podcast
details
.com
Print
Share
Look for any podcast host, guest or anyone
Search
Showing episodes and shows of
Nukta Habari
Shows
Nukta the Podcast
Wafahamu watu 10 tajiri zaidi duniani 2025
Ukuaji wa teknolojia umeendelea kuchochea ongezeko la utajiri duniani jambo ambalo limesababisha watu waliowekeza katika sekta hiyo kuendelea kujikusanyia ukwasi na kutawala orodha ya watu wenye ukwasi mwingi zaidi duniani.Orodha ya watu matajiri duniani ya mwaka 2025 inayotolewa na Jarida la Forbes la nchini Marekani inaonesha chanzo cha utajiri wa watu 10 matajiri zaidi ni uwekezaji katika teknolojia na biashara.Kwa mujibu Forbes duniani kuna zaidi ya mabilionea 2,700 wakiwa na jumla ya utajiri wa Dola Trilioni 14.2 za Marekani wakitokea katika sekta mbalimbali kama teknolojia, biashara, na huduma za kifedha na makala hii inaangazia watu 10 taji...
2025-03-24
10 min
Nukta the Podcast
HATARI INAYOUKABILI MTO NGERENGERE
Hujambo msikilizaji wa Nukta the Podcast, karibu katika mfululizo wa episode zetu maalumu zinazoangazia Usimamizi wa rasilimali maji pamoja na mazingira katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania. Katika sehemu hii ya tatu na ya mwisho tutamulika hatari inayoukabili Mto Ngerengere uliopo mkoani Morogoro kutokana na uchafuzi unaofanywa wa mto huo. Pia tutachambua hatua zilizochukuliwa na zinazotakiwa kuchukuliwa ili kuunusuru mto huo unaopita Morogoro mjini.
2024-10-22
21 min
Nukta the Podcast
VITA YA MAJI ILIVYOLETA AMANI NA MSHIKAMANO KATI YA WAFUGAJI NA WAKULIMA KILOSA
Katika episode hii tutaangazia jinsi tatizo la maji Ilivyowaunganisha wakulima na wafugaji Kilosa. Hapa utasikia simulizi ya wafugaji na wakulima waliokuwa maadui kutokana na mgogoro wa maji walivyogeuka marafiki baada ya kumfahamu adui wao wa kweli. Karibu twende nami mpaka mwisho wa episode hii.
2024-10-05
23 min
Nukta the Podcast
SCRAMBLE FOR WATER RESOURCES
This is the part of the three episodes that we have produced after visiting several districts in Morogoro region, eastern Tanzania meeting with farmers, livestock keepers, environmentalists, factory owners and government officials. In this first episode we will hear about how pastoralists fight for water resources in Eastern Tanzania due to the increase in demand of water amid ongoing decline of water levels in their localities, highly influenced by climate change. You are warmly welcome.
2024-09-30
19 min
Nukta the Podcast
Restoration of Lake Manyara Tilapia remains an uphill duty
Join Daniel Samson to explore in detail about endangered Manyara Tilapia in Lake Manyara. Stocks of Manyara tilapias have plummeted to alarmingly low levels in recent decades due to unsustainable fishing. The International Union for Conservation of Nature (IUCN) Red List of Threatened Species Report 2006 shows that the area of occurrence of the fish, which previously accounted for 73.6% of the total catch in the region, has shrunk from 5,000 km2 to 1800 km2 in recent decades. As a result, the fish is now listed as an endangered species by the IUCN because of driving forces, inc...
2024-05-20
10 min
Nukta the Podcast
From sunlight to harvest: How solar energy brings hopes to farmers in Iringa
For decades, farmers in Lupembe Lwa Senga village in Iringa region had relied on the traditional farming system for their livelihoods. Apart from using hand hoes, animal plows, they would wait for the rain to irrigate their crops. For small plots like gardens, they would use buckets or recently fuel-powered water pumps for irrigation. “We started irrigation farming as a group in1999, by that time we were using a fuel-powered pump with the cost of 200,000 for buying petrol to irrigate all five acres a day, it was terrible,” Gabriel Mmewa, farmer in Lupembe Lwa Se...
2024-03-17
07 min
Nukta the Podcast
UPUNGUFU WA WALIMU SHULE YA MSINGI UNAVYOATHIRI ELIMU TANZANIA
Wakati watahiniwa zaidi ya milioni moja wa elimu ya msingi Tanzania Bara wakiwa wanasubiri hatma yao, baada ya kumaliza mitihani yao jana Septemba 14, 2023, utoshelevu wa walimu katika ngazi hiyo muhimu ya elimu kwa shule za Serikali umeendelea kuwa kitendawili Kitabu cha hali ya uchumi cha mwaka 2022, kinabainisha kuwa mpaka Disemba mwaka 2022 kulikuwa na jumla ya wanafunzi milioni 10.8 katika shule za msingi za Serikali Tanzania, huku idadi ya walimu katika shule za Serikali ikiwa 173,276. Hii ni sawa na kusema idadi ya wanafunzi waliopo ni mara 62 zaidi ya idadi ya walimu na hivyo kwa wastani...
