podcast
details
.com
Print
Share
Look for any podcast host, guest or anyone
Search
Showing episodes and shows of
Stephen Kaaya
Shows
Kizazi Kipya Podcast
JUMA JIPYA #05: Kuurudisha uwezo wa kuamua mambo yako kwako
Katika Episode hii Stephen Kaaya amegusia kuhusu kuurudisha uwezo wako wa kuamua cha kufanya kwako, hasa pale unapo kuwa katika tukio ambalo ni la ghafla na hukulitaka. Itakua vyema sana ukichukulia matukio kama hayo kuwa ni fursa, fursa ya kurudisha uwezo wako; uwezo wa kuamua cha kufanya. Chukua fursa alafu twenzetu. Kwa mengi zaidi sikiliza Episode nzima pia tembelea instagram account; @kizazikipyapodcast .
2021-04-19
11 min
Kizazi Kipya Podcast
JUMA JIPYA #03: Tuliza Moyo
Karibu kwenye episode nyingine ya Juma Jipya Edition ambapo Stephen Kaaya amejaribu kuku kumbusha kutuliza moyo kwa kukumbuka wewe ni binadamu na kupunguza mwendo. Tunapo hisi kama kuna uzito ndani, kama huwezi kuendelea, unapata hisia nyingi kwa wakati mmoja na unashindwa kuelewa ufanye nini, kama unajisikia kushindwa na kukata tama. Ni sawa, ni sawa kabisa, wewe ni binadamu na changamoto ni sehemu ya kukua, changamoto ni sehemu ya hatua zitazo kusaidia kusonga mbele. Inawezekana kuzitumia vizuri.
2021-03-04
14 min
Kizazi Kipya Podcast
JUMA JIPYA #02: Simamia Ukweli Wako
Kwenye episode hii ya Juma Jipya Edition ya Kizazi Kipya Podcast Stephen Kaaya amejaribu kuku kumbusha kusimama tena na kuwa wewe kikamilifu, kuusikiliza ule msukumo ulio ndani yako, ule msukumo wa kujikubali na kuusimamia ukweli wako. Simama, uusimamie, hata kama ikikubidi kufanya hivyo peke yako, sawa!! Ikikubidi kutembea peke yako huku ukiamini huo ni ukweli wako na unafanya hivyo kwa upendo ni jambo zuri na la heri kuliko kufuata mkumbo.
2021-03-01
09 min
Kizazi Kipya Podcast
JUMA JIPYA #01: Tunavyo Anza 2021
Katika episode hii ya Juma Jipya edition Stephen kaaya amejaribu kuku kumbusha kuwa katika kila mipango tuliyo jiwekea ili tuikamilishe mwaka huu wa 2021 ni muhimu kuwa na misingi imara ambayo ni kwanzia sababu ya kufanya ulilopanga au unalo panga sasa, kiasi cha muda na nguvu utazo tumia kwenye jambo hilo, utayari wako juu ya changamoto zake na la muhimu zaidi ni litakusaidia vipi wewe kupiga hatua yaani kuwa bora zaidi, siyo zaidi ya mwingine bali zaidi ya wewe uliye kuwa mwaka jana.
2021-03-01
12 min
Kizazi Kipya Podcast
TRAILER
Kwenye episode hii utakua na Stephen Kaaya akikuelezea kuhusu Kizazi Kipya Podcast kwanzia mwanzilishi na mtayarishaji wake, hadithi ya maisha yake kwa ufupi na nini kilimpelekea kuanzisha KKP, pia natakuelezea mambo ambayo yatakuwa yakiongelewa kwenye hii podcast.
2021-03-01
11 min
Kizazi Kipya Podcast
JUMA JIPYA: 2020, Niliyo jifunza.
Katika Juma Jipya Edition hii ambayo ni kama episode maalum Stephen Kaaya amejaribu kuongelea mambo matano ambayo amejifunza hadi sasa katika mwaka 2020.Mambo hayo ni:-1. Siyo kuhusu unacho sema kuwa ni sahihi bali ni kuhusu unacho fanya. 2. Kasi yangu ni ile inayo niacha nikiwa na amani moyoni 3. Changamoto zinakuja kunionyesha upande mwingine wa jambo. 4. Kadiri unavyo lazimisha ndiyo kitavyo kuangusha zaidi. 5. Kupiga hatua na kuweka mipaka siyo jambo rahisi hasa ukiwa katika mazingira ya awali.
2020-12-14
25 min
Kizazi Kipya Podcast
JUMA JIPYA: Msukumo wa kupiga hatua na kusonga mbele.
Kwenye hii episode ya kizazi kipya podcast juma jipya edition, nimejaribu kugusia kuhusiana na kupiga hatua na kusonga mbele katika kujikubali jinsi tulivyo na katika kufanya mambo mengine pia. Tutapo weza kujikubali na kujiona kuwa tupo sawa jinsi tulivyo then tusonge mbele kwa mwendo wetu manake tumeweza kuangalia yale yote tuliyo pitia yawe ya kutisha, kuhuzunisha na kufurahisha kwa upendo na kwamba yamechangia kuwa hapa tulipo leo. Mtayarishaji ni Stephen Kaaya. Nashukuru kwa kuwa hapa.
2020-09-28
38 min
Kizazi Kipya Podcast
JUMA JIPYA: Moyo wa kujichagua wewe kwanza.
Katika episode hii ya Juma Jipya Edition Stephen Kaaya ame jaribu kukukumbusha kujichagua wewe kwanza, na ni kwa kuanza kutengeneza maana ya mambo mbali mbali yanayoendelea mashani mwetu ili pale tutapo anza kusikiliza nini kipo ndani yetu tupate maana zilizo za kwetu zenye tafsiri yetu, ya kipekee na salama kwetu. Tembelea akaunt Kizazi Kipya Podcast iliyopo Instagram kupata jumbe nzuri.
2020-09-14
23 min
Kizazi Kipya Podcast
JUMA JIPYA: Wewe ni Expert.
Karibu sana kwenye Juma Jipya Edition ya Kizazi Kipya Podcast na mtayarishaji ni Stephen Kaaya. Kwenye hii episode nakukumbusha kuwa wewe ni expert simply because umevuka mengi na umepita kwingi. Kwa lolote unalopitia na yatakayo kuja utavuka kwa sababu umekuwa katika mazingira ya namna hiyo mara nyingi sana. WEWE NI EXPERT Kwa mengi zaidi tembelea www.kizazikipya.online.
2020-08-24
27 min