya na hilo halijatuzuia kufanya naye mazungumzo na kumpatia maua yake. Boniluv ni Baba, Kaka, Rafiki na mwanafamilia. Ni mtu wa Muziki haswa. Ni mtu wa old school jams, akianza story za 80's hatumshiki!! Amefanya kazi na Ma-Pioneer wote wa muziki wa kizazi kipya. Amekuwepo kabla ya Bongo Fleva hivyo anastahili HESHIMA ya kuwa #TheGodFather wa muziki wa Bongofleva Ametupa heshima kubwa Sana na historia ya safari yake ya muziki na maisha tangu miaka hi...
2022-09-09
1h 17
Meza Huru
Mezani na DUNGA #05
#MezaniNaDunga #MezaHuru #Dunga Wengi wetu tunamfahamu kwa jina la Dunga ama Mandugu. Jina lake kamili ni Ambrose Akula Akwabi. Huyu ni mtu muhimu sana katika muziki wetu. Amekuwepo tangu enzi tunajitafuta. Dunga na kaka yake (Shakii) wanaunda Mandugu Digital. Amefanya kazi nyingi sana mashuhuri na nyingine unaweza usiamini anahusika nazo. Jumuika nasi mezani, tumsikilize Mwamba Huyu 😉 Karibu. Anchor - https://anchor.fm/meza-huru google podcast - https://podcasts.google.com/feed/aHR0... ...
2022-09-02
1h 55
Meza Huru
Mezani na JORS BLESS #04
Johnson Sululu a.k.a Jorsbless ni sehemu ya kizazi bora cha utayarishaji na uandaaji wa midundo katika tasnia ya muziki Tanzania Amefanya kazi na wasanii kama Mapacha, Rama Dee, Nikki Wa Pili , Adili n.k Unakumbuka kuhusu ANTI-VIRUS Movement? Tumeligusia hili pia 😁 Amefanya kazi kama DJ katika kituo cha #TimesFm na baadae #AzamTV kama Sound Engineer Tumekaa na JORS na kupiga soga kuhusu maisha kuanzia mwanzo wa kazi zake hizi mpaka leo hii Unajua Mwaka 2008 Baba yake mzazi alimpatia kiasi cha shilingi Mili...
2022-08-26
1h 32
More Than 30 With Marc
Tz Census| Man Utd Win | East Africa Radio | SA Hiphop Scene | Ommy Dimpoz
Welcome to today's episode, for once i was #MkuuWaKaya for the Census, Man Utd win, MezaHuru the podcast the late Rodney Mutie Mengi & EA radio, as well as Ommy Dimpoz new album announcement & Mavins very new Bayanni.Enjoy it. Twitter link :https://twitter.com/babbiekabae/status/1558007401357496320?s=08
2022-08-24
29 min