2023-09-30
09 min
Nukta the Podcast
Elimu ya Veta inavyowainua walemavu wa akili Tanzania
Awali, ilikuwa ni vigumu kushuhudia watu wanaozaliwa na ulemavu wakipata huduma muhimu wanazozihitaji kama elimu, afya, pamoja na kushirikiana na wanajamii wengine kuibua suluhu za matatizo yanayozikabili jamii zao. Hivi sasa zama hizo zimepita. Kutokana na hatua zilizochukuliwa na Serikali pamoja na wadau, ikiwemo kuielimisha jamii kutowabagua na kushirikiana na kundi hilo, kama binadamu wengine watu wenye ulemavu nao wanapata huduma wanazostahili. Miongoni mwao ni kijana Paulo Ngunyali, mhitimu wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) kilichopo Chang’ombe, Jijini Dar es Salaam. Pamoja kuwa mlemavu wa akili amehitimu fani ya uundaji wa mashine, na...
2023-09-15
08 min
Nukta the Podcast
MFAHAMU MBUNIFU WA MAJIKO YANAYOTUMIA MAWE TANZANIA
Nishati ya kupikia ni miongoni mwa mahitaji muhimu ya binadamu duniani kote, hiyo ndio huwezesha mapishi ya aina mbalimbali za vyakula tunavyokula ili kuimarisha afya na kuwezesha utendaji wa shughuli za kila siku. Watu wengi wanatambua gesi, mkaa, umeme, mafuta pamoja na kuni kama ndio vyanzo vya nishati ya kupikia kwa kuwa ndio ambavyo vinatumika kwa kiasi kikubwa kwa sasa huku jitihada nyingi zikielekezwa kuhamia kwenye matumizi ya nishati safi ya kupikia. Hata hivyo, jijini Dar es Salaam kuna ubunifu mpya wa nishati ya kupikia inayotumia mawe, ambapo inatajwa kupunguza kwa kiasi kikubwa gharama...
2023-09-08
07 min
Nukta the Podcast
JINSI MATAPELI WANAVYOTUMIA TAASISI YA MO FOUNDATION KUIBIA WATU
Kama wewe ni mtumiaji wa mtandao wa Facebook huenda umewahi kukutana na chapisho linalohusu fursa ya mikopo kutoka kwenye taasisi ya mfanyabiashara bilionea nchini Tanzania Mohamed Dewji Foundation Sehemu ya chapisho hilo lianasomeka ‘𝐉𝐈𝐏𝐀𝐓𝐈𝐄 𝐌𝐊𝐎𝐏𝐎 𝐊𝐔𝐓𝐎𝐊𝐀 𝐌𝐎𝐇𝐀𝐌𝐄𝐃 𝐃𝐄𝐖𝐉𝐈 𝐅𝐎𝐔𝐍𝐃𝐀𝐓𝐈𝐎𝐍 kwa maelekezo ya kupata vigezo na masharti njoo hwatspp kwa no👉🏿 0748923136’. Chapisho hilo pamoja na kuhamasisha watu kuomba mikopo wametaja kigezo cha kutoa kwanza kiasi cha hisa ya mkopo unaotaka kupewa kabla ya kupata mkopo wenyewe. Ufafanuzi zaidi wa taarifa hiyo unaonesha kama unahitaji kukopa Sh100,000 basi utalazimika kutoa kwanza hisa ya Sh22,000 ndipo upewe mkopo huo. Taarifa hiyo imesambaa katika mtandao wa Facebook kupitia akaunti zenye majina tofauti tofauti toka mwaka 2022 huku ikiwa imeambat...
2023-09-01
07 min
Nukta the Podcast
KWA NINI BANGI INALIMWA ZAIDI TANZANIA LICHA YA OPARESHENI KALI ZA DAWA ZA KULEVYA?
Mapema Agosti mwaka huu Serikali ya Tanzania ilitangaza kukamata magunia 131 ya bangi, kilo 120 za mbegu za bangi na kuteketeza jumla ya hekari 489 za mashamba ya bangi mkoani Morogoro, katika moja ya operesheni kubwa za kutokomeza dawa za kulevya iliyowahi kufanyika nchini. Katika operesheni hiyo Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Aretas Lyimo anasema wakulima hao wa bangi hufanya uharibifu mkubwa wa mazingira kwa kuchepusha maji pamoja na kukata misitu ili kufanya kilimo cha zao hilo haramu. Watu 18 walikamatwa katika operesheni hiyo iliyoshika mjadala katika vyombo vya habari n...
2023-08-25
09 min
Nukta the Podcast
Teknolojia ya vifuu vya nazi itakavyo waokoa wachimbaji na madhara ya zebaki
Huenda wachimbaji wadogo wa madini Tanzania wakaepukana na athari za afya pamoja na uchafuzi wa mazingira ikiwa wataasili matumizi ya bidhaa mpya ya kusafishia madini (Activated carbon) inayozalishwa nchini. Bidhaa hiyo inayotengenezwa kwa kutumia vifuu vya nazi itachochea uzalishaji wa madini na kuongeza mchango wa sekta hiyo kwenye pato la taifa kwa kuwa itapatikana kwa urahisi jambo litakaloongeza kasi katika shughuli za uchenjuaji huku mazingira na wachimbaji wakwa salama. Upatikanaji wa bidhaa hiyo mbadala wa zebaki katika shughuli za uchechuaji itakuwa mkombozi kwa wachimbaji pamoja na jamii ambayo inaweza kuathirika kwa kwa kuvuta h...
2023-08-18
07 min
Nukta the Podcast
Hizi ndio hifadhi tano kubwa za Taifa, Tanzania
Tanzania ni miongoni mwa mataifa ambayo yamebarikiwa vivutio vingi vya utalii ambavyo sio tu vinapendezesha nchi bali ni chanzo kizuri cha mapato hususani fedha za kigeni ambazo hutumika kwa shughuli za maendeleo. Tovuti ya runinga ya Tanzania Safari Channel ambayo hutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini, inabainisha kuwa Asilimia 40 ya ardhi ya Tanzania imetengwa kwa ajili ya uhifadhi. Hii inajumuisha hifadhi za Taifa 22, eneo la hifadhi ya Ngorongoro, mapori tengefu, hifadhi za misitu asilia na misitu ya kupandwa, maeneo ya kihistoria pamoja na hifadhi za bahari. Maeneo yote hayo ndio kitovu k...
2023-08-11
07 min
Nukta the Podcast
MVUVI MPAMBANAJI NDANI YA ZIWA VICTORIA
Ziwa Victoria ni moja ya maziwa makuu ya Afrika Mashariki. Ni ziwa ambalo lipo kwenye mstari wa ikweta na limezungukwa na nchi tatu zilizopo Afrika Mashariki yaani Tanzania, Kenya na Uganda. Ziwa hili ni chanzo cha Mto Nile wenye urefu wa kilomita 6,650 na urefu huo unaufanya kuwa mto mrefu zaidi duniani, Ziwa Victoria ndiyo ziwa kubwa zaidi barani Afrika na lina ukubwa wa kilomita za mraba 68,800 ambapo ni la pili duniani kwa ukubwa likitanguliwa na Ziwa Superior lililopo Amerika ya kaskazini, kwa ukubwa huu nchi za Rwanda na Burundi zinaweza kuwa visiwa ndani ya ziwa...
2023-03-21
06 min
Nukta the Podcast
ELIMU YA SAIKOLOJIA INAVYOWABEBA WATU WENYE UALBINO TANZANIA
Watu wenye ulemavu wa ngozi nchini Tanzania wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali unyanyapaa ikiwa miongoni, licha ya afua zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali kuelimisha watu wanaowazunguka, baadhi ya walemavu hushindwa kujumuika na wanajamii wengine kutokana na hofu au mitizamo ya kifikra waliyonayo wao wenyewe hata kama jamii ina mtizamo chanya juu yao. Abdushakur Mrisho ametuandalia makala yanayoonesha ni kwa namna gani elimu ya saikolojia inavyoweza kuwakomboa watu hawa na kuwafanya wajione kama watu wengine na kuchangamana na wanajamii wengine katika shughuli za kijamii.
2023-03-21
09 min
Nukta the Podcast
Ifahamu zahanati iliyoanzishwa kwa mkopo wa halmashauri
Ni Zahanati ya Afya ya Jamii iliyopo Kata ya Kipunguni jijini Dar es Salaam ambayo ni ya kwanza katika kata hiyo. Vijana nane wametumia mkopo Sh100 milioni wa Halmashauri ya Ilala kuianzisha ili kupunguza changamoto za afya jijini humo. Esau Ng'umbi anasimulia zaidi.
2022-10-01
08 min
Nukta the Podcast
Mradi wa umemejua unavyowafaidisha wanavijiji Tanzania
Ni mradi wa jiko linalotumia mionzi ya umemejua kupikia vyakula mbalimbali. jiko hilo la aina yake limebuniwa na Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam ili kupunguza matumizi ya kuni na mkaa.
2022-06-03
07 min
Nukta the Podcast
Wazazi wanavyopambana kuwapatia chakula wanafunzi shuleni Pangani
Salaaam msikilizaji wa NUKTA THE PODCAST karibu katika muendelezo wa makala zetu na leo tunasafiri hadi Wilayani pangani mkoani Tanga kumulika namna wazazi wanavyopambana kuwapatia chakula wanafunzi katika shule za sekondari, i mimi ni Suleman Omar Mwiru.
2022-04-22
06 min
Nukta the Podcast
Zaidi ya Watanzania 500,000 kukumbukwa na uhaba wa chakula
Wakati baadhi ya Watanzania wakila na kusaza kiasi cha kutupa chakula, ripoti mpya ya usalama wa chakula na lishe Tanzania inakadiria kuwa kuanzia Mei 2022 watu 592,000 watakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula kutokana na kushuka kwa uzalishaji wa mazao ya chakula katika baadhi ya maeneo nchini. Ripoti hiyo ya Tathmini ya Usalama wa Chakula na Lishe iliyotolewa Februari 2022 na Wizara ya Kilimo na Idara ya Udhibiti Maafa ya Ofisi ya Waziri Mkuu imeeleza kuwa hali hiyo ya uhaba mkubwa wa chakula itashudiwa kati ya mwezi Mei hadi Septemba mwaka huu. Nini sababu? Herimina Mkude anasimulia zaidi.
2022-03-25
03 min
Nukta the Podcast
“Show” ya kibabe iliyowakutanisha mastaa wa Afrika
‘Young, Famous & African’ au kwa kifupi unaweza kuita YFA, ni ‘reality show’ yaani imebeba uhalisia wa maisha ya wahusika. Natumaini katika pita pita zako kwenye mitandao ya kijamii, umeshakutana na jina hilo. Wahusika wake ni vijana nyota, maarufu na wenye ‘mishiko’ yao haswaa kutoka nchi mbalimbali Afrika. Ndani humo utakutana na ‘Dj’ maarufu kusini mwa Afrika, hapa namzungumzia Dj Naked, muimbaji Nadia, mtangazaji maarufu Afrika Kusini Andile, nyota wa muziki kutoka Nigeria 2baba na wengineo. Bila kuwasahau Zari na Diamond, ambao tunaweza sema wamesababisha Watanzania wengi kuitazama show hiyo.
2022-03-25
05 min
Nukta the Podcast
Jukumu la kutunza mazingira ni la kila mtu
Utunzaji wa mazingira yanayotuzunguka ni njia mojawapo ya kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi ikiwemo mafuriko na ongezeko la joto.
2022-03-25
01 min
Nukta the Podcast
Ukame ulivyowarudisha wafugaji kwenye umaskini Tanzania
Mwaka 2021 unavyoanza alikuwa ana matumaini lukuki kuwa ng’ombe wake aliokuwa nao wangechangia kwa kiwango kikubwa kumuongezea kipato na kumtoa katika umaskini. Miezi 11 baadaye ndoto ya Ndirana Ndirana Jijungu, mkazi wa Kijiji cha Mwamihanza wilayani Maswa mkoani Simiyu ilizimwa ghafla kwa kupoteza ng’ombe wanne kati ya sita baada ya kukosa malisho kutokana na ukame. Hata hivyo, ukame wa mwishoni wa mwaka 2021 umemfanya apoteze sehemu kubwa ya mali na kumrudisha kwenye umaskini. Tofauti na miaka mingine, mvua hizo zilichelewa kiasi cha kuathiri upatikanaji wa malisho na maji maeneo mengi wilayani Maswa, kama anavyosimulia Herimina Mkude.
2022-03-24
06 min
Nukta the Podcast
Mbinu zitakazosaidia kudhibiti taka za baharini
Kudhibiti uchafuzi wa bahari Serikali na wadau wanasema taasisi za utafiti na viwanda zinahitaji kufanya kazi kwa ushirikiano ikiwemo kuimarisha mifumo ya ulejerezaji taka. Pia kupiga marufuku kabisa matumizi ya chupa za plastiki na kutoa elimu kwa wananchi juu ya uhifadhi wa mazingira ya bahari kama anavyoripoti Suleman Mwiru.
2022-03-23
05 min
Nukta the Podcast
Gharama kubwa zinavyorudisha nyuma jitihada za kuokoa mazingira Wilaya ya Kibaha
Baada ya kubaini faida na urahisi wa kutumia nishati ya gesi kupikia, mwalimu wa moja ya shule za sekondari wilayani Kibaha aliamua kuchukua hatua. Alianza jitihada za kutumia gesi kuongeza ufanisi katika mapishi shuleni kwao na kupunguza kiasi cha kuni zinazotumika kupikia ili kuokoa mazingira. Hata hivyo, changamoto iliyobaki ni gharama kubwa za kupata nishati hiyo. Herimina Mkude anatujuza zaidi.
2022-03-22
05 min
Nukta the Podcast
Changamoto zinapokuletea fursa
Ni filamu ya "Fine Wine", inayomuhusu mwanadada Kaima anayepitia changamoto katika mahusiano. Licha ya uzuri na ‘usmati’ alionao binti huyu, mahusiano yake na kijana Tunji ni pasua kichwa kuliko hata majukumu yake ya kazi. Maisha ya Kaima yanabadilika siku ambayo wanakubaliana kukutana na Tunji katika mgahawa fulani, lakini kaka huyo anamwambia mpenziwe kuwa amsubiri kwani kuna jambo la ghafla limetokea.
2022-03-18
07 min
Nukta the Podcast
Taka za kielektroniki zinavyotafuna mazingira ya Tanzania
Hakuna mifumo mizuri ya kutupa taka za kielektroniki nchini Tanzania kama ilivyo kwenye nchi zilizoendelea hivyo suluhu kubwa iliyopo ni kuzitupa kama taka nyingine.
2022-03-14
04 min
Nukta the Podcast
The Last Royal Treasure: Filamu ya kuchangamsha wikiendi yako
Filamu ya ‘The Last Royal Treasure’, inahusu kundi moja la maharamia au kwa Kiingereza wanafahamika kama pirates. Meli yao imebeba watu ambao wana historia tofauti za kimaisha. Wengine walikuwa majenerali wa vita, watoto wa manahodha, huku wengine wakiwa ni wezi walioshindikana.
2022-03-11
06 min
Nukta the Podcast
Changamoto zinazorudisha nyuma urejelezaji taka Tanzania
Ukosefu wa elimu ya udhibiti wa taka hasa plastiki, sera na sheria zinazosimamia mazingira zimetajwa na wadau wa mazingira kuwa zinaweza zikachelewesha safari ya kupunguza uharibifu wa mazingira hasa unaosababishwa na taka za plastiki.
2022-03-10
07 min
Nukta the Podcast
Chupa za plastiki za vinywaji vya kuongeza nguvu zinavyochocheo uharibifu wa mazingira
Kuzagaa kwa chupa za plastiki za rangi zinazotumika kuhifadhia vinywaji vya kuongeza nguvu katika mitaa mbalimbali nchini Tanzania hasa jijini Dar es Salaam kumeibua changamoto mpya ya kudhibiti uchafuzi wa mazingira. Licha ya chupa za maji kuokotwa kwa ajili ya kufanyiwa urejelezaji, chupa za rangi zimekuwa zikiachwa zikizagaa mitaani kwa sababu wenye viwanda hawazihitaji katika shughuli zao. Nini kinafanyika kudhibiti taka hizo? Herimina Mkude anaeleza kwa undani suala hilo.
2022-03-05
07 min
Nukta the Podcast
Magugu maji yanavyowatesa watumiaji wa Ziwa Victoria
Kuendelea kuwepo kwa magugu maji katika Ziwa Victoria kumeibua kadhia mbalimbali kwa watumiaji wa ziwa hilo wakiwemo wavuvi na wamiliki wa boti na meli kwa sababu hutanda katika eneo kubwa na kuzuia shughuli zao. Wanafanya nini kukabiliana nayo? Msikilize mtangazaji Herimina Mkude ambaye anatoa ufafanuzi zaidi.
2022-02-28
06 min
Nukta the Podcast
Simulizi ya Mtaa unaomezwa na maji ya Ziwa Victoria
Ni Mtaa wa Ziwa mkoani Mwanza ambao umeharibiwa huku nyumba za wakazi wake zikizama kwenye maji baada ya kina cha maji cha Ziwa Victoria. Kuongeza kwa kina cha maji cha ziwa hilo ni matokeo ya uchafuzi wa mazingira, mafuriko na mvua kubwa iliyonyesha mwaka 2020. Wadau wa mazingira washauri watu kuondoka katika mtaa huo huku wakihimiza watu kuacha kujenga au kufanya shughuli za kilimo na uzalishaji ndani ya mita 60 ya vyanzo vya maji ili kuepuka madhara. Kufahamu zaidi, sikiliza makala haya yanayoleta kwenu na Herimina Mkude.
2022-02-25
06 min
Nukta the Podcast
Mashaka ya maumbile yanavyozuia penzi la kweli
Kwa maringo na mikogo ya Roxanne, unaweza kuhisi ni wa kishua au ana kila kitu lakini huwezi amini, na urembo wake wote alionao, anadaiwa kodi ya pango na kila siku anakimbizana na mwenye nyumba.
2022-02-18
08 min
Nukta the Podcast
Filamu ya Brazen: Maandishi yanayomuwinda mwandishi wa vitabu
Filamu ya “Brazen” inamuhusu mwanamama Grace Miller ambaye ni nyota maarufu wa vitabu vya simulizi nchini Marekani ambaye maandishi yake yanaanza kugeuka uhaisiana kumuwinda.
2022-02-11
07 min
Nukta the Podcast
Kifahamu kisa cha kuumiza kinachoihusu kampuni ya Gucci
Patrizia anavutiwa na kijana mmoja anaekutana naye kwenye party hiyo. Unaweza kuelezea hisia alizo nazo kama mtu kupata msamaha wa deni la timiza au kuwa zamu katika kupokea hela ya kikoba. Bila shaka unajua hisia hizo.
2022-02-04
08 min
Nukta the Podcast
Filamu: Dunia inampatia mwanamfalme nafasi ya kuchagua kati ya nchi yake na huba.
Izzy anajikuta akivunja kibubu chake alichojitunzia kwa muda mrefu kwa ajili ya kusafiri sehemu mbalimbali duniani.
2022-01-28
07 min
Nukta the Podcast
Utafanya nini pale ndoto yako inapokuingiza matatani?
Siku moja Bom akiwa katika shughuli za kikazi, anaona wafanyakazi wenzie wawili wanapigana, lakini anaposogea kwa karibu anakutana na kitu tofauti. Mfanyakazi mmoja ametapakaa damu usoni na anapomtazama kwa karibu anagundua kuwa mtu huyo amebadilika na kuwa kama ‘Zombie’.
2022-01-21
08 min
Nukta the Podcast
Ifahamu filamu ‘inayotrend’ kwenye mitandao ya Kijamii Tanzania
Changamoto za mahusiano, malezi, umaskini na mategemeo zote zimeelezewa kupitia wahusika wanne: Tumaini, Angel, Stella pamoja na Rose.
2022-01-14
09 min
Nukta the Podcast
Safari ya ndugu waliopotezana kutafuta ukweli wa wazazi wao
Filamu hii inawahusu mabinti watano ambao kwa mara ya kwanza wanakutana katika moja ya hoteli iliyopo Cancun mjini Mexico.
2022-01-07
09 min
Nukta the Podcast
Kumpoteza mtu umpendaye ni mwanzo wa safari mpya
Filamu hii inamleta tena Buster Moon, mdau wa sanaa za maonyesho ambaye kutengeneza show ya muziki inayoweza kukusanya sayari zote ni kitu kidogo sana.
2021-12-31
08 min
Nukta the Podcast
A Naija christmas : Filamu ya kuchangamsha siku kuu yako.
Filamu hii inahusu familia ya Madam Agatha, singo mother mwenye vijana wa kiume watatu Chike, Obi, na Ugo.
2021-12-24
07 min
Nukta the Podcast
Filamu ya king’s affection: Majukumu yanavyobadilisha jinsia
Filamu hii inaturudisha nyuma enzi hizo wakati nchi ya Joeson haijaitwa Korea. Katika kipindi hicho, Mwana mfalme mteule au “crown prince” Anatarajia mtoto ambaye atakuja kurithi kiti cha enzi kama mfalme wa Joeson.
2021-12-17
06 min
Nukta the Podcast
Coming to America: Filamu maalum kwa watu wasiotaka kuvunja viapo
Ni filamu inayomhusu mfalme anayepaswa kwenda kinyume na mila na desturi zilizowekwa na watangulizi wake
2021-12-17
05 min
Nukta the Podcast
Itakuwaje ikiwepo sayari ya wanaume peke yao?
Ni filamu inayomhusu mwanadada ambaye anajikuta katika sayari iliyo na wanaume tu baada ya kupata ajali.
2021-12-10
04 min
Nukta the Podcast
Huyu ndiye mwanamke shujaa wa Afrika
Historia ya malkia huyu inatufanya turudi nyuma miaka 500 iliyopita, ambapo Amina akiwa ni ‘princess’ mdogo mwenye ujasiri na kipenzi cha baba yake.
2021-11-29
05 min
Nukta the Podcast
Filamu ya ‘Red Notice’: Kikulacho ki nguoni mwako
Filamu ya “Red Notice”, ipo kutukumbusha kuwa makini na wale wageni wanaogonga kwenye milango ya mioyo yetu na kutufanya tuone kuwa dhamira zao juu yetu ni za dhati.
2021-11-19
07 min
Nukta the Podcast
Filamu ya “No Time To Die”: Mashaka yaliyojaa majuto
Bahati ya mapenzi siyo ya wote, Wakati Adamu akikutana na Hawa kwa urahisi, wengine ni Samson wanaoishia na Delila. Samson wa leo ni James Bond almaarufu kama Agent 007.
2021-11-12
06 min
Nukta the Podcast
Pesa zilivyoweka rehani maisha ya vijana watano
Ni katika filamu ya Filamu ya the Army of Thieves inayohusu kikundi cha wezi waliobobea kuibia mabilionea
2021-11-05
05 min
Nukta the Podcast
“My Name” Filamu ya kuchangamsha wikiendi yako
Katika filamu hii ya “My name”, yaani jina langu, tunakutana na binti mrembo Yoo Ji Woo, ambaye katika maisha yake amekuwa akilelelewa na baba yake tu. Kwa jinsi baba yake alivyokuwa akimpenda sana, basi Jiwoo anaweza kujiita “dad’s daughter” kama vile wadada huwa wanajigamba. Maisha ya Jiwoo na baba yake siyo mazuri sana, kwani baba yake hakuwa na kazi rasmi ya kuwaingizia kipato zaidi ya kuwa mtu tuanayejihusisha na kazi haramu au tunaweza kumuita ‘gangstar’ Licha ya umaskini wao, maisha ya upendo na furaha yalikuwa ni kila kitu. Maisha ya Jiwoo yanakuja k...
2021-10-22
06 min
Nukta the Podcast
Mfahamu ‘single mother’ mpambanaji wa filamu ya Maid
Clean Bandit hawakukosea walipoimba kibao Cha Rockabye, ambacho kinaelezea jinsi single mothers wengi wanavyopambana kwa hali na mali ili kuwalea watoto wao.
2021-10-15
06 min
Nukta the Podcast
Wanawake na safari ya ushiriki maendeleo Kigoma
Ushiriki wa wanawake katika maendeleo ya kata zao umechangia kuwepo kwa huduma muhimu za kijamii ikiwemo shule.
2021-10-13
04 min
Nukta the Podcast
Wema unaosukuma maendeleo ya elimu Tanzania
Kutana na watu wanaochangia maendeleo ya elimu Mkoani Kigoma kwa kuwasaidia wanafunzi kuvuka mto ambao umekuwa kikwazo cha elimu Mkoani humo.
2021-10-13
03 min
Nukta the Podcast
Maisha ya ahueni baada ya Teleza
Teleza ni wahalifu waliokuwa wanajipaka mafuta mwilini au oili na kuwabaka wakina mama mkoani kigoma.
2021-10-12
03 min
Nukta the Podcast
Matumaini mapya baada ya ujenzi wa shule kukwama Kigoma
Endapo serikali itachelewa kukamilisha mradi wa shule hii, huenda ikachangia kwa wananchi kukata tamaa ya kujitoa kwenye shughuli za maendeleo.
2021-10-12
03 min
Nukta the Podcast
Utafanya nini iwapo hakuna anayekuamini tena?
Ni filamu ya “The Last Duel”, inayohusu kufa kwa uaminifu kati ya Marguerite na watu wake wa karibu
2021-10-08
06 min
Nukta the Podcast
Filamu ya The Squid Game: Tamaa mbele mauti nyuma
Uchambuzi wa filamu ya ‘The Squid Game’ inakukutanisha na watu wanaofanya maamuzi magumu baada ya maisha yao kutokuwa na ahueni kila uchao, huku mmoja wapo akiwa ni Gi-Hun. Hun ni mhusika mkuu katika filamu hii, ambaye maisha yake amekuwa akiyaendesha kwa ‘kuunga unga’ tu, huku kazi yake kubwa ikiwa ni kucheza kamali.
2021-10-01
04 min
Nukta the Podcast
Saa 24 za kummaliza rafiki aliyegeuka kuwa adui
Filamu ya Kate inamhusu mwanadada ambaye hajawahi kufaidi mapenzi ya baba na mama, kwani waliomleta duniani walifariki akiwa bado ni mtoto.
2021-09-24
08 min
Nukta the Podcast
Wananchi wanaopambana kuokoa maisha Geita
Ni kupitia ujenzi wa zahanati ambazo zitatumika kufanya matibabu ya wakazi wa mkoa huo.
2021-09-23
05 min
Nukta the Podcast
Wakazi wa Geita wanavyopambana na kung'oa ujinga
Kutana na juhudi za Wanageita wanavyopambana kung'oa ujinga kwenye mkoa wao
2021-09-23
05 min
Nukta the Podcast
Ushirikishwaji ulivyowainua wanawake Geita
Kutana na Rebecca Makenza, Mwanamke anayehamasisha ushiriki wa wanawake kwenye maendeleo.
2021-09-21
04 min
Nukta the Podcast
Ukatili wa kijinsia sokoni ulivyokomeshwa Dar
Ili kukomesha ukatili wa wanawake kwenye masoko, sheria zimetengenezwa ili kuadhibu yeyote anayefanya udhalilishaji wa kijinsia.
2021-09-21
02 min
Nukta the Podcast
Vita ya baba na mtoto inayoacha alama kwenye familia
Huzuni, hasira na majuto yanamfanya Wenwu kuchochea moto wa kisasi huku kuni yake akiwa ni mtoto wake , Shang Chi.
2021-09-11
07 min
Nukta the Podcast
Hulka ya upole inapobadilika kuwa umafia
Filamu hii ya “The Devil Judge” yaani hakimu shetani inakukutanisha na hakimu ‘mtata’ kuwahi kutokea katika ardhi ya wana filamu.
2021-09-06
07 min
Nukta the Podcast
Zahanati itakayookoa maisha ya maelfu ya wanawake, watoto Geita
Wakazi wa kijiji cha Isebya mkoani Geita wamejenga zahanati itakayopunguza vifo vya watoto na wajawazito wanaosafiri zaidi ya kilomita 5 kufuata huduma za afya kata ya jira ya Ilolungulu.
2021-09-03
05 min
Nukta the Podcast
Kisasi kinavyogeuka kuwa safari ya penzi jipya
Ni filamu ya The Protege, inamhusu mwanadada ambaye waovu wamemaliza familia yake.
2021-08-27
06 min
Nukta the Podcast
Penzi linavyovunja mnyororo wa maisha
Inamhusu mwanababa anayelazimika kubadili maisha yake baada ya mrembo kupita machoni kwake.
2021-08-06
05 min
Nukta the Podcast
The Suicide Squad: Filamu ya waovu wanaobaki tumaini dunia
Pale Superman anapokufa, ulimwengu unabaki bila shujaa wa kumtegemea. Lakini Afisa wa Intelijensia nchini Marekani, Amanda Waller anaishawishi Serikali kuridhia kutengenezwa kwa kikundi cha magaidi walioshindikana.
2021-07-30
05 min
Nukta the Podcast
Filamu ya safari ya kuutafuta mti unaofufua waliokufa
Kama ulimmiss The Rock na filamu zake za “adventure”, hii itakufaa. Ukiitazama, tupe mrejesho wa kiasi ulichofurahia.
2021-07-23
05 min
Nukta the Podcast
Filamu ya Black Widow: Sababu kwanini usikimbie matatizo yako
Baaada ya kumwona katika hadithi ambazo alikuwa tayari katika mafanikio, Natasha Romanoff sasa anakuja na historia yake katika filamu ya Black Widow.
2021-07-09
06 min
Nukta the Podcast
Hii ndiyo maana halisi ya rafiki: Filamu ya Luca
Safari ya marafiki wawili inapoingia vikwazo na vizingiti, havitoshi kukakatisha ndoto zao.
2021-07-02
07 min
Nukta the Podcast
Lupin II: Filamu inayoelezea mwanzo wa uhalifu wa kitanashati
Katika sehemu ya kwanza, mtoto wa Assane Diop, Raoul alitekwa na Leonard ambaye ni kibaraka wa bilionea Hubert Pellegrini ikiwa ni mtego wa kumvuta Assane katika umauti wake.
2021-06-25
05 min
Nukta the Podcast
Filamu: “Uongo” unapobaki tumaini la kuukomboa ulimwengu
Loki ambaye amecheza na mpangilio wa muda analazimika kulipia makosa yake lakini mambo yanageuka pale anapobaki tumaini pekee la ulimwengu.
2021-06-18
04 min
Yesaya Software Podcast
Nianzie wapi Kutengeneza Mifumo ya Kompyuta
Ebwana mambo vipi, jina langu ni Yesaya. Ninakukabirisha kwenye mfululizo wa vipindi kwa njia ya sauti yaani Podcast. Dhumuni langu ni kukuelimisha, kukuhabarisha na kukuletea mijadala mbalimbali kuhusu Teknolojia ya Habari na Mawasiliano - TEHAMA, na mimi nitajikita zaidi kwenye mifumo ya Kompyuta. Leo tutazungumza wapi utaanzia tengeneza mifumo ya kompyuta, watu wengi wamekuwa wakiniuliza namna gani wanaweza anza tengeneza mifumo ya kompyuta au lugha gani nijifunze ipi ni bora kuliko nyingine. Na wengine hushangaa mambo ninayopost kwenye mitandao ya kijamii na kuuliza hivyo vinini unaweka, jibu linaweza kuwa rahisi kuwa ni Code. Lakini kwa...
2019-01-06
05 min